Freeman Mbowe: TRA walinidai Kodi Bilioni 2, Wakafunga akaunti zangu zote za biashara mpaka binafsi, Wakachukua hela

Dr Mpango ni shahidi Muhimu na anajua kila kitu

Na sasa ana madaraka na mamlaka makubwa ya kusahihisha udhalimu uliofanyika na vyombo vilivyo chini ya wizara ya fedha, BoT na TRA kama kweli wanataka nchi hii irudi ktk utawala wa sheria kwa kuheshimu utu na kufuata katiba ili tuweze kuitofautisha awamu ya sita na awamu ya tano ya mwendazake.
 
Kikundi cha wasiojulikana ambao baadhi walijulikana baadae akina Heri kisanduku, nyaulingo, Bashite, cyprian Musiba wana hali ngumu sana ingawa Bashite katengeneza kikundi cha propaganda mitandaoni cha kumchafua kikwete kwa nguvu kubwa ili kuwasahulisha watanzania juu ya uonevu wao pindi wakiwa madarakani
Mkuu hao wote hawana mwisho mwema, ni suala la muda.
Machozi ya nafsi walizo dhulumu hayawezi kuwaacha salama....
 
Mbowe ni muongo.

Mbowe anasema alifungiwa akaunti zote lakini akaamua kwenda kufanya Biashara Dubai, hizo hela za kwenda kuanzisha biashara Dubai zilikua akaunti gani kama akaunti zake zote TRA walifungia?
Kwa hiyo kama aliuza asset zake lazima akuambie?
 
Sasa naamini kuna kampeni chafu ya kumchafua JPM!

Kama ni toka 2018 alishindwa nini kuitumia ktk siasa za uchaguzi kama ilivyo kwa wanasiasa wetu kutafuta sympath!
Kwan ni formula? Kwan hayo Aliyoonge a ni uongo? Labda kama umeanza siku Hizi kufatilia habar
 
Wewe unahamu ya kuolewa na Mh. Mbowe, maana kila wakati unamtaja taja sana,sasa tuthibitishie kama umepata talaka kwa mumeo ili tumuone Mh. Mbowe kama yuko interested akufanye japo nyumba ndogo ili hicho kigololi chako kitulie.
 
Yaani ujinga na unafiki wetu waTanzania umezidi. Hivi ni kipi Mbowe kaongea ambacho tulikuwa hatukijui? Ni ujangili upi wa Ndugai ni mpya katika macho na masikio ya waTanzania? Ni kitu gani kwenye utawala wa jiwe hakijulikani? Tupunguze unafki twende mbinguni.

Kubambikia watu kesi, Kuua upinzani, kulazimisha watendaji wa serikali kuwa extension ya CCM, polisi kuwa CCM..ni kipi hatukijui?

Well some people here would love to rewrite the history.....BUT.....mitandao haisahau.

Mimi si mshabiki wa Mbowe lakini sidhani kama kuna Mtanzania alinyanyasika kwenye utawala wa Jiwe zaidi ya Mbowe na wale walioonekana wana mawazo tofauti na Jiwe.

Jiwe alikuwa kiongozi wetu. Lakini ntakuwa mtu wa mwisho kukubali kwamba alikuwa anafuata utawala wa sheria! He was simply not a Leader who believed in the Rule of law.

Popote alipo apumzike! Tutamkuta huko!
 
TUHUMA ZA MBOWE ZINAACHA MASWALI MENGI.
*
Mbowe kabla hata ya kujisafisha na uongo wake wa kulewa na kuangushwa na konyagi nyumbani kwa hawara Joyce Mkuya kisha kulitangazia taifa kwamba amepigwa na wasiojulikana, amekuja na igizo jingine kwamba alifilisiwa na akaunti zake zote zilifungwa na TRA!..
Mtu mjinga wewe
 
Watanzania wa wapi unawasemea? Mzunguko wa pesa ulipotea, watumishi wa umma miaka mitano bila nyongeza za mishahara, wafanyabiashara kutwa kubambikiwa kodi wanafungiwa account zao, wewe utakuwa ni mnufaika wa udikiteta wa marehemu magufuli
Kulipa kodi ni wajibu acha porojo minyoo
 
Doto aliteuliwa akiwa maskini lakini sasa ni tajiri kuliko Maelezo
Acha wivu! Ulitaka aendelee kuwa masikini wakati anafanyakazi nzuri na analipwa mshahara na marupurupu? Ungekuwa wewe ungebaki masikini tu?
 
Hongera kwa kinachokujia kichwani kukiandika kwa nguvu zako zote.
Taswira ya Chato peke yake inahakisi vya kutosha ukabila na ubinafsi wa kiwango cha hali ya juu kabisa pasipo shaka yoyote.
 
Hivi meko aliwezaje kuteka akili za mataga kwa kiwango kile mpaka wakamwamini eti kuwa ni mzalendo na anapambana na ufisadi? Ama kweli kuwa CCM inahitaji kujitoa ufahamu.
Magufuli kaacha legacy za kujivunia kama vile kaongeza shule, kaongeza hospital, viwanja vya ndege, barabara za juu na chini, Stand mpya za mabasi kubwa na za kisasa tena katika mikoa mbali mbali, upanuzi wa mabarabara, daraja la salender bridge, nidhamu makazini, kawabana wakwepa kodi, kawabana mashoga, kawabana mateja na wauzaji wao, I mean jamaa kafanya mengi ya maana na ya faida.

Haya ebu na ww nipe legacy ya maana aliyoacha Mbowe kule jimboni kwake kama mbunge maana anakula kodi zetu kupitia ruzuku ya chama na mshahara wa bunge bila kufanya lolote la maana.
 
Mbowe ni tapeli tu

Nae akamatwe kula hela za chama
Utapeli unakuja baada ya kugusa vyanzo vyako vya kutumia upepo wa magufuli kuwapora watu mali zao, muulize polepole ile pesa za ununuzi wa wabunge wa upinzani alipeleka wapi maana wapo waliogoma kununulika
 
Magufuli kaacha legacy za kujivunia kama vile kaongeza shule, kaongeza hospital, viwanja vya ndege, barabara za juu na chini, Stand mpya za mabasi kubwa na za kisasa tena katika mikoa mbali mbali, upanuzi wa mabarabara, daraja la salender bridge, nidhamu makazini, kawabana wakwepa kodi, kawabana mashoga, kawabana mateja na wauzaji wao, I mean jamaa kafanya mengi ya maana na ya faida. Haya ebu na ww nipe legacy ya maana aliyoacha Mbowe kule jimboni kwake kama mbunge maana anakula kodi zetu kupitia ruzuku ya chama na mshahara wa bunge bila kufanya lolote la maana.
Ruzuku ya CCM ndiyo inapigwa sana hata marehemu magufuli kaipiga sana enzi zake, miradi mingi ikiwemo kiwanja cha Ndege cha nyerere flyover vilianza kipindi cha Kikwete yeye kavikuta kamalizia tu cha ajabu sifa zote mnampa yeye, mmesahau wengine, magufuli kaacha legacy ya uonevu kuwabambikia kesi za utakatishaji fedha uhujumu uchumi wapinzani na wafanyabiashara
 
Back
Top Bottom