Freemason:Chanzo cha UVIVU na kukumbatia Umasikini USWAHILINI

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Katika pitpita za kimaisha. Watu flani walibuni taasisi ya kuwakomboa kiuchumi waumini wao. Lengo ni kutumia fursa zilizopo nchini ili Kutajirika kihalali na kuongeza spidi ya mafanikio yao binafsi na jumuia yao ya imani. Watu karibu wote wa kipato cha chini waliipinga vikali, Wakidai ni mkakati wa freemason, Wanaletewa mambo ya utajiri ya kifreemason.

Nikasema labda, imani iliwakolea katika kupiga story na jamaa zangu uswahili kwetu ndio balaa. Kila mwenye mafanikio ni freemason bidii yote ya muhusika inafukiwa ndani ya kichaka hiki. Yaani neno freemason limekuwa kama kichaka cha kuhalalisha uvivu, ukumbatiwaji wa umasikini na hofu ya kumiliki pesa.

Kuna sababu nyingi kwa nini tunahitaji nguvu kubwa kuvuka mstari wa umasikini wa mtu mmojammoja.
 
Back
Top Bottom