From Karimjee Hall: Public Hearing ya Kamati ya Bunge toka kwa wadau wa Dar es Salaam

Jaji Warioba amemaliza, Prof. Lipumba ndio yuko ulingoni. Atafuatiwa na James Mbatia wa NCCR-Mageuzi.
 
Prof. Lipumba ameanza kwa kuuchana kuanzia jina la Muswada, uandikwe kwa lugha ya Kiswahili sanifu na fasaha ili kila Mtanzania auelewe. Uitwe ni Muswada wa Katiba Mpya na sio marekebisho ya katiba kama ulivyo sasa!.
 
Prof. Lipumba ameuchekesha ukumbi aliposema wananchi waruhusiwe kujadili urais, kama wanataka Sultani, waseme, kama wanamtaka Sultani Kikwete, amridhishe usultani mwanae Ridhiwani waachwe waseme.
 
Prof. Lipumba amemaliza kuwa kuuchana chana muswada, na kuomba serikali iache mzaha kwenye mambo muhimu ka,ma haya ya katiba, hivyo ni mwanzo mbaya. Sasa amepanda ulingoni James Mbatia.
 
James Mbatia ameanza kwa kusema, muswada huu, haukuletwa kwa nia njema. Amesema Watanzania wanataka Katiba Mpya na sio marekebisho ya katiba. Tunataka katiba mpya hatutaki viraka kwenye katiba yetu.
 
JAMANI NI NANI HUYO AWAYE NA NGUVU HATA YA KIIBILISI AU VIJISENTI HATA AKATUMIA NGUVU HIYO KUSHINDA AZMA MURUWA WA 'NGUVU YA UMMA KATIKA NCHI?????????????????

Duu, kama Jaji wangu mwenyewe Sinde Warioba yuko ndani ya nyumba Mhe Tundu Lissu aka Lissu Mtundu Kibano cha Mafisadi basi sasa mambo poa sanaaaaaaaaaaaaaaa!!!!

Mafisadi hapo Karimjee TUNAKUJA KUWASHIA tupendavyo sie Nguvu ya Umma, hakuna matani tena. Kule kwa Baba Moi mlikoenda kudesa mambo ya kudhoofisha azma yetu kupata katiba (Mzee Msekwa na kamati yake ya siri) na pia zile zenu za KICHINA CHINA KUKODI AL-SHAABAB kwa kote Nairobi na Dar es Salaam; tayari file kama hiyo mliyopewa nakala tunayo na picha za wahusika pia.

Ni 'bomu' zito kisiasa ambayo sehemu yake ndogo nilishailipua humu kuhusu Copy and Paste ya Muswada mzima kwa kubadilisha tu jina na kuingiza JMT. Na zile mbinu chafu zaidi mlizozipewa mkithubutu kuzitumia basi mjue mkanda mzima utakwepo tambarare hapa JF na kwingineko.

People'Power na Maslahi ya Taifa mbeeeeeeeeeeeeeeeeellllllllllleee kama tai jaama!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Amesema utaratibu huu wana cut and paste kutoka mchakato wa Kenya, mazingira yetu sio kama Kenya, wao ni Jamuhuri tuu, wakati sisi ni Jamuhuri ya Muungano, hivyo ni vitu viwili tofauti
 
NCCR Mageuzi wamesema wao hawaitaki kabisa hiyo Tume ya rais, bali wanataka Bunge litunge sheria ya kuunda Baraza la Kutunga katiba, na baraza hilo ndilo liunde tume ya kukusanya maoni ambapo rais has nothing to do na katiba mpya.
Mbatia amemaliza, anafuatia Mzee kijana wa APPPT-Maendeleo, Peter Kuga Mziray.
 
Mziray ameanza kwa kusema, tunataka referendum na sio constituent assembly. Anataka wananchi wenyewe wasema na sio kutumia wawakilishi.
Namuona Mziray kama mtu wa anayeongea kwa mizaa, vichekesho vingi, huku akijisifu kila dakika, amesema tume ya taifa ya uchaguzi ivunjiliwe mbali, kwani mpaka sasa, hajui alishinda kwa kura ngapi.
Amemaliza na sasa anazungumza Mwanasheria, Gideon Mendes, mwenye ulemavu wa kutoona.
 
Mendes, amesema, muswada umewasahau watu wenye ulemavu, hawajatajwa popote. Amesema Tanzania ina asilimia 10 ya watu wenye ulemavu. Hivyo wajumbe wa tume ya kukusanya maoni, pia ijumuishe asilimiua 10 ya watu wenye ulemavu
 
Mendes amesema watu wenye ulemavu, hawapendelei nafasi za upendeleo kwa wanawake, bali nafasi za upendeleo, zingekuwa kwa watu wenye ulemavu. Amemuomba radhi mwenyekiti ambae ni mwanamke.
 
Awali, by the time naingia hapa Karimjee, wanasheria toka Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora, pamoja na wale wa Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu, waliuchana chana muswada mzima, kufungu kwa kifungu na kuuacha ....bila nguo zozote za kuusetiri, wao walibomoa mwanza, mwisho.
 
Mwanasheria Mendes, anaendelea kutetea kuwepo kwa vifungu vya haki za walemavu kwenye katiba.
 
Nzidi kuona watu humu ndani. Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji John Tendwa yuko ndani ya nyumba, huyu pia ni mzee wa vichekesho.

Mendes amemamilizia kwa kusema mchakato hauna time frame, unaweza kuendelea bila mwisho.

Maoni ya watu wa kawaida sasa ndio yaanza kukusanywa
 
Back
Top Bottom