FT: Ligi Kuu Bara: Yanga 1-0 Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa, 4/12/2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Full Time, Yanga inashinda 1-0.
Fei Toto anaipatia Yanga goli
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
88' Yanga wanapanga mashambulizi kutafuta goli la ushindi
87' Shambulizi kali kwa Prisons lakini mpira unatoka juu ya lango
85' Shuti kali langoni kwa Yanga, kioa Diarra anafanya kazi nzuri inakuwa kona
80' Prisons wanafanya shambulizi kali lakini wanakosa umakini
79’ Azizi Ki anafanya shambulizi lakini kipa anawahi kudaka mpira
77’ Shuti la Fei Toto linambabatiza beki na kuwa kona
75’ Morrison anaingia, anatoka Clement
70’ Yanga wanaendelea kupush mashambulizi
62' Prisons wanapata nafasi lakini hawaitumii vizuri
60' Yanga wanapata kona nyingine
60' Shuti kali la Fei Toto linapanguliwa kuwa kona
57’ Yanga wametawala mchezo tangu kuanza kwa kipindi cha pili
55’ Yanga wanapata kona ya 11, Prisons wana kona 1
50’ Kiungo wa Yanga, Aucho anapata njano kwa kucheza faulo

Kipindi cha pili kimeanza

MAPUMZIKO

45' Kipindi cha kwanza kimekamilika, matokeo ni 0-0
42' Shuti la Fei Toto linapanguliwa na kipa na kuwa kona
38' Timu zote zinashambuliana kwa zamu
30' Kasi ya mchezo imepungua kiasi tofauti na ilivyokuwa awali
22' Prisons wanaonekana kuamka
19' Prisons wamejibu mapigo, wamefanya shambulizi kali ikawa kona
13' Bado mambo ni magumu kwa Prisons, muda mwingi wanashambuliwa wao
11' Mashambulizi mengi yameelekea langoni kwa Prisons
6' Kipa wa Prisons anafanya kazi nzuri kuokoa mpira uliokuwa unaingia wavuni kwake
3' Yanga wanafanya shambulizi kali, mpira unatoka inakwa kona
Mchezo umeanza kwenye Uwanja wa Mkapa

FjJGNqWWYAIxA-A.jpg

Kikosi cha Yanga

Prisons.jpg

Kikosi cha Tanzania Prisons

Kabla ya mchezo kuanza, mashabiki wa Yanga wamepata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wakisherekea kucheza mechi 49 za Ligi Kuu Bara bila kupoteza hata mchezo mmoja, ikumbukwe walipoteza wiki iliyopia dhidi ya Ihefu kwa mabao 2-1.

FjJCh4ZXwAA4cYA.jpg

Msanii G-Nako

Huu ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga inahitaji kupata ushindi ili kurejea kileleni katika msimamo wa ligi hiyo, Prisons wenyewe ushindi ni muhimu kwa kuwa utawapa nafasi ya kurejea katika nafasi za kati ili kukwepa kushuka daraja.
 
Huyu refa ana uwezo mkubwa ku- officiate mpira kuliko Yale ma-idiot wengine wa kiume
 
Hii jezi ya Yanga nini kimetokea mpaka nikaiona tena ikitumika?, ninakumbuka imepigiwa kelele hapo nyuma
 
Akishinda sana ni draw, hap ni either yanga apoteze au prison ashinde
 
Wachezaji wa Yanga wanatakiwa kuonesha utulivu, na pia ukomavu. Kidogo kidogo wanaingia kwenye mfumo wa Tanzania Prisons, jambo ambalo ni hatari sana.

Mechi hii inatakiwa kumalizika kwa ushindi wowote ule kwa Wananchi! Na siyo kwa sare, au kufungwa tena na timu vibonde kutoka Mbeya.
 
Wachezaji wa Yanga wanatakiwa kuonesha utulivu, na pia ukomavu. Kidogo kidogo wanaingia kwenye mfumo wa Tanzania Prisons, jambo ambalo ni hatari sana.

Mechi hii inatakiwa kumalizika kwa ushindi wowote ule kwa Wananchi! Na siyo kwa sare, au kufungwa tena na timu vibonde kutoka Mbeya.
Sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom