Freeman Mbowe: Rais Magufuli wawajibishe Viongozi na Wasimalizi wa MV. Nyerere

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Leo Kwanzia Saa Baba Mchana Makao Makuu ya Chadema mwenyekiti wa Chadema Freeman Aikaeli Mbowe Ataongea na wana Habari kwenye Makao makuu ya Chama hicho tutawaletea yatakayo jiri moja kwa moja hapa hapa

Update Kutoka Makao Makuu ya Chadema
-------------------------------------
Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Aikaeli Mbowe anaikosoa Serikali


Freeman Mbowe: Kweli tumekosa taa ya kuona mita 100 ya kuokoa watu, basi tumeshindwa hata kuwasha jenereta kuunganisha umeme? Ina mana wameridhika na kuona kwamba watu wale tayari walishakufa jana

Freeman Mbowe: Kivuko kinauwezo wa kubeba abiria 100, na mizigo isiyozidi tani 20, hadi sasa zaidi ya watu 50 wamepoteza maisha, halafu wahusika wapo wapo tu, hivi hii inaingia akilini kweli

CHADEMA, yamtaka Rais Magufuli kuwachukulia hatua viongozi wote wanaohusika katika sekta ya usafiri, kufuatia tukio la kuzama kwa Kivuko cha Mv. Nyerere kilichozama katika Ziwa Victoria jijini Mwanza kwa kua viongozi hao hakuna aliyeonyesha msimamo.

Freeman Mbowe: Tunasubiri kwa hamu tuone Serikali itatoa orodha ya watu kiasi gani kwa majina na idadi ya watu pamoja na mizigo iliyopo katika kivuko hicho

Freeman Mbowe: Mwenyekiti wa CHADEMA amemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ajitokeze hadharani kuzungumza na watanzania kwakuwa ajali iliyotokea katika ziwa Victoria ni msiba wa kitaifa.

Freeman Mbowe: Tatizo linalotokea hatujajenga utamaduni wa kuwajibika, kwa hili la safari hii sisi kama CHADEMA tunawaomba watanzania wote tupige kelele ili wahusika wajiwajibishe" M/kiti wa CHADEMA akitoa salamu za pole kufuatia ajali ya MV. Nyerere

Freeman Mbowe: Kufuatia ajali hii ya kizembe ya MV Nyerere na kupelekea vifo vya mamia ya Watanzania wenzetu wasio na hatia kama tungekuwa kwenye Taifa linalowajibika, viongozi wanahusika wangeshawajibika kwa kujihuzulu

=======

*Tunamtaka Rais achukue hatua awawajibishe, amewajibisha watu wengi kwa makosa ambayo anadai ni kupambana na ufisadi na mambo mbalimbali kwenye hili tunamtaka Rais achukue hatua.Na asiseme sichukui hatua sababu kauli imetolewa na Mbowe, ajue nimezungumza kama Mtanzania ambae tunauchungu na ndugu zetu ambao wamepoteza maisha* Mhe Freeman Mbowe (FULL PRESS)

Kwa yale ambayo tumeyaona yanaendelea kule kwenye visiwa vya Ukerewe baada ya ajali ya MV Nyerere, bado kama taifa hatuna maandalizi ya kutosha kukabiliana na ajali zinazotokana na vyombo vya usafiri vya kwenye maziwa na bahari.

Jana kivuko kimezama saa 8 mchana kweupe mpaka saa 12:30 hakuna operesheni yoyote kubwa ya uokoaji ya watu wenye taaluma na vifaa vya kuokoa vilikuwepo kwenye eneo la ajali, waliokuwa wanahangaika pale ni wavuvi wadogo wadogo na boti ndogo ndogo, hakuna askari hakuna mwanajeshi, ni kipi kipaombele mbele chetu kama taifa?

Kutokana na vyanzo vyetu idadi ya watu waliokufa imefikia 120 hadi sasa, safari kutoka visiwa vya Bugorora kwenda Ukara ni safari ya dakika 45 hadi saa 1, na kivuko kilichozama cha MV Nyerere ni kivuko ambacho kimepewa heshima ya mtu muhimu katika taifa letu.

Taarifa za awali zinasema Kivuko hiki kinauwezo wa kubeba watu 101 na tani 20 za mizigo, lakini taarifa tunazopewa ni kwamba kivuko hiki kinasemekana kilikuwa kimebeba watu zaidi ya 400 na mizigo kadhaa ikiwemo magari.

Na jambo la kujaza kupita uwezo (overload ) limelalamikiwa mara nyingi na mbunge wetu wa Ukerewe Joseph Nkundi, akiitaka Serikali mara kwa mara ione kwa jicho la huruma hatima ya wananchi wa visiwa vya Ukerewe ili kuwepo na huduma za kutosha ili kuokoa maisha ya wananchi hawa.

Kwa yale ambayo tumeyaona yanaendelea kule kwenye visiwa vya Ukara, bado kama taifa hatuna maandalizi ya kutosha kukabiliana na ajali zinazotokana na vyombo vya usafiri vya kwenye maziwa au kwenye bahari.

Wote mtakumbuka mwaka 1996, tulipoteza zaidi ya Watanzania 1000 kwa ajali katika ziwa hili hili la Victoria kwa ajali ya MV Bukoba, ilistahili kuwa kuwa funzo la kutosha kwetu, lakini mwaka 2011 Spice Island ilizama katika bahari ya Hindi nayo wakafa abiria kwa mamia.

Na watu waliokuja kufanya uokozi waliouita uokozi wao kwa dakika chache tu giza likatanda wakasema hawawezi kuendelea uokozi kukiwa na giza, na hapa sio katikati ya ziwa, watu wamesimama nchi kavu wanakiona kivuko mbele yao.

Hatuna huduma ya uokozi (rescue service) katika maziwa yetu yote, Nyasa, Tanganyika na huku Pwani, rapid reacue services na ni lazima kwenye maziwa yote duniani, ukienda kwenye nchi za wenzetu wamejiandaa kwa ajali kama hizi na hili ni jambo la lazima kuwepo rescue service.

Tumepata majanga mengi makubwa, tunatoa divers Afrika Kusini, pale wanajaribu ku-dive pale ni wale wavuvi ambao hawana hata oxygen hawana mask hawana chochote, Maandalizi yetu kama taifa kwenye rescue operation kama hizi iko wapi?

Kama taifa hatujajenga utamaduni wa kuwajibika, hakuna hata anayetupa majibu kuhusu jambo hili, watu wanakufa hakuna mtu anajiuzulu katika taasisi au mashirika yaliyopewa majukumu na mamlaka ya kusimamia majanga kama haya.

Kuna watu wa TAMESA ambao ndio wanaoendesha vivuko vyote nchini, kuna SUMATRA wanaosimamia usafiri wa majini na nchi kavu, Jeshi la Navy, Police Marine na vyombo vingine mbalimbali, wote ni nani mmoja anawajibika, sasa tukihesabu wahanga waliokufa kwa ajali ya vyombo vya mbalimbali vya kwenye maji, ukiacha hizi boti kubwa zilizochukua mamia na maelfu ya watu, kwenye boti ndogo wanaokufa watu 30 - 40 - 60 katika ajali zinazotokea kila mwezi ni wengi sana, lakini hakuna hata mtu mmoja anayewajibika.

Sasa kwa hili la safari hii, sisi kama CHADEMA, tunawaomba Watanzania wote. tuungane katika hili bila kujali chama cha siasa bila kujali tofauti zetu tupige kelele awajibike mtu mtu na watu wawajibike katika uzembe huu.

Na utamaduni huu wa kuwajibika utasikia mawaziri wanasema mimi sikuhusika, unapotakiwa kuwajibika ni kama unaongoza taasisi ama ofisi ambayo kwa njia moja ama nyingine ingechukua hatua, ungeokoa maisha ya watu hawa.

Kama angewajibika Waziri, Katibu Mkuu na mlolongo wa maofisa katika hizi taasisi za umma Waziri atakaeingia katika nafasi yake hatokuwa tayari, kitu cha kwanza atasema ikizama meli nyingine itakuwa ni zamu yangu, tutaonana tunakuwa na rescue service.

Na sio kwenye mambo haya tu, yapo mambo mengi tunapoteza maisha ya watu kwa uzembe uliotukuka, nchi za wenzetu hawa watu wangeshafukuzwa kazi jana na hata sio leo, lakini kwa Tanzania hii tunayoambiwa Serikali hii inawajibisha watu kwa ufisadi na mambo kadha wa kadha tunasubiri tumuone Magufuli, kama Mawaziri wake na wote hawawajibiki waliohusika na katika uzembe huu wa kusababisha vifo, basi tunataka Rais achukue hatua awawajibishe.

Tunamtaka Rais achukue hatua awawajibishe, amewajibisha watu wengi kwa makosa ambayo anadai ni kupambana na ufisadi na mambo mbalimbali kwenye hili tunamtaka Rais achukue hatua.

Na asiseme sichukui hatua sababu kauli imetolewa na Mbowe, ajue nimezungumza kama Mtanzania ambae tunauchungu na ndugu zetu ambao wamepoteza maisha.

Hivi vivuko havitoshi na mbunge wa Ukerewe amelalamika na sio mbunge yule peke yake, kwenye ziwa Nyasa vivuko havitoshi, tuna taarifa Serikali inafanya utaratibu wa kuongeza meli na vivuko, vyema lakini bado havitoshi, wale watu wana haki ya kupewa usafiri kama wengine wanavyojengewa barabara, watu wanaoishi kwenye visiwa nao wanastahili haki ya usafiri unaotengenezwa na Serikali.

Katika hivi visiwa wanaishi watu kwa maelfu, kivuko hiki kilikuja wakati wa Rais Mkapa, idadi ya watu inazidi kuongezeka kwa kiasi kikubwa, ndio sababu kivuko cha kubeba watu 100 kinaingia watu 400 na mizigo na nawahakikishieni Watanzania wenzangu Serikali haitoweza kutoa orodha ya idadi ya watu waliokuwa kwenye kule kivuko.
Kwa sababu nahakika hakuna manifest, katika utaratibu wa usafiri wa vyombo vya majini, hata ndege ni lazima abiria wote wanaoingia kwenye chombo cha usafiri wajulikane majina na idadi yao ijulikane.

Kwa hiyo leo Serikali ishaanza kusema kutangaza watu wakachukue miili wakazike maana yake ni kwamba hata kuhesabu ni watu wangapi wamekufa na pengine hata hakuna huduma ya kuweza kuhifadhi miili hii. Kwa hiyo ni sahihi wakisema wazikwe mapema, lakini tunachokisema ni kwamba, tunasubiri kwa hamu tuone Serikali itatoa orodha gani ya watu kwa idadi na majina walioingia kwenye kile kivuko na ni mizigo kiasi gani kiliingia kwenye kike kivuko, kuna taarifa kwamba kuba canter imezama kule na vitu vingine mbalimbali.

Huu ni msiba wa kitaifa, tunamtaka Rais azungumze na taifa, isitoshe kwa Msigwa wa Ikulu kupeleka taarifa TBC kwamba Rais anatoa pole, Rais azungumze na Watanzania awape pole, na tunategemea atakapozungumza na taifa, Rais vile vile atautambua msiba huu ni wa taifa na aweze kutangaza maombolezo ya kitaifa.

Lakini vile vile tunaitaka Serikali ijiandae kulipa fidia kwa watu wote waliopoteza maisha na mali zao katika kuvuko kile, utaratibu wa kawaida wa vyombo vya usafiri vinakatiwa BIMA, wale watu lazima watengenezewe utaratibu wa BIMA ili família zao angalau zilipwe fidia, lakini sababu hakuna mtu anayewajibika hakuna mtu anayefanya mambo haya.

Kuna taarifa kwamba kile kivuko kilichozama kilikuwa na maboya machache sana kwa ajili ya watu kuelea watu walikuwa wananyang'anyana maboya na machache mengine yaliyokuwepo yalikuwa kwenye chumba ambacho kimefungwa kwa kufuli ndani ya kivuko.

Bado kuna watu watatoka salama wasiwajibike katika jambo hili, kwa hiyo niseme ndugu zangu Watanzania poleni sana, sisi kama Chama tutashiriki kwa kadri itakavyowezekana kuomboleza na Watanzania wenzetu ambao wamefikwa na msiba huu, Viongozi tunasubiri taarifa rasmi ni nini ambacho kinapangwa kama kutakuwa na mazishi ya halaiki au siku maalum au misa maalum au maombolezo maalum kwa ajili ya waliopoteza maisha yao, Sisi kama Chama tunasubiri kwa unyenyekevu mkubwa kuweza kuahiriki kwa kadri ambavyo vyombo vya serikali vitaelekeza, tutaungana na Watanzania wenzetu kwenda kuomboleza na kuwaombea maisha ya amani wenzetu hawa ambao wametangulizwa mbele ya haki kwa uzembe wa baadhi ya watu, Kwa hiyo poleni sana Watanzania wenzangu.
 
Leo Ijumaa tarehe 21.09.2018 saa saba na nusu mchana , Makao Makuu ya Chama Kinondoni Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe.Freeman Mbowe ataongea na wanahabari Katika mkutano na wanahabari ( Press Conference).
======÷===
 
Monduli.. Hai.. kumemchomaaaa na kwingine

💉💉💉💉💉

Usitujue jue wewe mwenyekiti bomu mlafi.. tuache zetu sisi

Wananchi tumewachoka.. na bado

Endeleeni kujifukia na porojo zenu za kuvaa vibwebwe

Eeeeh asinijuejue.. chama cha michambo ya kike.. na kucheza sasa vigodoro huku wakichamba

Leo sema haku mnikomeeee kwa sauti ya Joti akiigiza.. mtaniambia kasema mpasho upi leo..

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Huyu Mwana anatakiwa akumbushwa swala moja kuu la msingi.

Ni hivi mkuu kabla hujazungumza nikukumbusha kwamba KUPITA NJIA HIYO HIYO KILA CKU ISIKUPELEKE UENDAKO KIMSINGI HIYO NDIYO TAFSIRI YA UPUMBAVU. Labda nikazie kwa kusema hivi

Mwaka 1995 ndio ilikua mara ya kwanza Tanzania kuingia kwenye uchaguzi wa vyama vingi ambapo mzee wa Kiraracha (Mrema) alikua yuko juu kisiasa baada ya uchaguzi akatuambia eti zile karatasi za kura ukizikunja ile iki ilikua inahamia upande wa ccm.

Marehemu mchungaji Mtikila alisema hawezi kuingia kwenye uchaguzi mpaka katiba ibadilishwe ku reflect vyama vingi ikiwa ni pamoja na kubadilisha sheria tume ya taifa ya uchaguzi.

Akatokea maalimu wa Seif kule Zenji na Prof Ibrahim huku bara 2000 wakaleta balaaa HUKU NGUNGURI WAKIWASHUGHULIKIA NGANGARI afu kwa mara ya kwanza tukapata wakimbizi wakisiasa kwenda shimoni mombasa kenya.

Kikatokea kituko kingine ambacho tulipoambiwa CUF wanataka kupindua nchi lakini tulichoonyeshwa ni majambia

Sasa mkuu Mbowe angalia tusije kukusikiliza alafu ukatulalamikia badala ya kutuambia suluhisho
 
Wewe wawapi simumemwambia ombe msamaha ndani ya siku saba ndiyo Leo sasa anakuja kuwapa jani la kuomba msamaha.
 
Wewe wawapi simumemwambia ombe msamaha ndani ya siku saba ndiyo Leo sasa anakuja kuwapa jani la kuomba msamaha.
 
Waandishi wa habari mkipewa nafasi ya kuuliza maswali muulize choo cha kujisaidia kiko wapi? kwa sababu kuna taarifa ofisi hiyo haina choo.Mtupigie na picha mtuwekee.Hii yaweza kuwa habari kubwa kwenye magazeti na yakauzika sana.Choo kipo au hakipo? Mwenyekiti tujibu na utuonyeshe tukione hadi ndani.Waandishi changamkieni hilo swali
 
Waandishi wa habari mkipewa nafasi ya kuuliza maswali muulize choo cha kujisaidia kiko wapi? kwa sababu kuna taarifa ofisi hiyo haina choo.Mtupigie na picha mtuwekee.Hii yaweza kuwa habari kubwa kwenye magazeti na yakauzika sana.Choo kipo au hakipo? Mwenyekiti tujibu na utuonyeshe tukione hadi ndani.Waandishi changamkieni hilo swali
Nenda kaulize wewe si umepewa mdomo WA kuulizia.

Kumbe umatrego sana.
 
Waandishi wa habari mkipewa nafasi ya kuuliza maswali muulize choo cha kujisaidia kiko wapi? kwa sababu kuna taarifa ofisi hiyo haina choo.Mtupigie na picha mtuwekee.Hii yaweza kuwa habari kubwa kwenye magazeti na yakauzika sana.Choo kipo au hakipo? Mwenyekiti tujibu na utuonyeshe tukione hadi ndani.Waandishi changamkieni hilo swali
JE, yule mwenyekiti wa chama cha kijani na njano AKIULIZWA MASWALI KWA LUGHA YA KIINGEREZA taweza kujibu kweli? tunadokezwa kwamba eti kiingereza kinamsumbua sana ndio maana hataki hata kwenda walau Ulaya. Anajiuliza, hivi introduction itakaaje?
 
Nenda kaulize wewe si umepewa mdomo WA kuulizia.
Wahariri waambieni waandishi wenu waulize habari ya choo makao makuu na waje na Story.Waambieni waje na hiyo habari.Kesho iwekeni front page muone mtakavyouza magazeti.Watu wengi wana hamu ya kujua pale makao makuu kuna choo? Kikoje?
 
Monduli.. Hai.. kumemchomaaaa na kwingine



Usitujue jue wewe mwenyekiti bomu mlafi.. tuache zetu sisi

Wananchi tumewachoka.. na bado

Endeleeni kujifukia na porojo zenu za kuvaa vibwebwe

Eeeeh asinijuejue.. chama cha michambo ya kike.. na kucheza sasa vigodoro huku wakichamba

Leo sema haku mnikomeeee kwa sauti ya Joti akiigiza.. mtaniambia kasema mpasho upi leo..

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Wewe nawe ustaarabu wako ndo ulipokomea! Pole sana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom