Freeman Mbowe: Zamani tuliona nchi hii ina udikteta uchwara, ila sasa ina udikteta kamili

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416


Mwenyekiti wa (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kuachiwa huru yeye pamoja na viongozi wengine sita wa CHADEMA na kusema kuwa walipokuwa magerezani wameshuhudia mengi na watayaweka wazi karibuni.

Mbowe amesema hayo alipokuwa nje ya Mahakama ya Hakimu mzaki Kisutu baada ya kukamilisha masharti dhamana ambapo kila mmoja alitakiwa kuwa na wadhamini wawili pamoja na kusaini bondi ya shilling Million 20.

"Leo mahakama imetupa ruksa ya dhamana na tunaanza dhamana yetu siku ya leo kwa mashtaka ambayo yananikabili mimi na wenzangu, tumekuwa gerezani Segerea kwa siku saba mimi na wenzangu na tunamshukuru Mungu tuko salama mimi na wenzangu na tumewaona Watanzania wengi zaidi ya elfu mbili ndani ya gereza la Segerea ambao wengi wao haki yao imecheleweshwa kwa hiyo tunasema ni haki iliyominywa, tutazungumza mengi tuliyoyaona Segerea na baadaye tutatoa taarifa rasmi ya chama kuhusiana na kesi hii" alisema Mbowe

Aidha Mbowe aliendelea kusema kuwa "Zamani tuliona nchi hii ina udikteta uchwara ila sasa ina udikteta kamili, tutayazungumza na kutolea ufafanuzi kamili katika muda muafaka" alisisitiza

Source: EATV
 
Walimissjudge the whole situation...afadhali ili wajuwe umuhimu wa katiba mpya sasa!

Katiba tuliyonayo sasa ni kama inampa uhuru huo wa kuwa dikteta, so we have to rely on his mercy...Ndo maana JK aliweza kuzungumza aliyozungumza wakati anamtambulisha Maghufuli...Kuwa mkali kwa kufuata katiba na sheria hakuna shida. Lakini hata hii iliyopo pamoja na sheria zilizopo, havifuatwi!

Hata kushiriki kwenye uchaguzi kwa chadema huwa kunanishangaza sana!
 
Jpm sio Raisi dhaifu kama walivyokuwa wakimuita JK
Udhaifu na uoga wa Kiongozi unakuja pale unapo ogopa kupingwa kwa hoja au unapo chukia kukosolewa, matokeo ya huo udhaifu ndio unakuta maamuzi ya uoga yanaanza, kama kuteka au kuua kabisa anaejaribu kukukosoa, kukutafutia kesi ili akufunge ili akunyamzishe, kuongea kwa maneno ya vitisho au kejeli ili kujaribu kuficha uoga wako, kuongopea watu na kujisifia ili ujaribu kuficha udhaifu, unaweza ukakuta kiongozi anaogopa hata Safari za nje akihofia labda nyuma atapinduliwa, Matoeo ya huo Udhaifu mara nyingi ndio zenyekuleta Udikteta, kwasababu mwisho utaogopa kuachia madaraka kwa hofu ya yale uliyo yatenda kwa uoga. Kwa kifupi TZ ndio tunakotaka kuelekea kwa sasa.
 
Afadhali ya dikteta huyu inaonekana kuna kitu hakipo sawa
Wewe ndiye hauko sawa upstairs. Unakuwa kama bendera kufuata upepo, achana na wanasiasa watakuyumbidha tu otherwise na wewe ni walewale. Wanasiasa wanachotaka ni kutawala hivyo watatumia njia zote za kuidunisha Serikali. Sasa kutokana na umburura wenu mnadhani hao wa upinzani wakiingia hiyo ideal democracy, mnayolilia mtaipata. Wapi wapinzani barani Afrika walipochukua madaraka walibadilika kuwa wa-demokrasia?
 
Zamani tuliona nchi hii ina udikteta uchwara ila sasa ina udikteta kamili, tutayazungumza na kutolea ufafanuzi kamili katika muda muafaka" alisisitiza
Hawa viongozi sijui hawajasoma,hata masharti ya dhamana hayajui,hili la kumsimanga Raisi magufuli pia ni kosa la jinai wasubiri tu akaoge halafu wamueende tena.
 
Back
Top Bottom