FT: CAF Champions League | Raja Casablanca 3-1 Simba S.C | Stade Muhammed V | 01.04.2023

mwarabu feki

JF-Expert Member
Feb 16, 2023
682
1,461
Kuna watu wamedandia mtumbwi wa vibwengo
uchambuzi utafata baadae

Stay tuned,...................
raja.jpg

kUHOnpoQgVggxqGLVi6S.jpg

==========

Kikosi cha Simba
Fsk647wWwAIwTS7.jpg

Kikosi ch Raja Casablanca
Raja.jpg
Mchezo umeanza
2’ Mashabiki wa Raja wameanza kuonesha presha kwa kushangilia kwa nguvu
4’ Wenyeji wakigusa mpira wanakuwa nakasi kubwa
6’ Raja wanapata kona ya kwanza, inapigwa inaokolewa
10’ Timu zote hazina utulivu, wenyeji wakionekana kutsks goli la mapema
16’ Raja almanusura wapate goli, mpira unagonga nguzo na kutoka nje
17’ Shambulizi lingine kali langoni kwa Simba, mpira unatoka nje
22’ Simba wanacheza pasi kuanzia nyuma, shuti la Saido linapaa
24’ Mzamiru anapiga shuti linatoka nje la lango
27’ Timu zinapeana zamu kumiliki mpira
29’ Shuti la Gadiel linaoaa juu ya lango la Raja
33' Baleke anaweka mpira wavuni lakini mwamuzi anasema alicheza faulo
36' Chama wa Simba anapata kadi ya njano
43' GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Khabba anafunga goli baada ya Onyango kuchanganyana na Manula wakati wa kuokoa
45' Walinzi wa Simba wamecheza vizuri lakini wameanza kufanya makosa kadhaa

MAPUMZIKO

Kipindi cha pili kimeanza
46' Wenyeji wameanza kwa kasi ya chini
48’ GOOOOOOOOOOOO
Baleke anafunga bao na kuisawazishia Simba
55' Simba wanapiga pasi kadhaa na kuonesha kujiaminia
57' Manula yuoo chini baada ya kuumia, anapatiwa matibabu
62' Kibu Denis anachezewa faulo karibu na eneo la 18 la Raja
69' Onyango anacheza faulo, inakuwa penati kwa Raja
Goooooooooo Hamza Khabba anafunga goli ka pili kwa penalti
71' Shangwe linaendelea kwa mashabiki wa Raja
goooooo
Mohamed Boulacsout anafunga goli la tatu kwa Raja
89' Kapombe kaumia, ametoka nafasi imechukuliwa na Israel
89' Saido katoka kaingia John Bocco
90' Zimeongezwa dakika 4

FULL TIME
 
Back
Top Bottom