FT: Fainali, Mapinduzi Cup: Mlandege 2-1 Singida Big Stars

leadermoe

R I P
Feb 15, 2017
1,392
4,573
Hatimaye leo hii Fainali ya Mapinduzi Cup inaenda kupigwa kumtafuta Bingwa mpya msimu huu ambapo ni kati ya Singida Big Stars dhidi ya Mlandege kutoka Zanzibar majira ya saa 2:15 usiku.

Singida wameingia hatua hii ya fainali baada ya kuitungua Azam FC kwa mabao 4-1 na kuingia hatua hii kwa mara ya kwanza baada ya kupanda daraja msimu huu akiwa na kikosi cha wachezaji wenye uwezo mkubwa.

Wakati kwa upande wa Mlandege yeye ameingia hatua hii ya fainali mara baada ya kumtoa Namungo kwa matuta na kutaka kubakiza Kombe hilo nyumbani kwao ambalo hawajalipata kwa muda mrefu.

Hans Pluijm anatarajia kunyakua Kombe hilo kutokana na kuwa na ubora wa kikosi alionao na usajili wa wachezaji alioufanya akiwemo Francy Kazadi aliyefunga hat trick mechi iliyopita na kuwaondoka Mabingwa mara nyingi wa kombe hili.

Lakini je, ataweza mbele ya Mlandege aliyemtoa Simba na Namungo?. Lakini pia toka Kombe hili lianzishwe timu kutoka visiwani Zanzibar ni moja tu ambayo iliweza kutwaa Ubingwa wa Kombe hili.

Leo hii inawezekana ikashuhudiwa mechi bora kabisa ya Fainali ambayo inazikutanisha timu mbili ambazo kila moja ikiwa na uchu wa kuchukuataji hili.

========

MLANDEGE BINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI 2023

Timu hiyo imetwaa ubingwa baada ya kuifunga Singida Big Stars magoli 2-1 katika fainali iliyopigwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
-
Magoli ya washindi yamefungwa na Bashima Saite dakika ya 7 na Abdulnassar Mohamed dakika ya 19 wakati lile la Singida mfungaji ni Francy Kazadi dakika ya 51.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa timu kutoka Zanzibar kutwaa ubingwa huo tangu ilivyotokea Mwaka 2009.
 
Back
Top Bottom