Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe: Uchaguzi Mkuu wa 2020 CHADEMA hatukuwa na wagombea sahihi

Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amekiri kuwa walikuwa na baadhi ya wagombea ambao hawakuwa wakikubalika kwenye maeneo waliyogombea nafasi mbalimbali ikiwemo ubunge na madiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Pia, amesema kwa sasa falsafa zake za kisiasa zinakwenda sawa na zile za aliyekuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Marekani, Thomas "Tip" O'Neil Jr.

Amesema O'Neil kupitia kitabu chake cha 'All Politics is Local' amesema siri za ushindi za chama cha siasa ambazo ndizo anazutimia kuongoza mapambano ya kushika dola nchini. Amezitaja falsafa hizo kuwa ni chama kupata mgombea sahihi na nayekubalika kwa wapiga kura.

"Nikiri kuna maeneo mengi tulikuwa na wagombea sahihi, lakini kuna maeneo kadhaa tulikuwa na wagombea dhaifu, huo ni ukweli na haupingiki kwa sababu waswahili wanasema wali wa kushiba unaonekana kwenye sahani," amesema Mbowe.

Ametaja jambo la pili kuwa ni chama kuwa na ajenda ya kuwashawishi wanachi kukichagua, ambapo kwa upande wa Chadema, Mbowe amesema hakijawahi kukosa ajenda ya kushindana na Chama tawala-CCM.

"Ilani yetu ya uchaguzi ilikuwa bora kwa sababu imefanyiwa utafiti," amesema.

Mambo mengine ambayo Mbowe ameyataja ni kuwa na uongozi imara na rasilimali fedha ambapo kwa sasa chama kinatengeneza miundombinu rafiki ikiwemo kuwekeza kwa vijana na kukuza teknolojia kutoka analojia kwenda dijitali.

"Sasa hivi wanachama wa Chadema ni ambao hawazidi umri wa miaka 45 hii ni dalili nzuri kwamba, upinzani utakuwa imara zaidi lakin pia tunapambana kuhakikisha kila kitu tunachokifanya kinafanyika kidijitali," amesema Mbowe.

Kiongozi huyo amesema kikao cha Kamati ya Utendaji ya Chadema Kanda ya Victoria kimeafiki kuwa kila Jumamosi kuwa siku ya kuvaa sare ya Chama hicho kwa wanachama wake.

"Tunatambua kuwa wana Chadema walikuwa wameshaanza kusahau hadi kuvaa sare, lakini sasa wanachama wa Chadema watavaa sare kila Jumamosi ili kuongeza motisha na idadi ya wafuasi wetu," amesisitiza.


Chanzo:
Mwananchi
 
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amekiri kuwa walikuwa na baadhi ya wagombea ambao hawakuwa wakikubalika kwenye maeneo waliyogombea nafasi mbalimbali ikiwemo ubunge na madiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020...
Kumbe hawakuibiwa kura na mwendazake?
 
Nilishasema kuna bifu Kati Lisu na mwenyekiti wake haya sasa wale wapambe nuksi njoeni tena.
Utabiri wangu Mbowe atadondoshwa na Lisu maana Ile mashine sio mchezo.
''Kuna baadhi ya maeneo tulikuwa na wagombea dhaifu''Lissu kaingiaje hapo.
 
sasa mlikua mnamsingizia Magufuli ili iweje ?

mi naanza kua na wasi wasi hata waliompiga risasi Lisu …
 
''Kuna baadhi ya maeneo tulikuwa na wagombea dhaifu''Lissu kaingiaje hapo.
1.Tulikuwa na wagombea dhaifu ikiwemo ubunge na udiwani,2.tulikuwa na wagombea dhaifu katika ubunge na udiwani,hizi ni kauli mbili zenye mtazamo mmoja Ila maana tofauti.kauli ya Kwanza ndo kaisema Mbowe na ndiyo inayomaanisha hata kwenye urais mgombea alikuwa dhaifu
 
Anaanza kutoa siri
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amekiri kuwa kushindwa kwa CHADEMA kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kulitokana na kuweka wagombea dhaifu kwenye nafasi mbalimbali ikiwemo uraisi na hivyo wamejifunza na uchaguzi ujao wataweka wagombea wenye nguvu na ushawishi watakaozunguka nchi nzima kunadi sera na ajenda za wanachi...
 
Aliyemtesa Mbowe, anatetewa na Lissu.

20210602_200509.jpg
 
Hapa kuna mgogoro wa ki maslai kabisa....kwa kuwaza tu napata picha ya usaliti ndani ya chama.. Yan kusalitiana.
Wameona kama mambo ni mepesi vile na wanaweza chukua dola next election sasa wameanza kuvurugana wenyewe, siasa ni mchezo hatari mno.
Wa ughaibuni atakuwa na wakati mgumu sana kutengeneza team ya kumsapot na huyu wa home yeye kashaanza kurudisha nyumbani majembe yake yaliyochukuliwa kilazima na yeye mwenyewe aliyakataa na nafikir sio mara moja.

Kusema kuwa wakirudi na kutubu maana yake ni kuwa kwa sasa wanaweza kurudi,,, tunapima upepo wa wanachama wengine hasa BAWA. C. H. a... Baada ya muda watarudi lakin hawatakiri kosa maana hawawez sema kuwa walifog sign zile... Na kwa kuwa wanaushawish mkubwa basi mzee anajitengenezea allies wake na taratibu ant wa ugaibuni anawekwa pemben ya reli...

Uchaguzi ujao tusishangae sana kumuona alkaeli akigombea uRais,,,na huyo mwingine hatakuwa na support hapa ndani unless ajiengue na kuweka chama chake kabisa. Siasa n mchezo wa faida raia tu huku chuni ndio hufia vyama.

CDM ni chama private na hakitakaa kiwe na mfumo wa waz wa kubadilisha mwenyekiti... Sasa chama kimeshindwa kujiendesha kama taasisi za kisasa kwa kuogopa fraud kutoka vyama vingine kitaweza kweli kuendesha nchi kikipewa ridhaaa?

Anyway sisi wapiga kura, tutachagua watu na sio vyama
 
Hapa kuna mgogoro wa ki maslai kabisa....kwa kuwaza tu napata picha ya usaliti ndani ya chama.. Yan kusalitiana.
Wameona kama mambo ni mepesi vile na wanaweza chukua dola next election sasa wameanza kuvurugana wenyewe, siasa ni mchezo hatari mno...
Kumbuka Lisu aligalagazwa na Nyarandu kwenye kamati kuu
 
Back
Top Bottom