From Hyatt Regency, The Kilimanjaro: the 2nd Tanzania Oil & Gas Congress. Wazungu Wengi Kuliko Wenyeji!

1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,170
2,000
Tunasu

Mkuu uchambuzi wako uko poa kabisa,kigezo mojawapo cha kuonyesha ufukara wa nchi ni kwa kuangalia idadi ya wananchi walio kwenye lindi la umaskini ukilinganisha na hao wenye neema waliojenga nyumba nzuri mkuu.Kama sikosei zaidi ya asilimia hamsini ya wanachi wa tanzania wako kwenye kundi la maskini wa kutupwa yaani wanaishi chini ya kiwango cha dola mbili kwa siku.Jpm anachotakiwa kufanya ni kupunguza hili kundi la wanaoishi kwenye umaskini na ndio atasifika haswa ,
Wachumi wanatudanganya sana sana kwa kufuata vigezo vya nchi zao na vigezo vyao.

Watanzania ni matajiri sana.

Kule shinyanga kuna Msukuma ana Ng'ombe laki moja.
Ngombe laki moja kwa bei ya sh. 500,00/- ni sawa na Jumla ya bil. 50. Eti huyu naye wanamweka kwenye kundi la watu wanaoishi Chini ya dola moja kwa siku wakati anaiwezo wa kula ng'ombe mmoja kila siku kwa miaka 33.

Kwa wafugaji ambao kwa Tanzania ni jamii kubwa sana ya watu wasiopungua mil. 15 ukianzia Dodoma,Arusha ,Manyara, Singida ,Shinyanga,Mwanza, Shimiu,Geita n.k mtu kumiliki ng'ombe 50 kwa kiwango cha chini kabisa ni jambo la kawaida. Lakini cha ajabu viongozi wetu wanashindwa kuwapa elimu namna ya kujitambua kuwa wao sio maskini MTU anakuja na kuwaaminisha kuwa wao ni maskini wanahitaji elimu bure na misaada kibao toka kwa wanasiasa.Wanawageuza kuwa ombaomba na kuamini kuwa wao ni maskini kwa sababu hawajaajiriwa na mtu mwingine kuajiriwa.

Kundi lingine ni la wakulima wanaotokea mikoa yenye ardhi kubwa yenye Rutuba kama Mtwara,Ruvuma,Iringa ,Morogoro, Rukwa, Katavi, Mbeya ,Tanga hasa maeneo ya Lushoto ambao Masaa 24 FUSO zinasomba vyakula kupeleka DSM . Hao nao wanaitwa maskini wasio na uwezo wa kula Milo miwili.

Mikoa kama ya Kilimanjaro , Kagera na Tabora wao wanategemea mazao ya wakoloni kama Tumbaku na Kahawa. Lakini hata hivyo wale waliotumia mazao hayo vizuri wakati wa bei nzuri walisomesha watoto wao na wakabadili mifumo yao ya maisha kuwa ya kigeni.

Mwaka Juzi na mwaka Jana Kule Mtwara na Lindi walipata sana Korosho na bei ilikua nzuri lakini chaajabu watu wengine walijenga mpaka nyumba za bati la msauzi . Yani hao tatizo pia ni matumizi ya maarifa kukabiliana na ugumu wa maisha lakini mali wanazo.
Kuna Vijana wengi Kule Moshi na Mirerani wanapata pesa kwa kazi za madini na Kubeba mizigo ya watalii lakini wakishapata fedha wanakimbilia kwenye Pombe mpaka wanaoga na kufua nguo zao kwa Bia. Hawa nao wanaisubiri serikali iwawezeshe ili wapate Milo miwili kwa siku.
Nilikwenda kijijini Mwaka 2014 karibu kila nyumba ina mtu moja au wawili wanaomiliki gari na nyumba nzuri huko mijini. Unapotathimini utajiri unaomilikiwa na watanzania wenyewe kuanzia nyumba,magari , mifugo,mashamba na vitalu vya madini na mitumbwi ya kuvulia samaki huko ziwani na baharini utagundua kuwa ni utajiri mkubwa sana ukilinganisha na idadi ya watu . China watu wengi wanakaa nyumba za umma na kwenye vimitumbwi na vijumba vya mbao.

Hata nchi za magharibi wengi wanaishi nyumba za umma. Ni aina ya mfumo waliouona unawafaa. Mifumo yetu ya asili ya kumiliki Mali wao wanaona ni umaskini.
 
french

JF-Expert Member
Aug 2, 2017
3,341
2,000
Final Updates.
Mkutano umemalizika, kwa vile umeendeshwa kwa lugha ya Kiingereza, nitawawekea baadhi ya presentations.
Ila pia nimefanya interviews za one on one na watu wafuatao kuhusu hoja mbalimbali za mafuta na gesi.
 1. Waziri wa Nishati na Madini, Dr. Kalemani kuhusu policy issues
 2. Waziri wa Mazingira, January Makamba atatoa Statement ya Waziri Mkuu.
 3. Waziri wa Nishati wa SMZ
 4. Waziri wa Nishati wa Uganda.
 5. Mkurugenzi Mkuu wa TPDC kuhusu ugawaji vutalu vya gesi kwa wazawa
 6. Mkurugenzi Mkuu wa TIC kuhusu mazingira ya uwekezaji Tanzania kwenye sekta ya mafuta na gesi
 7. Mkurugenzi Mkuu wa PURA, hawa ni regulator wa Upstream
 8. Mkurugenzi wa Ewura, hawa ni regulator wa Downstream
 9. Mkurugenzi Mkuu wa EPZA kuhusu mchango wa gesi kwenye EPZ.
 10. Mkurugenzi Mkuu wa Bandari kuhusu uwezo wa bandari zetu kuihudumia sekta ya mafuta na gesi.
 11. Mwakilishi wa Exinox kuhusu uwekezaji kwenye sekta ya gesi
 12. Mwakilishi wa Shell, walioinunua BG.
Ambao nitawaleta kwa awamu awamu.
Asanteni kwa kuufuatilia mkutano huu
Paskali
Ni equinor mkuu sio exuinox. Equinor ilikuwa statoil. Ni kampuni ya norway. Au labda unamaanisha kampuni nyingine
 
Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,399
2,000
Wachumi wanatudanganya sana sana kwa kufuata vigezo vya nchi zao na vigezo vyao.

Watanzania ni matajiri sana.

Kule shinyanga kuna Msukuma ana Ng'ombe laki moja.
Ngombe laki moja kwa bei ya sh. 500,00/- ni sawa na Jumla ya bil. 50. Eti huyu naye wanamweka kwenye kundi la watu wanaoishi Chini ya dola moja kwa siku wakati anaiwezo wa kula ng'ombe mmoja kila siku kwa miaka 33.

Kwa wafugaji ambao kwa Tanzania ni jamii kubwa sana ya watu wasiopungua mil. 15 ukianzia Dodoma,Arusha ,Manyara, Singida ,Shinyanga,Mwanza, Shimiu,Geita n.k mtu kumiliki ng'ombe 50 kwa kiwango cha chini kabisa ni jambo la kawaida. Lakini cha ajabu viongozi wetu wanashindwa kuwapa elimu namna ya kujitambua kuwa wao sio maskini MTU anakuja na kuwaaminisha kuwa wao ni maskini wanahitaji elimu bure na misaada kibao toka kwa wanasiasa.Wanawageuza kuwa ombaomba na kuamini kuwa wao ni maskini kwa sababu hawajaajiriwa na mtu mwingine kuajiriwa.

Kundi lingine ni la wakulima wanaotokea mikoa yenye ardhi kubwa yenye Rutuba kama Mtwara,Ruvuma,Iringa ,Morogoro, Rukwa, Katavi, Mbeya ,Tanga hasa maeneo ya Lushoto ambao Masaa 24 FUSO zinasomba vyakula kupeleka DSM . Hao nao wanaitwa maskini wasio na uwezo wa kula Milo miwili.

Mikoa kama ya Kilimanjaro , Kagera na Tabora wao wanategemea mazao ya wakoloni kama Tumbaku na Kahawa. Lakini hata hivyo wale waliotumia mazao hayo vizuri wakati wa bei nzuri walisomesha watoto wao na wakabadili mifumo yao ya maisha kuwa ya kigeni.

Mwaka Juzi na mwaka Jana Kule Mtwara na Lindi walipata sana Korosho na bei ilikua nzuri lakini chaajabu watu wengine walijenga mpaka nyumba za bati la msauzi . Yani hao tatizo pia ni matumizi ya maarifa kukabiliana na ugumu wa maisha lakini mali wanazo.
Kuna Vijana wengi Kule Moshi na Mirerani wanapata pesa kwa kazi za madini na Kubeba mizigo ya watalii lakini wakishapata fedha wanakimbilia kwenye Pombe mpaka wanaoga na kufua nguo zao kwa Bia. Hawa nao wanaisubiri serikali iwawezeshe ili wapate Milo miwili kwa siku.
Nilikwenda kijijini Mwaka 2014 karibu kila nyumba ina mtu moja au wawili wanaomiliki gari na nyumba nzuri huko mijini. Unapotathimini utajiri unaomilikiwa na watanzania wenyewe kuanzia nyumba,magari , mifugo,mashamba na vitalu vya madini na mitumbwi ya kuvulia samaki huko ziwani na baharini utagundua kuwa ni utajiri mkubwa sana ukilinganisha na idadi ya watu . China watu wengi wanakaa nyumba za umma na kwenye vimitumbwi na vijumba vya mbao.

Hata nchi za magharibi wengi wanaishi nyumba za umma. Ni aina ya mfumo waliouona unawafaa. Mifumo yetu ya asili ya kumiliki Mali wao wanaona ni umaskini.
Mkuu inawezekana kuwa kweli hao ukitaja kuwa wana mifugo na bado wanawekwa kwenye kundi la jamii ya watu maskini ni kwa sababu zifuatazo:
1.Una ngombe hamsini na bado unanala kwenye nyumba ambao ndio ngombe wanakofugiwa.
2.Mlo wa mfugaji unaweza kuwa ni duni kwani hauko balanced.
3.Mkulima anaweza kuwa na mufugo mingi tu lakini bado vitu vya msingi kabisa hana mfano ,choo cha shimo,hajui kusoma wala kuandika .
4.Mkulima ana mifugo mingi tu na bado anapata mlo mmoja kwa siku ili apunguze matumizi kwa familia.
Kwa ufupi mkuu umaskini una vigezo vingi sana .
 
Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,399
2,000
Kama nimekupa hadi sheria, umeshindwa kuona kifungu, kwa vile mimi nimehudhuria kongamano, elimu hiyo ya PPP kwenye oil and gas, nimeipata ya kunitosha, hivyo kwa hiyo elimu yako ya PPP, ifungulie thread utupige darasa, tuongezee kwenye kile kidogo tulichopata.
P
Nashukuru mnoo kwa kunielewa Bosi ,niko tayari kutoa elimu ya PPP pindi nitakapoona maada inayozungumzia swala husika mkuu.Kwa kifupi tu PPP kwa kuanzia ni concept iliyobuniwa na nchi za Magharibi kwa ajili ya ushirikiano wa sekta binafsi na setikali kwa ajili ya kuendeleza miundo mbinu haswa ya barabara ,umeme na hata maji .Kuna necessary conditions ambazo zinafanya mradi uwe na sifa ya kuitwa PPP ambazo kwa sasa sitaziweka wazi hadi pale nitakapoona uchambuzi wa hiyo miradi ya PPP kwenye utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta .
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,383
2,000
Nashukuru mnoo Bosi ,niko tayari kutoa elimu ya PPP pindi nitakapoona maada inayozungumzia swala husika mkuu.Kwa kifupi tu kuna necessary conditions ambazo zinafanya mradi uwe na sifa ya kuitwa PPP ambazo kwa sasa sitaziweka wazi hadi pale nitakapoona uchambuzi wa hiyo miradi ya PPP kwenye utafutaji na uchimbaji wa gesi na mafuta .
Mkuu Makupa asante, japo naona na wewe unaendeleza yale yale madhaifu yanatufanya Watanzania tunashindwa kuendelea, kwa kusubiri wengine wafanye!. Wewe una uelewa wa PPP lakini hiyo elimu hutaitoa hadi utakapoona mada inayozungumzia suala husika ipandishwe na mwingine!. Halafu umezungumzia some necessary conditions ambazo hutaziweka wazi hadi pale utakapoona uchambuzi wa miradi hiyo ya PPP kwenye gesi na mafuta!, then utasubiri sana na hiyo elimu kaa nayo mwenyewe ikufaidie mwenyewe!. Unategemea utaona uchambuzi wa PPP za oil and gas humu jf!, wewe kama unayo hiyo elimu ya PPP, anzisha thread elimisha, usisubiri wengine!.

P.
 
1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
5,170
2,000
Mkuu inawezekana kuwa kweli hao ukitaja kuwa wana mifugo na bado wanawekwa kwenye kundi la jamii ya watu maskini ni kwa sababu zifuatazo:
1.Una ngombe hamsini na bado unanala kwenye nyumba ambao ndio ngombe wanakofugiwa.
2.Mlo wa mfugaji unaweza kuwa ni duni kwani hauko balanced.
3.Mkulima anaweza kuwa na mufugo mingi tu lakini bado vitu vya msingi kabisa hana mfano ,choo cha shimo,hajui kusoma wala kuandika .
4.Mkulima ana mifugo mingi tu na bado anapata mlo mmoja kwa siku ili apunguze matumizi kwa familia.
Kwa ufupi mkuu umaskini una vigezo vingi sana .
Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa wazungu na waarabu ndio waliotuletea maisha ya furaha ,amani ,upendo ,raha, haki,utu, umoja ,chakula bora , na maendeleo?
Maana hayo ndiyo mambo ya mdingi kabisa kwa binadam.

Niliwahi kutembelea Boma la Mzee mmoja mfugaji wa Kabila fulani. Ana wanawake watatu na watoto wengi tu. Wanaishi maisha ya raha sana ,kuheshimiana sana, Upendo na wanafanya kazi ,wanakula chakula bora sana cha asili. Wanaishi kwenye nyumba zao za asili. Watoto wa umri tofauti wanacheza michezo ya asili na ngoma za asili kwa raha ajabu, wazee wanakutana na kujadili mambo ya jamii yao kwa amani kabisa.

Sijawahi kusikia maeneo yao yakiwa na ugonjwa wa Kipindupindu kutokana eti na ukosefu wa vyoo vya kizungu. Magonjwa kama Presha,Kisukari,kansa, Ukimwi ,pumu,TB n.k ni nadrasana kuyasikia.

Tatuzo Waafrika tumeamua kucheza Ngoma za Wageni na kudharau ngoma zetu. Tumeamua Kuishi kama wageni kwa tabu na kwa dhiki kubwa .
Tumeamua kuita maisha yetu ya asili kuwa ni ujinga na kukosa elimu. Elimu zetu za asili zilizotufundisha namna ya kutibu maradhi mbalimbali tumezidharau na kuona kuwa ni umaskini. Dini zetu za asili tumeziita ni za kishenzi na upagani kwa sababu ya kuenzi dini za wageni. Leo hii kuna watu wanaongea Kiswahili kwa lafudhi ya kizungu kwa sababu mpaka lugha zetu tunaona sio za kimataifa na hazina heshima na ukiongea lugha za asili unaonekana kama mtu mshamba na mjinga asiye na maendeleo.

Hata hivyo mtu mwenye ngombe 10000 ukitaka abadilike na kuishi maisha ya kimagharibi au mashariki ni suala la wakati lakini sio kuwa ni umaskini.

Wananchi Wengi kwa sasa waliopo vijijini walinunua Solar Power zao wenyewe kabla ya umeme wa REA bila kutegemea misaada ya wanasiasa wanaojifanya wanahuruma kumbe ni uroho wao wa kujipenda na kupenda kuishi maisha ya kifahari na kimagharibi kupitia madara wanayolipwa mamilioni kupitia kodi na migongo ya wananchi.

Enzi za ukoloni machifu waliuza nchi zetu ili tu waishi maisha yanayofanana na ya wakoloni. Wengine waliwakaribisha wakoloni kwa sababu ya kupewa nguo,wengine bunduki,wengine shanga na wengine watoto wao kuahidiwa kuwa watasomeshwa ili waje kuwa wakoloni weusi na watawala kwa lugha itakayotambulika n.k.
 
Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,399
2,000
Mkuu Makupa asante, japo naona na wewe unaendeleza yale yale madhaifu yanatufanya Watanzania tunashindwa kuendelea, kwa kusubiri wengine wafanye!. Wewe una uelewa wa PPP lakini hiyo elimu hutaitoa hadi utakapoona mada inayozungumzia suala husika ipandishwe na mwingine!. Halafu umezungumzia some necessary conditions ambazo hutaziweka wazi hadi pale utakapoona uchambuzi wa miradi hiyo ya PPP kwenye gesi na mafuta!, then utasubiri sana na hiyo elimu kaa nayo mwenyewe ikufaidie mwenyewe!. Unategemea utaona uchambuzi wa PPP za oil and gas humu jf!, wewe kama unayo hiyo elimu ya PPP, anzisha thread elimisha, usisubiri wengine!.

P.
Mkuu P,kimsingi sijakataa kutoa elimu ya PPP bali nilishangazwa na hiyo miradi ya oil na gesi ya aina ya PPP ambayo ndio niltaka kuona ikoje ndio nami niweze kutoa elimu ya PPP kwa ujumla wake mkuu
 
Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,399
2,000
Kwa hiyo unataka kuniambia kuwa wazungu na waarabu ndio waliotuletea maisha ya furaha ,amani ,upendo ,raha, haki,utu, umoja ,chakula bora , na maendeleo?
Maana hayo ndiyo mambo ya mdingi kabisa kwa binadam.

Niliwahi kutembelea Boma la Mzee mmoja mfugaji wa Kabila fulani. Ana wanawake watatu na watoto wengi tu. Wanaishi maisha ya raha sana ,kuheshimiana sana, Upendo na wanafanya kazi ,wanakula chakula bora sana cha asili. Wanaishi kwenye nyumba zao za asili. Watoto wa umri tofauti wanacheza michezo ya asili na ngoma za asili kwa raha ajabu, wazee wanakutana na kujadili mambo ya jamii yao kwa amani kabisa.

Sijawahi kusikia maeneo yao yakiwa na ugonjwa wa Kipindupindu kutokana eti na ukosefu wa vyoo vya kizungu. Magonjwa kama Presha,Kisukari,kansa, Ukimwi ,pumu,TB n.k ni nadrasana kuyasikia.

Tatuzo Waafrika tumeamua kucheza Ngoma za Wageni na kudharau ngoma zetu. Tumeamua Kuishi kama wageni kwa tabu na kwa dhiki kubwa .
Tumeamua kuita maisha yetu ya asili kuwa ni ujinga na kukosa elimu. Elimu zetu za asili zilizotufundisha namna ya kutibu maradhi mbalimbali tumezidharau na kuona kuwa ni umaskini. Dini zetu za asili tumeziita ni za kishenzi na upagani kwa sababu ya kuenzi dini za wageni. Leo hii kuna watu wanaongea Kiswahili kwa lafudhi ya kizungu kwa sababu mpaka lugha zetu tunaona sio za kimataifa na hazina heshima na ukiongea lugha za asili unaonekana kama mtu mshamba na mjinga asiye na maendeleo.

Hata hivyo mtu mwenye ngombe 10000 ukitaka abadilike na kuishi maisha ya kimagharibi au mashariki ni suala la wakati lakini sio kuwa ni umaskini.

Wananchi Wengi kwa sasa waliopo vijijini walinunua Solar Power zao wenyewe kabla ya umeme wa REA bila kutegemea misaada ya wanasiasa wanaojifanya wanahuruma kumbe ni uroho wao wa kujipenda na kupenda kuishi maisha ya kifahari na kimagharibi kupitia madara wanayolipwa mamilioni kupitia kodi na migongo ya wananchi.

Enzi za ukoloni machifu waliuza nchi zetu ili tu waishi maisha yanayofanana na ya wakoloni. Wengine waliwakaribisha wakoloni kwa sababu ya kupewa nguo,wengine bunduki,wengine shanga na wengine watoto wao kuahidiwa kuwa watasomeshwa ili waje kuwa wakoloni weusi na watawala kwa lugha itakayotambulika n.k.
Aisee ,kwa hali ilivyo mkuu naona unaami zaidi katika fikra za kijima kuliko wa hali halisi ya mambo yalivyo hapa duniani
 
monaco

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,187
2,000
Mkuu Kalam ,Pasco ana kahesima kake ila wakati mwingine anapotosha wasiojua na bahati mbaya hawajajua kuwa wanapotoshwa na Pasco
Wewe sijui nikuweke kundi gani....
Kila siku kujifanya Mjuaji,unajua sanaaa,mkosoaji kwa Pasco.
Bahati mbaya Huweki/Husemi kile kilicho Sahihi kwako,Zaidi nimeona Sijui unaandaa Soft copy,sijui hata wazungu wamekuomba,Sijui ulikuwa nyuma ya Benzi Nyeusi!Allah acha hizo wewe, be Critical, logical,analytical,Coherent and Provide Soln and Probken!
Cc:mad:Pascal Mayalla
 
monaco

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,187
2,000
Kama nimekupa hadi sheria, umeshindwa kuona kifungu, kwa vile mimi nimehudhuria kongamano, elimu hiyo ya PPP kwenye oil and gas, nimeipata ya kunitosha, hivyo kwa hiyo elimu yako ya PPP, ifungulie thread utupige darasa, tuongezee kwenye kile kidogo tulichopata.
P
Wewe jamaa Una Akili Sana sana Aisee
You are so Objective and Positive!
Ila Huyu sijui Makupaa,Kazi yake ni Kupinga tuuu,He needs to be logical,Analytical, critical coherent ,Msomi sio kubisha tuu Toa Way forward,toa unachofikiri...
Ahsante Pascal Mayalla
 
monaco

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,187
2,000
Wewe jamaa Una Akili Sana sana Aisee
You are so Objective and Positive!
Ila Huyu sijui Makupaa,Kazi yake ni Kupinga tuuu,He needs to be logical,Analytical, critical coherent ,Msomi sio kubisha tuu Toa Way forward,toa unachofikiri...
Ahsante Pascal Mayalla
Kwanini una Akili....answer is....kwasababu nimekuona kitambo unapenda sana kujifunza/Kusikiliza!
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,383
2,000
Mkuu P,kimsingi sijakataa kutoa elimu ya PPP bali nilishangazwa na hiyo miradi ya oil na gesi ya aina ya PPP ambayo ndio niltaka kuona ikoje ndio nami niweze kutoa elimu ya PPP kwa ujumla wake mkuu
Kwa kadri unavyozidi kuchangia ndivyo ninavyokuona ulivyo kichwa panzi!. Tangu tumeanza kugawa vitalu vya gesi, Mtwara, tumesaini PSA 23, mpaka sasa ni PSA 11 ndizo zinafanya kazi na hakuna hata moja ina hata pua ya mzawa kutokana na hatuna uwezo hata punje ya hata ku bid tuu ni US $ 1,000,000. Mpaka sasa, miradi mikubwa ya gesi ya Mtwara, bado iko kwenye stage ya upstream, downstream bado. Hivyo kwenye upstream hakuna hata kampuni moja ya wazawa. Sheria mpya inataka wazawa tushirikishwe kwa kuuziwa hadi 25% lakini kampuni gani ya ndani ina jeuri hiyo?. Hivyo concentration yetu sasa iwe ni kwenye downstream. Hivyo kama unasubiri kuona hiyo miradi ya upstream, utangoja milele!.

Kama una elimu kuhusu PPP toa, kama unaiona hiyo elimu iliyonayo ni mali sana, hivyo una set conditions ndipo utoe, then kaa nayo hiyo elimu yako labda itakufaidia sana.

JF ni users generated forum, mtu kuna kitu unajua, unamwaga na kushare na wengine, hujui unakaa kimya na kuwaacha wenye elimu zao wasio na uchoyo, wajimwage.
P
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,383
2,000
Wewe jamaa Una Akili Sana sana Aisee
You are so Objective and Positive!
Ila Huyu sijui Makupaa,Kazi yake ni Kupinga tuuu,He needs to be logical,Analytical, critical coherent ,Msomi sio kubisha tuu Toa Way forward,toa unachofikiri...
Ahsante Pascal Mayalla
Du kumbe huyu ndiye yule jamaa wa benzi jeusi!, amini usiamini, mimi niliisha sahau sikumkumbuka tena!. Maana sisi watu wa boda boda na bajaj kuitwa kwenye benzi nyeusi, lazima uogope!, unaweza kutoka mbio, kukimbilia mwito wa benz nyeusi, ukifikiri ni zile benz nyeusi za ikulu, kufika, ukakutana na Nissan nyeupe!.
P
 
Tumbo

JF-Expert Member
Oct 21, 2013
282
500
Haya mambo sio asili yetu, sisi kazi yetu kupinga tu na kulalamika tunaibiwa. Saivi hatuongei, wakishanunua hawa jamaa ndio mtatuona tulipo watanzania ktk ubora wetu wa kulalamika.

Nchi haijengwi kwa maneno
Siyo asili yenu na nani? Sasa hivi unataka tuongee nini wakati wakubwa walishagawana gesi kwa kupitisha hiyo mikataba ya mafuta na gesi kwa hati za dharura kule bungeni?

Tulipo zungumza huko bungeni kupinga hiyo mikataba ya kinyonyaji, nyie miccm mlitukebehi, mlitupuuza na kutuona kama si WAZALENDO, haijachukua mda mrefu jiwe aliyekuwa miongoni mwa wapiga kura za ndioooo kakiri wakubwa washagawana rasilimali zetu...! what do you people n' children of darkness want us to discuss...!!!!
 
Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,399
2,000
Mk
Kwa kadri unavyozidi kuchangia ndivyo ninavyokuona ulivyo kichwa panzi!. Tangu tumeanza kugawa vitalu vya gesi, Mtwara, tumesaini PSA 23, mpaka sasa ni PSA 11 ndizo zinafanya kazi na hakuna hata moja ina hata pua ya mzawa kutokana na hatuna uwezo hata punje ya hata ku bid tuu ni US $ 1,000,000. Mpaka sasa, miradi mikubwa ya gesi ya Mtwara, bado iko kwenye stage ya upstream, downstream bado. Hivyo kwenye upstream hakuna hata kampuni moja ya wazawa. Sheria mpya inataka wazawa tushirikishwe kwa kuuziwa hadi 25% lakini kampuni gani ya ndani ina jeuri hiyo?. Hivyo concentration yetu sasa iwe ni kwenye downstream. Hivyo kama unasubiri kuona hiyo miradi ya upstream, utangoja milele!.

Kama una elimu kuhusu PPP toa, kama unaiona hiyo elimu iliyonayo ni mali sana, hivyo una set conditions ndipo utoe, then kaa nayo hiyo elimu yako labda itakufaidia sana.

JF ni users generated forum, mtu kuna kitu unajua, unamwaga na kushare na wengine, hujui unakaa kimya na kuwaacha wenye elimu zao wasio na uchoyo, wajimwage.
P
Mkuu naweza kuwa kichwa panzi kwa kadri unavyoona ila ninachosisitiza ni kwamba acha kupotosha umma kupitia humu jamvini .Nilipokuuliza nionyeshe kipengele cha sheria kinachoongelea PPP kwenye utafutaji wa gesi na mafuta ulinitajia section 218 ambayo sikuona mahali popote kuhusu PPP.Ningekuomba sana mkuu fanya utafiti kidogo tu ili uweze pata taarifa kuwa kila PSA signed serikali ina participarting interest ambayo si chini ya asilimia 20%.Unapongolea dowstream operations uwe muwazi basi ni eneo lipi hao watanzania watashiriki kwa mfumo wa PPP ?na sio kusema tu oh watanzania wazawa washiriki bila kuonyesha ushiriki wao utakuwa kwa mfumo wa aina gani?
 
Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,399
2,000
Wewe jamaa Una Akili Sana sana Aisee
You are so Objective and Positive!
Ila Huyu sijui Makupaa,Kazi yake ni Kupinga tuuu,He needs to be logical,Analytical, critical coherent ,Msomi sio kubisha tuu Toa Way forward,toa unachofikiri...
Ahsante Pascal Mayalla
Acha papara mkuu,issue hapa ni Pascali kupotosha na kutoa kifungu cha sheria ambacho hakina anachokiongelea humu.Unawezaji kuwa logical kwa kulishwa matango pori na waongo wa humu JF?
 
Capital G

JF-Expert Member
Jul 2, 2017
1,540
2,000
Kitu kikubwa sana hiki ulishauri mkuu
Mkutano umeanza kwa kuhutubiwa na waziri wa Nishati wa Zanzibar, Waziri wa Nishati wa Uganda na sasa anazungumza Naibu waziri wetu wa Nishati.

Kusema ukweli, kuwe kunafanyika assessment ya uwezo wa mawaziri wetu na manaibu waziri kuhutubia mikutano na makongamano ya kimataifa kwa lugha ya Kiingereza!, maana haya mambo ya kuhutumbia kwa lugha za watu, wakati lugha zenyewe hazipandi kivile kwenye mikutano ya kimataifa sio mazuri!

Maadam tumekubaliana kuwa lugha yetu ya taifa ni Kiswahili, then utolewe muongozo kwa viongozi wote ambao sio fluent in English, wawe wanahutubia kwa Kiswahili, halafu hao wazungu watapewa traslated version, kuliko kutuletea mawaziri wetu wanaojiuma uma kwa lugha za wenzetu!.

Tumehudhuria mikutano kibao China, wanazungumza Kichina!. Mikutano ya Korea, kinazungumzwa Kikorea, hivyo Mikutano yote ya kimataifa Tanzania, tuzungumze Kiswahili na hii pia ndio namna bora ya kukikuza Kiswahili.

P.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Capital G

JF-Expert Member
Jul 2, 2017
1,540
2,000
Dah, inasikitisha sana mkuu
@

Pascal Mayalla investment katika mambo ya gesi inahitaji very huge funds injection . Hakuna mwenye uwezo wa hizo hela Tanzania, hata bank hawawezi ku risk kukupa hela hizo. Muhongo alipishana na Mengi akasema size yenu ni viwanda vya soda wakamshambulia mpaka kiama! Sasa ukweli umeouna mwenyewe Pascal! Ukiangalia hiyo mitambo inayoelea baharini huko kilwa unakata tamaa! Pascal, hata expertise hatuna. That means hata wataalamu uwaazime kutoka nje kuja kuchimba!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Capital G

JF-Expert Member
Jul 2, 2017
1,540
2,000
Huyu professor dah, basi bhana ndio Tanzania
Pia CAG amezungumzia mradi dola bilioni 20 wa mtambo wa kuchakata gesi ambao kwa sasa mazungumzo yamekwama.
Amesema huu ni mradi muhimu sana, na akatoa maoni yake kama Prof. Mussa Assad na sio kama CAG wa Tanzania.

Ameshauri kitu muhimu cha kwanza kwa pande zote zinazohusika ni kuaminiana, trust, kitu cha pili na kwa pande zote kuwa wakeli kabisa, truthfulness, na kitu cha mwisho ni kuwa transparent, wawazi, mradi huu ufanikiwe.

Tumeingia Lunch Break.

P.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
39,383
2,000
Unapongolea dowstream operations uwe muwazi basi ni eneo lipi hao watanzania watashiriki kwa mfumo wa PPP ?na sio kusema tu oh watanzania wazawa washiriki bila kuonyesha ushiriki wao utakuwa kwa mfumo wa aina gani?
Mkuu Makupa, kwa heshima na taadhima, nakuelimisha tena, jf ni user generated forum, unaongolea kile unachokijua, unachangia kwa kadri ya uwezo wako, unakosoa kwa kupangua hoja kwa hoja. Usipangie watu humu cha kuchangia, wewe changia ulichonacho.

Nimesema humu kwenye upstream Watanzania hatujashiriki kwasababu hatuna uwezo, hivyo ushiriki wetu wa local content ni kwenye downstream only, sasa ni eneo lipi na kwa mfumo gani, atasema anayejua.

If you know something, please share, if you don't then keep your knowledge and what you know to yourself ikufaidie wewe na familia yako.

Be free hata kuanzisha thread kumwaga data of what you you na sio kuwapangia watu kitu cha kuchangia, tena wengi humu kwenye kinachoendelea kwenye mambo ya gesi asili ndio wameanza sasa, Chuo chetu kikuu cha UDSM ndicho pekee kwa Tanzania kinatoa elimu ya Oil & Gas na wahitimu wa kwanza wata graduate October 2020, sasa angalia mimi elimu hii ya Gesi asili nimeanza kuitoa lini humu

P
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom