1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 6,255
- 7,931
Wachumi wanatudanganya sana sana kwa kufuata vigezo vya nchi zao na vigezo vyao.Tunasu
Mkuu uchambuzi wako uko poa kabisa,kigezo mojawapo cha kuonyesha ufukara wa nchi ni kwa kuangalia idadi ya wananchi walio kwenye lindi la umaskini ukilinganisha na hao wenye neema waliojenga nyumba nzuri mkuu.Kama sikosei zaidi ya asilimia hamsini ya wanachi wa tanzania wako kwenye kundi la maskini wa kutupwa yaani wanaishi chini ya kiwango cha dola mbili kwa siku.Jpm anachotakiwa kufanya ni kupunguza hili kundi la wanaoishi kwenye umaskini na ndio atasifika haswa ,
Watanzania ni matajiri sana.
Kule shinyanga kuna Msukuma ana Ng'ombe laki moja.
Ngombe laki moja kwa bei ya sh. 500,00/- ni sawa na Jumla ya bil. 50. Eti huyu naye wanamweka kwenye kundi la watu wanaoishi Chini ya dola moja kwa siku wakati anaiwezo wa kula ng'ombe mmoja kila siku kwa miaka 33.
Kwa wafugaji ambao kwa Tanzania ni jamii kubwa sana ya watu wasiopungua mil. 15 ukianzia Dodoma,Arusha ,Manyara, Singida ,Shinyanga,Mwanza, Shimiu,Geita n.k mtu kumiliki ng'ombe 50 kwa kiwango cha chini kabisa ni jambo la kawaida. Lakini cha ajabu viongozi wetu wanashindwa kuwapa elimu namna ya kujitambua kuwa wao sio maskini MTU anakuja na kuwaaminisha kuwa wao ni maskini wanahitaji elimu bure na misaada kibao toka kwa wanasiasa.Wanawageuza kuwa ombaomba na kuamini kuwa wao ni maskini kwa sababu hawajaajiriwa na mtu mwingine kuajiriwa.
Kundi lingine ni la wakulima wanaotokea mikoa yenye ardhi kubwa yenye Rutuba kama Mtwara,Ruvuma,Iringa ,Morogoro, Rukwa, Katavi, Mbeya ,Tanga hasa maeneo ya Lushoto ambao Masaa 24 FUSO zinasomba vyakula kupeleka DSM . Hao nao wanaitwa maskini wasio na uwezo wa kula Milo miwili.
Mikoa kama ya Kilimanjaro , Kagera na Tabora wao wanategemea mazao ya wakoloni kama Tumbaku na Kahawa. Lakini hata hivyo wale waliotumia mazao hayo vizuri wakati wa bei nzuri walisomesha watoto wao na wakabadili mifumo yao ya maisha kuwa ya kigeni.
Mwaka Juzi na mwaka Jana Kule Mtwara na Lindi walipata sana Korosho na bei ilikua nzuri lakini chaajabu watu wengine walijenga mpaka nyumba za bati la msauzi . Yani hao tatizo pia ni matumizi ya maarifa kukabiliana na ugumu wa maisha lakini mali wanazo.
Kuna Vijana wengi Kule Moshi na Mirerani wanapata pesa kwa kazi za madini na Kubeba mizigo ya watalii lakini wakishapata fedha wanakimbilia kwenye Pombe mpaka wanaoga na kufua nguo zao kwa Bia. Hawa nao wanaisubiri serikali iwawezeshe ili wapate Milo miwili kwa siku.
Nilikwenda kijijini Mwaka 2014 karibu kila nyumba ina mtu moja au wawili wanaomiliki gari na nyumba nzuri huko mijini. Unapotathimini utajiri unaomilikiwa na watanzania wenyewe kuanzia nyumba,magari , mifugo,mashamba na vitalu vya madini na mitumbwi ya kuvulia samaki huko ziwani na baharini utagundua kuwa ni utajiri mkubwa sana ukilinganisha na idadi ya watu . China watu wengi wanakaa nyumba za umma na kwenye vimitumbwi na vijumba vya mbao.
Hata nchi za magharibi wengi wanaishi nyumba za umma. Ni aina ya mfumo waliouona unawafaa. Mifumo yetu ya asili ya kumiliki Mali wao wanaona ni umaskini.