From Historical Chambers; Slobodan Milosevic rais katili wa Yugoslavia aliyeinjinia mauaji ya kinya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

From Historical Chambers; Slobodan Milosevic rais katili wa Yugoslavia aliyeinjinia mauaji ya kinya

Discussion in 'International Forum' started by KAMBOTA, Nov 11, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Slobodan_Milosevic_picture.jpg
  Na Nova Kambota Mwanaharakati,

  Leo ikiwa ni miaka ni miaka kumi na moja tangu vikosi vya NATO vikiongozwa na Marekani kuung’oa utawala wa rais wa zamani wa Yugoslavia Slobodan Milosevic mnamo mwaka 2000 bado wanahistoria kutoka kila pembe ya dunia wanazidi kumiminika nchini humo kutafiti moja ya migogoro ya kinyama kabisa kuwahi kutokea ulimwenguni uliofahamika kama “vita ya Kosovo” huku kumbukumbu na ushahidi wa wazi ukimtaja dikteta Slobodan Milosovic kuwa ndiyo haswa mtu aliyechochea uovu huo.

  Slobodan Milosevic alizaliwa mnamo tarehe 20 Agosti mwaka 1941 katika eneo la Pozarevac lililoko Serbia huku akitokea kwenye kabila la Vajocevici kwa maana nyingine Slobodan Milosevic alizaliwa wakati wa vita kuu ya pili ya dunia huku akilelewa katika imani ya kanisa la Orthodox. Mikosi ilianza kwa wazazi wake ambapo mwaka 1962 baba yake mzazi alijiua mwenyewe kwa kujipiga risasi , mambo hayakuishia hapo kwani miaka kumi baadaye yaani 1972 mama yake mzazi ambaye alikuwa ni mwalimu naye alijiua mwenyewe kwa kujinyonga.

  Baada ya kuhitimu masomo yake ya awali na sekondari mnamo mwaka 1961 Milosevic alijiunga na chuo kikuu cha Belgrade akisomea shahada ya sheria hadi alipohitimu mwaka 1966. Akiwa chuoni Slobodan Milosevic alianza mikakati yake ya kujijenga kisiasa ambapo inaelezwa kuwa alijenga urafiki mkubwa na Ivan Stambolic ambaye alikuwa mpwa wa waziri mkuu wa Yugoslavia wa wakati ule Petar Stambolic. Milosevic hakuishia hapo aliendeleza mbwembwe zake kwenye siasa kwa kujiingiza kwenye tawi la vijana la chama cha kikomunisti cha “Yugoslav Communist League”.

  Tarehe 16 Aprili 1968 Slobodan Milosevic alianza kuvuna matunda ya urafiki wake na familia ya Stambolic kwani akisaidiwa na familia hiyo iliyokuwa kwenye nafasi za juu za uongozi aliteuliwa kuwa meya wa mji wa Belgrade na mwaka 1978 akateuliwa kuwa mkuu wa moja ya mabenki makubwa nchini Yugoslavia ilijulikana kama “Beobanka” . Akiwa kwenye nafasi hiyo Slobodan Milosevic aliendelea kujiimarisha kisiasa huku akijiegemeza upande wa wafanyakazi wa iliyokuwa Serbia ya kikomunisti.

  Mbinu zake za kujishikiza kwa wafanyakazi zilimzalia matunda mnamo tarehe 21 february mwaka 1986 ambapo umoja wa wafanyakazi wa nchini Serbia walimsimamisha kama mgombea wao katika kiti cha urais. Akiungwa mkono na wafanyakazi wengi Slobodan aliibuka kidedea na kukalia kiti cha urais wa Serbia huku pia akiwa mjumbe kwenye baraza la urais la shirikisho la Yugoslavia ambapo Serbia ilikuwa mwanachama pamoja na nchi nyingine kama Montenegro, Bosnia, Albania na Croatia.

  Baada ya kukamata madaraka ya urais nchini Serbia Slobodan Milosevic aliasisi kile kilichoitwa “Anti-beaucratic revolutions” katika azma yake ya kuendesha vuguvugu la utaifa nchini Serbia na kwenye nchi nyingine katika shirikisho la Yugoslavia. Milosevic alitaka kuwaunganisha waserbia wote kuanzia walioishi nchini Serbia na wale walioishi nchini Croatia, Montenegro, Albania na Bosnia, mwenyewe alinukuliwa akisema “I want to build a Greater Serbia” akimaanisha anataka kujenga dola kubwa la waserbia. Matendo ya Slobodan yalichochea vita ndani ya shirikisho la Yugoslavia.

  Kufuatia kile kilichofahamika kama “Anti-beaucratic revolutions” Slobodan Milosevic alichochea mapinduzi kwenye mataifa mengine ndani ya shirikisho la Yugoslavia huku akishikilia msimamo kuwa waserbia ni lazima watawale. Milosevic alizidi kuishangaza dunia ambapo aifanikiwa kuzipindua nchi zote za shirikisho la Serbia na kuweka vibaraka wake lakini lililo la ajabu zaidi ni kuwa hata kuliko na waserbia wachache kama Croatia, Montenegro na Albania kote alihakikisha waserbia ndiyo wanaongoza. Katika vuguvugu lake hili Milosevic alipambana na upinzani mkali katika jimbo la Kosovo nchini Bosnia ambapo inaelezwa waislamu wa huko walipinga vikali uongozi wa waserbia wa kupachikwa na Milosevic hivyo kuzusha vita ya wabosnia dhidi ya jamii ya waserbia ambao walikuwa wachache tu.

  Mnamo mwaka 1997 kwa kutumia ushawishi wake na vibaraka wake aliowaweka kwenye nchi nyingine ndani ya shirikisho Slobodan Milosevic alifanikiwa kumsaliti swahiba wake waliyesoma wote Ivan Stambolic aliyekuwa rais wa shirikisho la Yugoslavia ambapo alimpindua kwa staili ya kumshinikiza ajiuzulu hivyo yeye akateuliwa kuwa rais wa shirikisho la Yugoslavia . Wanahistoria mashuhuri duniani wanaeleza kuwa kuteuliwa kwa Slobodan Milosevic kuwa rais wa Yugoslavia ilikuwa ni fursa yake aliyokuwa anaiota na kuitamani kila siku ya kuwashughulikia wabosnia wa jimbo la Kosovo waliokuwa wanapingana na sera zake za chini kwa chini alizozianzisha akiwa rais wa Serbia.

  Dunia ilishuhudia unyama wa aina yake pale Slobodan Milosevic alipoanza kugawa silaha za vita kama sio za moto kwa waserbia walioishi nchini Bosnia ambapo aliwapa jukumu moja tu nalo ni kuwateketeza wabosnia hasa wa madhebu ya kiislamu ambao walimpinga vikali, Milosevic hakuishia hapo aliwapa silaha hata baadhi ya wananchi wa Serbia na kuwaambia waende kusaidia ndugu zao walioko Bosnia katika kujenga kile alichoita “The Great Serbia”. Dunia iliona unyama wa hali ya juu, watu waliuwawa kama kuku, walichinjwa hovyo, Kosovo ikageuka sehemu ya kutisha duniani kwa mauaji ya mamilioni ya watu wasio na hatia huku Slobodan Milosevic akisistiza “I want to build a Greater Serbia”

  Katika kumaliza unyama ulioendelea kwenye jimbo la Kosovo majeshi ya NATO yakiongozwa na Marekani walifanya mashambulizi ya kijeshi kuanzia mwezi machi mpaka juni 1999 katika jimbo la Kosovo na kuzima mauaji yaliyokuwa yakifadhiliwa na Slobodan Milosevic huku wito ukitolewa wa kufanyika uchaguzi mkuu wa Yugoslavia . Katika uchaguzi uliofanyika septemba 24 mwaka 2000 kiongozi wa upinzani Vojislav Kostunica alimshinda Milosevic katika kinyang’anyiro cha urais hata hivyo Milosevic hakuyakubali matokeo hali iliyochochea maandamano nchi nzima ambapo katika kujibu mapigo Milosevic alianza kuuwa watu wake huku akisisitiza yeye ndiyo rais.


  Majeshi ya NATO yaliingilia kati na kufanya mapinduzi ambapo mnamo Machi 31 mwaka 2001 Slobodan Milosevic alilazimika kukabidhi madaraka kwa kiongozi wa upinzani Vojislav Kostunica na baadaye tarehe 28 juni mwaka huohuo alitiwa nguvuni na kufikishwa kwenye mahakama ya kimataifa mjini The Heagae akikabiliwa na kesi dhidi ya uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki kwenye jimbo la Kosovo. Hata hivyo mnamo tarehe 11 Machi mwaka 2006 Slobodan Milosevic alifariki dunia ghafla akiwa kizuizini huko mjini The Heagae kabla hata kesi yake kwisha. Kifo chake kilizua maswali mengi huku wengine wakidai kauwawa na mahakama hiyo ya kimataifa na wengine wakisema alijiua mwenyewe kwa kunywa vidonge vya kushusha mapigo ya moyo.


  Mnamo tarehe 21 Machi mwaka 2006 mwili wa Slobodan Milosevic ulirudishwa nchini Serbia na kuzikwa katika eneo la nyumbani kwake kwa asili katika mji wa Pozarevac huku akiacha maswali mengi kuliko majibu kuhusu kuhusika kwake katika mgogoro wa Kosovo. Slobodan Milosevic atakumbukwa kwa tabia yake ya undumilakuwili ambapo alikuwa na tabia ya kueleza masikitiko yake na anavyokerwa na mauaji ya kutisha katika jimbo la Kosovo lakini wakati huohuo akiwafadhili wauaji huku akisisitiza kuwa hakuna kurudi nyuma ni lazima wanaompinga wafe pasipo huruma.

  Nova Kambota,
  +255717 709618
  novakambota@gmail.com
  www.novakambota.com
  Tanzania, East Africa
  Ijumaa, 11 November, 2011.
   
Loading...