FT: Dodoma Jiji 0-2 Yanga / Uwanja wa Jamhuri / Dodoma / Ligi Kuu Bara

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,302
5,441
Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC, leo Jumapili Mei 15, 2022, Yanga watakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Jamhuri kucheza dhidi ya Dodoma Jiji FC Mkoani Dodoma.

Ikumbukwe kuwa Yanga haijapata bao hata moja katika mechi tatu zilizopita mfululizo katika Ligi Kuu Bara, presha kubwa ipo pia kwa mshambuliaji wao Fiston Mayele ambaye ameshafung mabao 12 hadi sasa akiwa mmoja wa vinara wa mabao msimu huu.

Kikosi cha Yanga kinachoanza katika mchezo wa leo Mei 15, 2022


281141070_333193078928931_2402279377489133133_n.jpg

Kikosi cha Yanga

Dodoma Jijii.jpg

Kiosi cha Dodoma Jiji FC​


KOCHA YANGA AFUNGUKA
Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema kucheza mechi mfululizo ndani ya muda mfupi, kulifanya wachezaji wawe na uchovu, lakini suala la ubingwa lipo mikononi mwao, kilichobaki ni wao kukamilisha michezo licha ya kutoshinda mechi tatu mfululizo.

Kuhusu Mayele amesema kukosa penati ni bahati mbaya hata wachezaji wakubwa wanakosa, akizungumzia kikosi kuwa na mabadiliko katika mchezo wa leo amesema imetokana na uchovu wa baadhi ya wachezaji ili miili yao ikae vizuri, na wana imani kuwa wakiingia kutokea benchi inaweza kuwasaidia.

NENO LA DODOMA JIJI
Kocha Msaidizi wa Dodoma Jiji, Mohamed Muya amesema wanaiheshimu Yanga lakini wanaingia uwanjani kwa ajili ya kupambana.

Kuhusu kukabiliana na Mayele ambye amekuwa hatari msimu huu amesema Yanga wana wachezaji wazuri, hivyo mipango yao siyo kumdhibiti Mayele pekee bali wachezaji wote.

----------------
Timu zinaendelea kupasha misuli.

Timu zimeshaingia uwanjani, mashabiki ni wengi uwanjani, mchezo unaweza kuanza muda wowote kuanzia sasa.

Mchezo umeanza

1' Mchezo umeanza na Dodoma Jiji FC wanatoa mpira nje.
2' Yanga wanapata kona, inapigwa lakini walinzi wa Dodoma wanaokoa
4' Mchezo bado haujashika kasi, timu zote ni kama zinazomana.
6' Dodoma wanafanya shambulizi kali lakini walini na kipa wa Yanga wanakuwa makini kuondoa hatari
10' Kasi ya mchezo inaanza kuongezeka pande zote zinaongeza kasi
11' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dickson Ambundo anafunga bao kali kwa shuti la mbali kutoka nje ya 18
12' Yanga wanafanya shambulizi lingine lakini walinzi wanaokoa
16' Timu zote zimeotea mara moja
17' Cleophance Mkandala wa Dodoma anaumia na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake inachukuliwa na Khamisi Mcha
23' Dodoma wanapata faulo karibu na lango la Yanga, Mcha anapiga mpira unadakwa na Diarra
26' Yanga wanaongeza kasi ya kushambulia
29' Djuma Shaban anapata kadi ya njano kwa kupishana lugha na mwamuzi
30' Dodoma Jiji wanapata nafasi ya wazi lakini kichwa cha Anwary anapiga mpira unatoka nje
35' Yanga wanaongeza kasi ya mchezo
35 GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Yanga wanapata bao la pili, kipa Yusuph anajifunga, anapangua shuti la Mauya kisha katika kuokoa anausukuma ndani ya lango lake.
45' Mapumziko, Yanga wanaongoza mabao 2-0

KIPINDI CHA PILI

Kipindi cha pili kimeanza
46' Mchezo umeanza kwa kasi ndogo
50' Dodoma wanafika langoni kwa Yanga lakini hawana madhara
58' Djuma anapata nafasi ya kufunga lakini shutilake linakosa nguvu
60' Yanga wanapata kona, inaokolewa.
65' Shambulizi kali langoni mwa Dodoma lakini wachezaji wa Yanga wanakosa umakini
70' Kipa wa Yanga, Diarra anafanya kazi kubwa kuokoa hatari langoni kwake
73' Kasi ya mchezo imepungua kiasi
77' Yanga wanafanya mabadiliko, Bangala na Denis Nkane wanaingia kuchukua nafasi za Fei Toto na Moloko
79' Yanga wanafanya shambulizi kali, mpira unagonga nguzo na kurejea uwanjani
85' Ambundo wa Yanga anatoka, nafasi yake inachukuliwa na Farid Mussa
88' Mayele anatoka anaingia Makambo kwa upande wa Yanga
90' Zinaongezwa dakika 4

FULL TIME
 
Kila la kheri Yanga African..
Makolo tunawaomba sana nje mcomment huu Uzi maana nyie ndio mnaongezea sisi Yanga spirit ya Mapambano..
Njooni Makolo maana m atamani tufungwe au tudraw Ila Leo mtafungwa wote.
 
Back
Top Bottom