From Hyatt Regency, The Kilimanjaro: the 2nd Tanzania Oil & Gas Congress. Wazungu Wengi Kuliko Wenyeji!

Hivi wewe unajua kuwa kwa kutoa huduma almost zote bure anaharibu ubunifu wa watu wengi? Hili si lilitokea wakati wa ujamaa au? Maduka ya kaya, maduka ya ugawaji, maduka ya RTC, huku ukizuia biashara binafsi??!! Kwani manuafaa yanayozungumzwa kwamba yanaletwa na SMEs yamezuka tu hayakuwepo toka wakati wa utawala ule? Ukisema ili upate leseni ya biashara yoyote lazima uwe na kadi ya TANU/CCM unakuwa unalenga kitu gani?
Wewe muulize tu kuwa hivi China wananchi ni matajiri au serikali yenye pato kubwa kutokana na ukusanyaji wa kodi unaotokana na wingi wa watu bil. 1.6.
China ina watu wengi sana masikini wa kutupwa.

Hata hivyo China imeanza kukua kwa kasi baada ya kubadili mfumo wake wa uchumi wa kijamaa. Ujamaa ni unyonyaji mana wenye juhudi wananyonywa na wasio na juhudi.
 
Sehemu ambayo Kiingereza kinatumika sana ' Kimawasiliano ' Watanzania wengi huwa tunakuwa na ' allergy ' nako!
Inferiority complex unayo wewe, kwani ulisikia WAARABU wanazungumza kiingereza. Na unafikiri wote hao wazungu waliokuja wanatoka uingereza, au wote wanajua kiingereza.

Sababu kubwa ya watanzania kutoshiriki katika uwekezaji ni hii: Matajiri wishio Tanzania/watanzania wamejikuta kama wahanga wakuu katika awamu ya 5. Kwa matajiri kipindi hiki hakitofautiani sana na kile kipindi cha SOKOINE. Hata huko mahakamani kwa matajiri kupata haki ni taabu kweli kweli, na hasa ukituhumiwa kama muhujumu uchumi ndio umesahaulika.

Mambo ya uchumi yanapelekwa kisiasa zaidi. Tajiri Mtanzania anajiuliza kama, Dangote analalamika katika uwekezaji wake bila kupata jibu ni vipi mtanzania anaweza kuwekeza katika miradi mikubwa huku akiwa na uhakika na mali zake? Kwa muwekezaji yeyote yule kitu cha kwanza ni security ya pesa zake. Matajiri wa kitanzania wanafahamu upepo wa hali ya hewa katika awamu hii ndio maana hawakutokea hapo.

Kazi kubwa kwa matajiri wa Tanzania leo hii ni kutorosha mali zao nje kwa kile kinachoitwa usiweke mayai yote katika kikapu kimoja. Halafu mnatataka waende katika kongamano hilo wakajianike. Watawala Tanzania ni lazima wajirekebishe kama tuna nia ya dhati ya kuingia katika uchumi wa kati.

Hawa ni wachache waliofuata katika mali zao kwa sababu za kisiasa:

  • Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye
  • Mchungaji Kakobe
  • Tajiri Manji
 
Pascal,

Kwa taarifa yako ninamjua mtu niliyemsaidia katika kutengeneza Business Plan na Prospectus ili kuipeleka kampuni yao (start-up) kwenye DSE kupitia unaloliita dirisha dogo. Kiingereza chake kizuri ni Enterprise Growth Market (EGM) segment. Mimi nilikuwa consultant lakini nikitoa ushauri wangu bure kabisa, yaani bila malipo. Nilifanya kazi kubwa sana ya kufanya Feasibilty Study na kutengeneza report, kutengeneza Business Plan (a master piece - according to me), kutengeneza draft Prospectus kwa kumsaidia "Nominated Advisor" (kwa sababu ni kazi yake). Nilichoambulia ni pathetic. Na hasa kutoka CMSA. Ni kejeli. Swali la kwanza waliloniuliza eti mimi nafaidikaje kwa kufanya consulting bila kulipwa, SERIOUSLY????!!!???? Hili lilikuwa ni swali la kitaalamu? Swali lingine au maoni yao walisema eti watu hawawezi kununua hisa za kampuni ile kwa sababu sisi hatujweka hela. Walitaka tuweke kuanzia 60% na kuendela. Mimi nikawaambia **** hiyo 60% ingelikwepo kusingekuwa na haja ya kwenda kwao for EGM. Mengine nimeshayasema kwenye posting yangu ya awali. Ninayo experience na watu hawa bwana. They have very un-supportive behaviour! Mwisho wake ile project ikakwama. Sema tena Pascal!
Tembelea mitaa hii




P
 
Ni kweli kabisa , jambo la muhimu sana kwa dunia ya leo ni Elimu bora kwa wananchi wetu. Sio suala la kujua kusoma na kuandika tu kama tunavyoona sasa bali Suala la Elimu ya kumpa mtu ujuzi na utaalam.
Mfano tulitegemea mipesa mingi ingewekezwa vijana wetu kwenda kusoma nje kwa ajili ya kuiba teknolojia na ujuzi mbalimbali ili miaka 10 ijayo tuweze kujitaegemea kiteknolojia kwanza na kiutaalam wa masuala ya uchumi na biashara kabla ya mambo mengine.

Nilitegemea tujivunie kuwasomesha angalau kila mwaka vijana zaidi ya 40 kwenye nchi za Ulaya, Marekani,Canada,Brazil,India ,Indonesia,Afrika kusini,Japani,China,Urusi ,Israel,Iran, Pakistani,Misri,Algeria,Australia na kwingineko kwa gharama za serikali na hata kwa ufadhili wa mashirika makubwa na taasisi za umma.
Lakini badala yake ni kuwa awamu hii hata wale waliokua wanajisomesha wakiwa kazini kwa sasa inakua ni shughuli pevu.

Watawala ambao kwa kiwango kikubwa walijisomesha wakiwa kazini huku wakiwa wanalipwa na hata kufikia ngazi ya kupata digrii za uzamivu lakini hao hao Leo wanaweka mazingira magumu kwa wafanyakazi kuweza kujisomesha.

Wameng'ang'ana na kile wanachokiita Elimu bure kabisa ambayo kwa kiwango kikubwa imezidi kuipa serikali mzigo usio na manufaa kwa ukuaji wa uchumi wa nchi mana wanaosomeshwa bure ni kwa ngazi ya Elimu ya chini ambayo inachukua muda mrefu sana kuipata ,miaka 11 bila kumpa mwanafunzi ujuzi wowote zaidi ya kusoma na kuandiaka na kukariri vitabu tu.

Tulitakiwa tuwekeze zaidi Elimu ya juu na kati. Hawa wa elimu ya chini ni suala la kutumia sheria tu kuwabana wazazi wawasomeshe watoto wao ambao gharama ya Elimu ya Msingi ni ndogo kwa mzazi anayeambiwa hapa kazi tu.
Elimu ya Msingi Mzazi akiuza kuku wawili kwa mwaka anasomesha mtoto lakini chuo labda auze nyumba. Sasa serikali imewekeza bure kule kwenye unafuu na kukimbia kule kwenye umuhimu na kwenye gharama kubwa.

Hata hao wakubwa wanaamini katika kuwekeza kwenye Elimu bora kwa watoto wao lakini kwenye taifa wanawekeza kwenye Elimu ya kupata kura bure.
Kweli kabisa mkuu bila elimu tutaendelea kulaumiana tu. Tunahitaji kuwekeza katika elimu na teknolojia kwa kiwango kikubwa kwa sababu dunia inakimbia kwa kasi sana
 
Kwa taarifa yako makampuni makubwa sana ya Ulaya na Amerika ndiyo waliowekeza China kwa kiwango kikubwa mno. Ndiyo maana wafanyabiashara wanaona "tariffs" anazoweka Trump kwa bidhaa kutoka China zitayumbisha uchumi wa Marekani yenyewe. Sisi hao tunawaita Mabepari si kwa maana nzuri ila ni kwa maana ya "wezi"
"Kwa taarifa yangu"? Eeh, mbona uko chini kiasi hicho aise. Uchumi wa China umejengwa na makampuni ya nje? Usifikiri sielewi uwiano wa uwekezaji wa makampuni na kuendelea kwa uchumi wa nchi. Umekariri vibaya aisee.
 
Hivi wewe unajua kuwa kwa kutoa huduma almost zote bure anaharibu ubunifu wa watu wengi? Hili si lilitokea wakati wa ujamaa au? Maduka ya kaya, maduka ya ugawaji, maduka ya RTC, huku ukizuia biashara binafsi??!! Kwani manuafaa yanayozungumzwa kwamba yanaletwa na SMEs yamezuka tu hayakuwepo toka wakati wa utawala ule? Ukisema ili upate leseni ya biashara yoyote lazima uwe na kadi ya TANU/CCM unakuwa unalenga kitu gani?
Tunaweza kuyajadili yote haya vizuri tu ukitaka. Anzisha mjadala huo.
 
Wanabodi,

Leo nimepata fursa ya kuhudhuria kongamano la pili la Oil and Gas linalofanyika hapa Hoteli ya Hyatt, Kilimanjaro, ambapo mgeni rasmi ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kasim Majaliwa, anayewakilishwa na Waziri January Makamba, (kufuatia ajali ya MV Nyerere, kumeitishwa kikao cha dharura cha Cabinet).

Kitu cha kwanza ku note, wajumbe wazungu ni wengi zaidi kuliko wenyeji, kitu kinachoashiria sisi Watanzania, ama bado tuko nyuma katika kuchangamkia fursa za uchumi wa gesi, na bomba la mafuta, ama mambo ya uchumi wa Gesi ni mambo la level ya juu sana, not reachable kwa Watanzania walio wengi, ndio maana hata kwenye vitalu vyote vya gesi, hakuna hata kitalu kimoja kinachomilikiwa na kampuni ya Kitanzania!.

Mkutano umeanza kwa one minute silence kuwakumbuka wahanga wa ajali ya MV Nyerere.
Ratiba ni hii

08:20 Welcome Address
08:30 Ministry of Energy Address: Outlining the Vision for Tanzania's Industrialisation Powered by Oil & Gas
08:45 Official Presidential Address
09:00 Sponsors Welcome Addresses
09:20 Session 1: Ministerial Session Opening Remarks
11:30 Session 2: Oil & Gas Latest Developments in Tanzania: Government & Industry Collaboration to Move the Projects Forward
14:15 Session 3: Project Spotlight: East Africa Crude Oil Pipeline (EACOP) - The Pipeline's Strategic Importance to Tanzania & the Region
16:00 Session 4: PANEL DISCUSSION: Creating a Robust & Investor Friendly Business Environment in Tanzania's Oil & Gas Projects
17:30 End of Congress Day One
Congress Day Two - Tuesday 25 September (Location: Mezzanine Floor)

09:00 Session 5: PANEL DISCUSSION: Attracting Investment to Upstream E&P Projects in Tanzania & Around the Globe
11:00 Session 6: Gas Monetisation as a Force to Power Industrialization & Economic Development
14:00 Session 7: PANEL DISCUSSION: Local Content & Job Creation Ensuring a Sustainable Development in Tanzania's Oil & Gas Projects
15:30 Session 8: Downstream Projects & Infrastructure Development in Tanzania
17:00 Session 9: Tanzania Oil & Gas Congress Closing Remarks & Official Conclusions
18:00 End of Tanzania Oil & Gas Congress 2018

Nimeperusi kwa haraka haraka sura za wale top ten wafanyabiashara mabilionea wa Tanzania, sikufanikiwa kuziona, ila kwa vile nimetokea airport kuja hapa ukumbini, pale Airport nimeshuhudia ndege za private Jet, zaidi ya 5, zimewaleta mabilionea kutoka sehemu mbalimbali duniani akiwemo bilionea mmoja mkubwa sana kutoka Arabuni.

Kitendo cha ushiriki mdogo wa wazawa katika makongamano kama haya, ni uthibitisho wa kuhitajika elimu ya uhamasishaji zaidi kwa Watanzania wazawa, tuchangamkie fursa za uchumi wa gesi na bomba la mafuta la Uganda.

Karibuni sana.

Paskali
Muhongo was right. Hii biashara si tu inahitaji logistics na uelewa mkubwa wa biashara za kidunia, ina sayansi na sanaa yake. Hatuwezi mambo haya hata tusijindanganye na tukitaka kununa bhasi apewe Mbongo tena black skinned!!!,.

Ukitazama hata biashara za matajiri wetu japo wanapata hela ni biashara za viwanda vidogovidogo na uchuuzi ambazo wanatrade locally na nji jirani.
 
Prof

Muhongo aliposema ukweli kuwa hawa mabilionea wa Tanzania wanaweza kuwekeza kwenye soda mlimwona ni pimbi pamoja na ukweli ya kwamba Prof nae ni mmojawapo ya walioharibu sekta nzima ya utafutaji na uendelezaji mafuta hapa nchini.
Hakuharibu chochote. Mlimwonea wivu, eti ni arrogant!!
 
Hata hao wazungu hawana mitaji wanacheza na Mabank ka ma ambavyo hawa unaowaita wauza soda walicheza wakaazisha viwanda vya soda sasa walitaka kucheza na Mabank wawekeze pia ktk gas. Wewe baki na ujinga wenu wa asili mtaishia kulalia uji wa ndimu hadi kufa.
Hapo ishu si mtaji bali ni logistics za hii biashara.
 
Ni kweli kabisa hayo uliyoyaeleza. Huo ni mkutano wa wakubwa, lakini sisi kama wadogo, tena tuliowakaribisha waje hapa tunashindwa vipi kuitumia fursa hii kujifunza hata yale madogo yaliyomo ili tuweze kunufaika nayo?
Kuna vijana chungu nzima wamefuzu kwenye eneo hili, hatuwezi hata kuwapa nafasi ya kujifunza zaidi kwa kuhudhuria mkutano kama huu. Wizara mama ingeamua hata kuwalipia registration fee, hata wanafunzi kadhaa tu waliopo vyuo vikuu kwenye vitivo husika. Hata makampuni hayo yangeombwa kutoa 'sponsorship' kwa baadhi ya vijana hao isingekuwa taabu hata kidogo.
Tatizo letu ni lilelile. Hatuna uthubutu. Mioyo yetu imelala sana.
Mkuu utaifa wa kizalendo uliondoka na Mwl.Nyerere,Nyerere alikuwa na uwezo wa kufanya matayarisho ya vijana kujifunza nje namna ya kuendesha miradi hiyo kabla ya mradi,wakati wa ujenzi na kuendesha mradi baada ya kumaliza ujenzi.
 
China ina watu wengi sana masikini wa kutupwa.
400 million wachina waliondoka ndani yatabaka la umaskini ndani ya mwaka mmoja 2016. That is the kind of economic growth reaching down to the people. Ujamaa uliondoka na Azimio la Zanzibar. Hesabu sasa ni miaka mingapi. Na hiyo ndio ilikuwa maana ya mfano wangu huo na China. Muwe mnasoma na kuelewa kilichoandikwa. Kama huelewi uliza.
 
Kaka Paschal waswahili wamo humu jukwaani, kazi wanayoiweza ni kukosoa na kukejeli.

Hayo mambo ya oil and gas ni ya level ya juu sana kwao. Sasa hivi hawashiriki kwenye mijadala halafu kesho utasikia wakisema wanaibiwa na wawekezaji.
Pia Kumbuka :-
1/Mkuu kasema gesi (70%) imeshauzwa kabla ya kuchimbwa,
2/Mh Prof MhongHo (serikali) alisha sema Mabilionea wa TZ wana mitaji ya juice na maandazi, hawana pesa za kuwekeza kwenye gesi, tena kwa kuwatisha zaidi akatoa mfano wa kampuni ya kiBRAZIL iliyopewa kitalu ikapoteza mamilioni ya $s na hawakupata gesi.

Kwa msingi huo ni wazi walifukuzwa kwenye ISSUE za mafuta na gesi.

Hivyo ili manilionea wetu wajongee kwenye mambo hayo nilazima wizara husika ifafanue taarifa hizo za Profesa m-bobezi wa miamba na Madini..

NB Bila kujali muda biashara siku zote hulenga faida na si hasara, ukiwa na hakika ya kupoteza fadha huwezi jisumbua na hyo biashara.
 
Pia Kumbuka :-
1/Mkuu kasema gesi (70%) imeshauzwa kabla ya kuchimbwa,
2/Mh Prof MhongHo (serikali) alisha sema Mabilionea wa TZ wana mitaji ya juice na maandazi, hawana pesa za kuwekeza kwenye gesi, tena kwa kuwatisha zaidi akatoa mfano wa kampuni ya kiBRAZIL iliyopewa kitalu ikapoteza mamilioni ya $s na hawakupata gesi.

Kwa msingi huo ni wazi walifukuzwa kwenye ISSUE za mafuta na gesi.

Hivyo ili manilionea wetu wajongee kwenye mambo hayo nilazima wizara husika ifafanue taarifa hizo za Profesa m-bobezi wa miamba na Madini..

NB Bila kujali muda biashara siku zote hulenga faida na si hasara, ukiwa na hakika ya kupoteza fadha huwezi jisumbua na hyo biashara.
Poa, lakini mkuu mimi p mhongo alikuwa sahihi au no , mimi kwangu binafisi yuko right sijui wewe mkuu
 
Wanabodi,
Japo nilipotea, mkutano huu ndio unafungwa sasa na Waziri wa Nishati, Mhe. Dr. Medard Kalemani. Waziri ngeli inapanda.
P
 
Mjadala umefika hapa.
Ukiangalia yaliyoandikwa humu na kuyalinganisha na dondoo za mkutano wenyewe kama alivyoiwasilisha mleta hoja utaona ni jinsi gani tutakavyojikwamua kama taifa.
 
Waziri Kalemani amesema serikali imejifunza mambo matano.
1. Tanzania investment climate is very conducive.
2. Tanzania bado ina good resources kuzalisha faida kwa wawekezaji.
 
3. Lazima kuishirikisha private sector kwa kuongeza PPP kwenye kila mradi
4. Dialogue inahitajika sana.
5. Tunatakiwa kuongeza trust na transparency
 
Back
Top Bottom