Frolent Kyombo: Wasiojua vema mashairi ya wimbo wa Taifa na Kiswahili mkoani Kagera wanaambiwa siyo raia wa Tanzania

Mathias Byabato

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,020
690
Katika mchango wake kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Mbunge wa jimbo la Nkenge (CCM) Frolent Kyombo amelalamikia mateso na adha wanayoipata wakazi wa wilaya za Kyerwa, Karagwe, Missenyi na Ngara katika mkoa wa Kagera kufuatia kuwa mpakani na nchi jirani na kuwa baadhi ya watumishi wa idara za Serikali wanatumia kigezo cha lugha na wimbo wa Taifa kubaini nani ni raia na ambaye siyo.

Kuwa wasiomudu vema lugha ya kiswahili au kutoimba vema mashairi ya wimbo wa Taifa wanaelezwa siyo raia wa Tanzania.

Je, wewe unajua vema mashairi ya wimbo wa Taifa au kwa kigezo hicho nawe siyo raia?

Majibu ya Serikali > Simbachawene: Kupata kitambulisho cha NIDA siyo mwarobaini wa kutokuulizwa uraia wako

Video yake hii hapa tumsikilize katika attchment

 
Haya kwanini msitoe vitambulisho vya uraia?
Tangu kujiandikisha ni miaka 5
 
Kafanye utafiti kuanzia kwa jamaa zako hata katika familia kama wanaweza kuimba vema wimbo wa Taifa au kuongea kwa ufasaha lugha ya kiswahili
Haiwezekani.

Yaani hao wamesoma wapi? Nje ya nchi?

Kama hujui wimbo wa taifa wewe ni mganda
 
Kwa nini usijue kuongea Kiswahili?

Huko wahamiaji wengi.

Tanzania kuna wahamiaji wengi wahusika wapo wapo tu kutwa kukimbizana na Watanzania halisi aka wapinzani.

Jeshi kwa ujumla halifanyi wajibu wao wamejiingiza kwenye siasa badala ya kulinda mipaka ya nchi na raia
 
Kuna watu siyo raia kwa asili, lakini jambo la kwanza wanajifunza wimbo wa taifa kwa ufasaha. Nimelishuhudia hilo kwa raia kutoka mataifa mawili ambayo ni jirani zetu.

Lakini pia, kuna wazaliwa asilia wa mikoa ya Kagera hasa Karagwe & Ngara hawajui kuimba wimbo wa taifa lkn ni raia.
Waliokosa fursa za kusoma shule walau elimu ya msingi changamoto hii ni kubwa sana.

Safari bado ni ndefu.
 
Kuna waru siyo raia kwa asili, lakini jambo la kwanza wanajifunza wimbo wa taifa kwa ufasaha. Nimelishuhudia hilo kwa raia kutoka mataifa mawili ambayo ni jirani zetu...

Kikitumika kigezo cha wimbo wa Taifa kuamua nani ni raia na ambaye siyo nafikiri itakuwa shida kubwa kwa nchi. Labda kama watu hawajui maeneo mengi ya mashambani hata majina ya viongozi wa kitaifa hawawajui kabisa sembuse wimbo
 
Wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu, CCM mwaka 2015 pale Jangwani, wasanii waliambiwa kuanzisha wimbo wa Taifa. Waliikimbia Mic hadi alipoichukua Ruby aliyeanzisha kwa mbine bila uhakika. Watanzania wengi hawafaham wimbo wa Taifa.
 
Wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu, CCM mwaka 2015 pale Jangwani, wasanii waliambiwa kuanzisha wimbo wa Taifa. Waliikimbia Mic hadi alipoichukua Ruby aliyeanzisha kwa mbine bila uhakika. Watanzania wengi hawafaham wimbo wa Taifa.
Nao sasa waambiwe siyo raia
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom