From Hollywood to Bollywood, Nollywood na sasa Tollywood. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

From Hollywood to Bollywood, Nollywood na sasa Tollywood.

Discussion in 'Sports' started by WomanOfSubstance, Jun 3, 2009.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Filamu ni moja ya kazi za sanaa zenye kuelimisha, kuburudisha na pia kuingiza kipato.Binafsi napenda sana Filamu na nafuatilia sana maendele ya fani ya filamu hapa Tanzania.Nakumbuka miaka ya nyuma, nyingi ya filamu zilizotamba zaidi katika kumbi za sinema enzi hizo – Drive-in, Avalon,New Chox,Empire, Empress,Odeon ( Dar Es salaam), Majestic kule Tanga, Shaan kule Morogoro, Tivoli - Mwanza, Plaza – Moshi, ni sinema zilizokuwa zinatengenezwa Hollywood na Bollywood kwa maana ya Marekani na India.Polepole majumba hayo yakapoteza umaarufu hasa baada ya watu kuanza kujipa raha wenyewe katika sebule zao kwa maana ya video n.k.
  Polepole Filamu za kinaigeria nazo zikapanda chati na kupendwa sana thanks to Nollywood productions.Kenya nayo ( sijui Kenya inajiita nini katika hizi xxxxwood LOL)haikubaki nyuma katika kutoa burudani na hasa Kiswahili cha Kenya kiliongeza ladha katika filamu hizo.Kama watanzania, nadhani tulipokea changamoto na kuanza kukomaa katika utengezaji wa filamu – tamthiliya, maigizo n.k.Tukaanza kuona nyota zetu zikijitokeza kuanzia akina Onyango, Mama Haambili( RIP) Mzee Jongo (RIP) wakipanda chati kutoka kuigiza michezo ya redio hadi kwenye Filamu za kwenye TV.Vijana machachari kama akina Ray – Vincent Kigosi, Nora, Dr Cheni, Kanumba,Irene Uwoya, na wengine wengi wakaanza kung'ara na kuiweka Tanzania katika ramani – thanks to Tollywood productions.

  Tumeona wasanii wetu kadhaa kama Kanumba, Ray C,Mwisho na sasa Richard Bezuidhouit ( Big Brother winner 2007) wakipata fursa kubadilishana ujuzi kwa kwenda kuigiza na wasanii waliokomaa wa Nigeria kama akina Nkiru Sylvanus, Damijo, Vivien Nnamji,Ngozi Ezeoni nakadhalika.Hii inatia moyo sana.Na kuonyesha kuwa sanaa hii inakuwa kwa kasi, Filamu za Tanzania zinaonyeshwa siyo ndani ya Tanzania tu, bali hadi nje ya mipaka.Thanks to Multi-choice/M-net na TBC arrangements.LAKINI kuna tatizo linalohitaji kushughulikiwa haraka nalo ni la lugha.Nyingi ya filamu zetu ziko kwa Kiswahili which is good.Lakini ili kupanua soko na kuingizia kipato wahusika inabidi kuangalia ni vipi hili litafanyika.Nimeona filamu nyingi zikiwekewa sub-titles za Kiswahili – hii ni mbinu nzuri na rahisi zaidi kuliko kulazimisha wasanii kuigiza kwa kiingereza au ku superimpose kiingereza kwenye filamu za Kiswahili.TATIZO kubwa liko kwenye utafsiri wa maneno kwenye hizo sub-tiles , kuandika maneno ya kiingereza na pia grammar.Binafsi nimekuwa nikijiuliza, kwani wahusika hawatafuti wahariri kupitia na kuhakikisha kuwa kila kitu kiko sawa kabla ya kuzirusha hewani tena nje ya mipaka?
  Hebu tujadili tuone wenzetu hawa tunawasaidia vipi.
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Hapo kuna matatizo makubwa sana, nilipata kusomea fani hii hapa nchini kwa bahati nzuri walimu wetu walikuwa pia ni watengenezaji wa filamu zile za zamani chini chini ya taasisi ya filamu nchini(miaka ya 70 na 80). kwa kweli ukiangalia filamu zao na hizi za new generation akina Ray ni kama tumerudi nyuma hatua mia mbili.Binafsi nilijaribu kutaka kuwasaidia lakini resistance ikawa ni kubwa mno ndio hapo nikagundua kwa nini wasomi wa fani hii hawhusishwi kwenye filamu hizi za sasa, kifupi watengenezaji wa sasa wanatafuta umaarufu na pesa kidogo tu za kula wala hawana nia ya kuendeleza fani hii. Hivyo hayo makosa ya lugha na mengine ni matokeo ya kukurupuka, huwezi kuamini wanaweza kuandika, kupiga picha, kuhariri na kusimika filamu kwa siku tatu..amazing
   
 3. Soulbrother

  Soulbrother JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 408
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  tatizo kubwa ni lack of planning pamoja na budget finyu

  Lingine ni ukosefu wa subira, sinema zetu zinaanza kutengenzwa leo, kesho kutwa zipo dukani... hamna muda wa kuzipitia vizuri kuhakikisha kila kitu kimekamilika
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Burn,
  Asante Ndugu yangu kwa kutumegea uzoefu wako kwenye sekta na fani hii.Kama ni kuganga njaa tu, basi mbona watakosa mengi! Ni kipi bora uwekeze leo uvune kesho au usiwekeze na kesho ukose kabisa.Kwa mwenendo huu , kuna siku watajikuta hawana soko pale watazamaji watakapochoka na mediority - isitoshe kama ni filamu za Kiswahili na zenye kiwango mbona wenzao wa Kenya watawafunika.Tatizo la Watanzania katika almost kila kitu ni kupuuza viwango.Hapa ndipo tunapokosa kitu cha ziada cha kutubakiza kwenye ushindani.
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kwani mchakato mzima wa kuandaa filamu ukoje kwa wale wenye uzoefu?
  Hii inajumuisha kuandaa script,auditions, mpangilio mzima ikiwa ni pamoja na kwenda kwenye location, mikataba mbalimbali...na mwisho lazima kujua fedha kiasi gani itahitajika na itapatikana vipi.
  TUHABARISHENI WENYE KUJUA.
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Moja ya kazi kubwa ya Kenya ni sinema ya Mlevi. Sinema hii pamoja na kuwa na vionjo vya Hollywood na Bollywood, iliweza kuonyesha wazi tabia za waafrika katika kunyanyapa! Tanzania kipindi hicho tulikuwa na sinema za akina Yombayomba. Ubora wa sinema hizo bado upo juu sana kulinganisha na takataka za Nigeria na uigizaji wa video(sio sinema) wa sasa hapa TZ.
   
 7. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tanzania wanaiga uigizaji wa Nigeria.....na hakuna movie nisizozipenda kama zile za kinigeria they have same story kila movie na lazima uchawi uwepo!...inaonyesha jinsi gani watu wanavyo believe uchawi......Kiwango cha movie tanzania bado ni changa sana we have long way to go...kutengeneza movie ni kazi kubwa sana kwanza you need to find a story and to write a story siyo kitu cha lelemama...
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Asante Kibs!
  Umenukumbusha sinema ya Mlevi - yule bwana alivyolowea kwa hawara hadi mkewe nyumbani anakaribia kufa -- bwana yule akiimbiwa
  Darling go home..there is nothing more to say..sijui mamaa ndo alishadedi!
  Anyway... ulivyosema ni kweli kabisa...kuna Yombayomba na Harusi ya Mariam - iliyoigizwa na akina Theckla Mjata na wengine kutoka kitivo cha sanaa za maigizo UDSM.
  Hivi, Chuo kikuu wao wanamchango gani kuboresha hii fani ya Filamu?
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Yaani!
  WaTz wameshaanza kuiga hayo ya Uchawi wa kinaigeria siyo tu kwenye Filamu bali hata kwenye maisha.Kila leo unasoma au kusikia wasanii wakiendeana kwa waganga!
   
 10. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Hiyo mambo ya uchawi in real life nimeisikia sana...tena nasikia hiyo kasumba wanayo wanawake sana...kuna this guy a friend of mine anasema alivyokwenda bongo mama yake alimwambia ukikutana na mwanamke anataka kukusalimia kwa mkono usimpe mkono anakuwa anataka kukuvuta na once akishakutia mkononi tuu basi utaanza kuwa zezeta...I think tanzania sasa tunakwenda kubaya sana....wanawake hawapendi mtu kama siyo pichi yako!zamani ilikuwa kwa wanawake wa certain age sasa hivi nasikia watoto wadogo sana start 18years old.......this is typical nigeria style....
   
 11. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2009
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hii thread nimeipenda na nina uhakika nitajifunza mengi kuhusiana na film industry ya Tanzania.

  -Development(bajeti,kudraft script, kuiandika mpaka kufikia kwenye kuwa final script tayari kwa kutengenezea filamu)

  Pre-production (waigizaji wanatafutwa, eneo la kutengenezea linatafutwa, na vitu muhimu vyote vinakamilishwa kama kutengeneza sets)

  Production (kushoot na kurecord kila kitu tayari kwa editing na for post production)

  Post-production ( hapa ndipo kwenye kazi, maana kila kitu kuanzia visual effects[my area], sauti zinaingizwa, muziki, na vikolombwezo vyote vinavyotakiwa.)
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Speaking of content now,
  Hivi wenzetu wanapoigiza wanakuwa na story au script yenye ku highlight hiyo story? Mara nyingi nimeshindwa hata kuelewa ujumbe au maudhui kuu inayoonyeshwa.Utakachoona ni ama mwanamke kakutana na mwanaume kwenye mazingira ya kuchekesha kama siyo ya kushangaza..mara wamependana... the usual stuff.Hapo utaona watu wanaishi lavishly bila kuonyesha wanafanya kazi gani - sana sana utasikia wakizungumzia mzigo umeshaingia au kutoka bandarini.Ni mzigo gani huwezi kuona au hata kuelewa.This is also typical Nigerian.Ningetegemea tuone maisha ya ama middle class na shughuli wafanyazo kufikia huo u middle class ( hata kama ni ufisadi hahah) na kama ni shughuli zisizo halali basi tuone angalau mwisho mbaya kama kukamatwa, kufunguliwa mashtaka na kuishia jela.Vinginevyo basi tuone maisha ya kawaida ya Mtanzania wa kawaida akiishi nyumba za kawaida na kuwe na story inayoendana.Matokea ya kuangalia kusadikika life - watu wengi wanavutiwa na image zinazoonyeshwa za maisha ya majumba makubwa kama mahekalu yenye spas, jacuzzi,60 inch plasma TVs, nicely dressed beautiful women and men! Hivi haya ndiyo maisha halisi ya kila Mtanzania?
   
 13. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  I don't know kama kuna can answer me this…I have noticd this like on the script right ok I know character names must be capitalized but utakuta some words are completely capitalized..and why is that?...and what kind of words should be capitalized…nous,pronouns,actions or sounds?..
   
 14. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2009
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Sijawahi kuangalia filamu yoyote ya kitanzania ila kwa kusikiliza watu wengi tatizo liko kwenye script na kwenye sets(sijui kama wana ma-production designer wanaojua kazi zao).
   
 15. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ninazo nyingi tuu kutakufanyia dublicate alafu nikutumie shem wangu uweze kuangalia pamoja na za kinigeria kama unataka pia....ushindwe mwenyewe.
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  WomenofSubstanc:

  Kuna tatizo la kusahau mapema sana miongoni mwetu. Hebu jiulize ni wangapi ambao wanakumbuka kuwa Tanzania ilikuwa na Shirika la Filamu? Ni wangapi wanaokumbuka kuwa Zanzibar kupitia TVZ walitengeneza sinema ngapi za Dr. Ayubu? Ni wangapi ambao waliweza kuona sinema za kitanzania kama za kina Yombayomba?

  Tanzania ilikuwa na Tv kuanzaia mwaka 1974- Zenj huko, Kilimanjaro walikuwa wakiangalia KTN mpaka miaka ya akina Mengi. Baada ya vita ya vita vya Kagera, wananchi wengi waliweza kuona video(betamax) na ni baada ya Wanajeshi wetu kusweep Tv na beta huko Kampala. DSM walikuwa wakiona video na TVZ, antena zikaanza kupanda katika baadhi ya nyumba. Hata hivyo soko la movie lilikuwa bado lipo juu sana.

  Wengi wanamkumbuka Hammie Rajabu, mkurugenzi mzalendo katika sinema(muvi) za kibongo, kulikuwepo na hata magazeti yaliyo kuwa yakisambaza habari ya utengenezaji wa filamu hapa nchini.

  Ni wakati mwingine wa kuangalia kwa nini TFC ilianguka..! Kumbuka hawa ndio waliokuwa wakipreview muvi toka hollywood na kwa Wadosi. Na kupanga aina ya watazamaji wa movie hizo. Kufa kwa TFC kulipelekea hata kufa kwa majumba rukuki ya movie uliyoyataja hapo juu(ingawa umekuwa mbinafsi kidogo katika kutaja... Kila mkoa ulijitahidi kuwa na jumba la sinema, mf. Arusha walikuwa na Metropol na jumba jingine mkabala na barabara ya uhuru au karibu na shule ya msingi ya Uhuru, Mbeya nao opposite na posta, Shinyanga, Majestic, Malindi huko ZNZ n.k).

  Je ni mfumo wa uchumi wetu ambao ulisababisha kadhia hii, Je hii ilikuwa ni mabadiliko ya utazamaji tu wa sinema, Je hii ilichangiwa na kuanza kuanguka kwa sekta ya Viwanda Tz? Kuanguka kwa vipato kwa wananchi wa kawaida? Je ni kwa kuwa na mapenzi zaidi kwa movie za kidosi? Je kulisababishwa na kuingia/kuanzishwa kwa Tv Tanzania Bara?

  Mbona jirani zetu Kenya waliweza kuendelea? Au kuja kwa Tv na video kuliweza vipi kuangusha soko la movie nchini pasipo kugusia uwezo wetu kiuchumi miaka hiyo?

  Maswali ni mengi, watu wanapenda kuona movie, hata hivyo system imewafanya waangalie hata movie ambazo zipo chini ya viwango. Na hizi ni video za Nigeria, movie toka China, Thailand na Malaysia.

  Au Wawekezaji katika sekta hiyo walichelewa kuungana na wenzao wakati wa ujio wa digital sound? Movie complex na cine complex?

  Ni mengi ya kujiuliza, na itapendeza kupata maoni ya watanzania ambao wapo kwenye soko la movie huko LA kama akina dada Chiku. Ili kuweza kujua ni nini chanzo hasa cha kuanguka kwa movie na kukimbilia kwenye video zilizochini ya viwango!
   
 17. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kibs ( hope u dont mind me calling u this shortform)
  Asante kwa kuleta maswali ya msingi kabisa.Nimetaja baadhi ya majumba ya sinema kwa vile ndiyo niliyowahi kufika ndugu yangu na siyo kwamba nimependelea LOL.
  TFC sijui hata iliishia wapi.Najua Mkurugenzi wake Martin Mhando yuko Australia kwa sasa na anafanya maajabu kwenye movie production na hata kuna kipindi aliwahi kuja Tz kutengeneza sinema na wachezaji wa Hollywood ( including Barbra O.) mwanzoni au katikati ya miaka ya 90 kama sikosei.Cine Club ni moja ya miundombinu ya TFC na sasa imegeuka sehemu ya starehe - kunywa na kula na sijui hata wanaoenda pale wanajua historia yake.
  Anyway ni vizuri kuangalia tumetoka wapi na tunaenda wapi,wapi tulikosea na tunaweza vipi kurekebisha.Ngoja tusikie na wengine watasema nini.
   
 18. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2009
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  @Kelly01, Ahsante kwa offer yako, ikifika wakati wa mimi kutaka kuziangalia hizo filamu nitakustua.

  Wakati huo huo tujiulize
  I.tunataka kutengeneza filamu za aina gani na za quality hipi,(design ya Nigeria au Hollywood)?
  II. soko la hizi filamu zetu litakuwa ni nyumbani tuu au la kimataifa?
   
 19. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Unakumbuka miaka ya tisini, jinsi watz wengi walivyoanza kuhifadhi kumbukumbu za arusi na matukio mengine kwenye mikanda ya video?Unakumbuka ni katika miaka hiyo hiyo mambo mengi yalianza kurekodiwa, ni katika miaka hiyo hiyo ndio kwa mara ya kwanza wengi wetu tuliweza kuona tamithilia katika Tv na video na katika miaka hiyo hiyo ndio tulianza kuona bendi zetu katika Tv na video na mbaya zaidi ni katika miaka hiyo hiyo Tanzania ilikuwa ni nchi ya ruska na kwa uchungu zaidi hapakuwepo na chombo chochote cha kusimamia ubora wa video hizo.

  Huo ndio ulikuwa ni mwanzo wa kwenda kombo katika fani hii, kuanzia serikali kuu, asasi za burudani na wananchi wenyewe walikaa kimya na kushangilia kuvamiwa kwa fani ya sinema. Hata wale ambao walipendeza zaidi katika tamithilia za redioni walijiunga katika mfumo mpya wa video.

  Kukosekana kwa mamlaka ya kusimamia utengenezaji wa video hapa nchini ndio kumesababisha kuwepo na vurumai kubwa katika uzalishaji wa video nchini. Hii ina maana kuwa hakuna viwango vyovyote vinavyofuatwa ili kulinda utamaduni na maadili ya watanzania.

  Hakuna usimamizi wowote wa kukuza lugha ya taifa katika video hizo, hakuna usimamizi wowote wa kuona kuwa yanayoonyeshwa katika video hizo hayawezi kuathiri maisha ya ukuaji wa watoto wetu. Na hii yote imetokana na kuto kuwepo na chombo mahsusi kwa ajili hiyo.

  Ndio maana leo hii hata hizo subtitles zinaandikwa kutokana na utashi wa muhusika wa uandaaji wa video hiyo. Ninavyo elewa katika nchi ambazo wanatabia ya kuweka subtitle, huwa sio kazi ya Producer, Director au Editor. Bali ni kazi ya kampuni iliyopatiwa leseni ya kufanya hivyo.

  Je hapa kwetu Tanzania utafsiri wa video unasimamiwa na nani, leseni ya kazi hiyo inatolewa na nani, na ni nani anawajibika kusimamia hilo?
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Jun 4, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,471
  Trophy Points: 280
  Ulichosema hapo juu ni kweli kabisa pia kwa kuongezea ni lack of exposure also. Labda wengi wa watengenezaji wa sinema wa Kitanzania baada ya kuona sinema za Kinigeria na jinsi zinavyopendwa na Watanzania wengui basi na wao wakaona ili kupata soko inabidi wafuate nyoyo za Wanigeria.

  Viwango ni tatizo letu lingine kubwa Watanzania. Tunatengeza vitu kwa haraka haraka ili kupata senti mbili tatu na hapo tunaridhika. Ndiyo maana humsifu sana mengi kwa kuweza kumaintain viwango vya kimataifa katika bidhaa mbali mbali toka katika makampuni yake.

  Hawa watengenezaji sinema zetu nchini hawana malengo ya muda mrefu wala vision ya kuongeza ukubwa lwa soko lao, wameridhika na soko la ndani ambalo nalo wana ushindani wa hali ya juu hasa kutoka katika sinema za Kinigeria. Wangekuwa na mtazamo wa mbali basi wangehakikisha wanayaingia masoko ya nchi za jirani zetu na kuweza kushinda huko kama wangekuwa na mikakati ya kuinua viwango vya sinema zao katika viwango vinavyokubalika, labda hapa napo lack of capital inachangia kwa kiasi kikubwa kwa wao kushindwa kuwa na mtazamo wa mbali na kuhakikisha wanapanua soko lao hadi nchi za jirani.

  Pia labda kubadilishwa kwa majengo yetu ya sinema enzi hizo Avalon, Express, Drive in, Empress, New Chox, Empire na ama kuwa ya biashara nyingine au pale Drive in kujengwa Ubalozi wa Marekani kumechangia kwa kiasi kupunguza exposure ambayo wangeipata katika sinema za kutoka nje.

  Nakumbuka enzi zile mnaingia sinema kigroup kama cha watu 20 hivi au hata zaidi ilikuwa ni raha iliyoje na ni outing ambayo miaka ile ilikuwa maarufu sana. Nakumbuka pale Empire ambapo mara nyingi ndiyo walikuwa wanaonyesha sinema za Bruce Lee, enter the dragon, fist of fury n.k. walikuwa wanauza ticket kwa walanguzi kwa saa moja tu baada ya hapo wanadai zimekwisha basi kama umechelewa ni lazima ulanguliwe ticket ta shilingi 10 ulikuwa unaweza kurushwa hadi shilingi 100 ha ha ha starehe za bongo lakini pamoja na kulanguliwa jumba lilikuwa linafurika katika kila show. Sinema za Bruce lee watu walikuwa hawaendi na walimbwende maana inaweza ikabidi uingie vitani ili kuhakikisha unapata ticket ya shilingi 10 badala ya kulangulia na ukishaipata shati lililopigwa pasi liko nyeng'enyeng'e na kibanda au afro utadhani umekisusa miaka chungu nzima maana kimeshatimuliwa hovyo hovyo LOL!

  Kuna raha yake ya kuangalia sinema nyumbani kwenye HD screen lakini haishindi raha ya enzi zile kuingia katika majumba mbali mbali ya sinema. Halafu pale empire kulikuwa na mishkaki ambayo ilikuwa mitamu sana mji mzima kulikuwa hakuna mishkaki mizuri kama pale empire na bi poa kabisa shilingi mbili tu basi njemba zilikuwa zinaagiza mishkaki mpaka au zaidi ha ha ha ha halafu miaka ile wala huogopi kula barabarani maana kulikuwa hakuna kipindupindu 50.
   
Loading...