From Hyatt Regency, The Kilimanjaro: the 2nd Tanzania Oil & Gas Congress. Wazungu Wengi Kuliko Wenyeji!

3. Lazima kuishirikisha private sector kwa kuongeza PPP kwenye kila mradi
4. Dialogue inahitajika sana.
5. Tunatakiwa kuongeza trust na transparency
 
Mwisho amemalizia kwa kusisitiza kuwa Serikali ya Tanzania iko tayari kupokea mapendekezo yote toka Private Sector jinsi ya kutumia resources zetu zitufaidie sote.
P.
 
Vote of thanks toka kwa Abdulsamad Abdulrahim, mkurugenzi wa Pietro Fiorantini Tanzania ambao ndio waandalizi wa kongamano hili
P
 
Hakuna mtanzania mwenye uwezo wa kuinvest kwenye oil and gas industry. Hiyo ni level nyingine ndugu yangu. Kwanza inataka hela nyingi sana na utaalamu wa hali ya juu. Sie tuendelee na biashara yetu ya juice na biscuti tu. Kama serikali inataka watanzania tunufaike na hiyo gas basi ipeleke vijana wetu nchi zenye huu utaalamu wakapate elimu. Na pia izingatie swala la kuhakikisha haya mashirika yana ajiri watanzania. Nakumbuka mawaziri wetu waliwahi kwenda Oman kuona jinsi serikali ilivyo weza kuhakikisha raia wananufaika na ajira za oil and gas.
 
Wanabodi,

Leo nimepata fursa ya kuhudhuria kongamano la pili la Oil and Gas linalofanyika hapa Hoteli ya Hyatt, Kilimanjaro, ambapo mgeni rasmi ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kasim Majaliwa, anayewakilishwa na Waziri January Makamba, (kufuatia ajali ya MV Nyerere, kumeitishwa kikao cha dharura cha Cabinet).

Kitu cha kwanza ku note, wajumbe wazungu ni wengi zaidi kuliko wenyeji, kitu kinachoashiria sisi Watanzania, ama bado tuko nyuma katika kuchangamkia fursa za uchumi wa gesi, na bomba la mafuta, ama mambo ya uchumi wa Gesi ni mambo la level ya juu sana, not reachable kwa Watanzania walio wengi, ndio maana hata kwenye vitalu vyote vya gesi, hakuna hata kitalu kimoja kinachomilikiwa na kampuni ya Kitanzania!.

Mkutano umeanza kwa one minute silence kuwakumbuka wahanga wa ajali ya MV Nyerere.
Ratiba ni hii

08:20 Welcome Address
08:30 Ministry of Energy Address: Outlining the Vision for Tanzania's Industrialisation Powered by Oil & Gas
08:45 Official Presidential Address
09:00 Sponsors Welcome Addresses
09:20 Session 1: Ministerial Session Opening Remarks
11:30 Session 2: Oil & Gas Latest Developments in Tanzania: Government & Industry Collaboration to Move the Projects Forward
14:15 Session 3: Project Spotlight: East Africa Crude Oil Pipeline (EACOP) - The Pipeline's Strategic Importance to Tanzania & the Region
16:00 Session 4: PANEL DISCUSSION: Creating a Robust & Investor Friendly Business Environment in Tanzania's Oil & Gas Projects
17:30 End of Congress Day One
Congress Day Two - Tuesday 25 September (Location: Mezzanine Floor)

09:00 Session 5: PANEL DISCUSSION: Attracting Investment to Upstream E&P Projects in Tanzania & Around the Globe
11:00 Session 6: Gas Monetisation as a Force to Power Industrialization & Economic Development
14:00 Session 7: PANEL DISCUSSION: Local Content & Job Creation Ensuring a Sustainable Development in Tanzania's Oil & Gas Projects
15:30 Session 8: Downstream Projects & Infrastructure Development in Tanzania
17:00 Session 9: Tanzania Oil & Gas Congress Closing Remarks & Official Conclusions
18:00 End of Tanzania Oil & Gas Congress 2018

Nimeperusi kwa haraka haraka sura za wale top ten wafanyabiashara mabilionea wa Tanzania, sikufanikiwa kuziona, ila kwa vile nimetokea airport kuja hapa ukumbini, pale Airport nimeshuhudia ndege za private Jet, zaidi ya 5, zimewaleta mabilionea kutoka sehemu mbalimbali duniani akiwemo bilionea mmoja mkubwa sana kutoka Arabuni.

Kitendo cha ushiriki mdogo wa wazawa katika makongamano kama haya, ni uthibitisho wa kuhitajika elimu ya uhamasishaji zaidi kwa Watanzania wazawa, tuchangamkie fursa za uchumi wa gesi na bomba la mafuta la Uganda.

Karibuni sana.

Paskali
Poti tunashukuru umetuwakilisha sisi....
 
Kweli kabisa mkuu bila elimu tutaendelea kulaumiana tu. Tunahitaji kuwekeza katika elimu na teknolojia kwa kiwango kikubwa kwa sababu dunia inakimbia kwa kasi sana

Hilo ni kweli na halina ubishi hata kidogo kwani msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Lakini wakati wengine wanakimbia sisi tunajikongoja. Tunasema eti tunataka kubadilisha lugha ya kufundishia kuwa kiswahili katika madaraja yote ya elimu. Tutaanza na kutafsiri vitabu vyote vilivyoko kwa lugha nyingine yoyote kwenda kwenye kiswahili. Tukifanya maamuzi haya basi tutakutana na wenzetu tulioko kwenye safari moja ya kusaka maendeleo wanarudi kutoka kwenye safari hiyo huku sisi tukianza na nini vile... (JKT "ya zamani" tulikuwa tunauita mwendo wa mbwa siyo?). Sasa hivi watu wanazungumzia IoT (kwa kirefu ni "Internet Of Things" - TUKI watatusaidia kuiweka kwenye kiswahili fasaha) sisi tunazungumza nini sijui... tutapata tabu sana siyo?. Kwa uongozi wowote ule ni lazima tuwe na matumaini ndiyo jambo la msingi.
 
Sasa hivi watu wanazungumzia IoT (kwa kirefu ni "Internet Of Things" - TUKI watatusaidia kuiweka kwenye kiswahili fasaha) sisi tunazungumza nini sijui... tutapata tabu sana siyo?. Kwa uongozi wowote ule ni lazima tuwe na matumaini ndiyo jambo la msingi.
Yote haya yanazidi ku'expose' hali halisi ya uwezo uliopo..
 
Abdulsamad Abdulrahim, mkurugenzi wa Pietro Fionantini Tanzania ambao ndio waandalizi wa huu mkutano
Naelewa huyo bwana Abdul na juhudi zake na bomba la Uganda. Najua pia ni kiongozi, nadhani ni Vice Chairman of the Association of Tanzania Oil and Gas Service Providers.
Ni jambo jema ametuwakilisha katika kuuandaa Mkutano huo Lakini kama ameshindwa kuwashirikisha na kuwasaidia wenzake ndani ya chama chao nao wanufaike na yaliyojadiliwa, atakuwa hajafanya kazi yake vyema.

Hao akina Fiorentini ni waandalizi tu, kazi ambayo hata akina Paskal wetu wangeweza kuifanya kwa ufanisi mkubwa kama wangejiamini na kujipa uwezo zaidi.
 
Back
Top Bottom