Freeman Mbowe, nchi kuongozwa na Mwanamke siyo fursa ya kutaka mambo kwa pupa

SOPINTO

Senior Member
Oct 19, 2020
155
385
Kuna wakati kila jambo linahitaji kufikiriwa kwa undani sana, kila mtu katika taifa ana haki yake lakini katika kudai haki yako kuna taratibu nyingi za kufuata pamoja na kufanya uzingativu hivyo ukikosea katika utaratibu huo basi haki yako inageuka kuwa kaa la moto hata kama ni jambo la faida kwako au kwa taifa, mfano wa uhalisia ambao upo sasa hivi ni ule unaoendelea kule Afrika Kusini kuhusiana na kesi ya Jacob Zuma.

Aliyekuwa Rais wa kwanza Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela mapema tu baada ya kutoka Gerezani alifanya kampeini kubwa ya watu weusi kwenda shule na aliwasihi sana waende shule kwa lengo la kupata uelewa mpana wa kudai haki zao nafikiri kuna kitu alikiona kwa watu weusi.

Nirudi hapa nchini katiba ya JMT ya mwaka 1977 imefanyiwa marekebisho mengi tu katika vipengere mbalimbali kulingana na mabadiliko ya sera mbalimbali za ndani na nje aya nchi, hatua za mabadiliko ya katiba mpya zimefanyika mpaka kufikia ngazi ya Rasimu mpya . Hivi karibuni kumetokea vuguvugu la kudai katiba mpya chini ya chama cha Chadema na viongozi wake wakiongozwa na Mbowe kwa kuendesha semina na mikutano ya ndani na nje, hili jambo ni kama limeibuka ghafla tu kwani wakati wa awamu ya tano haya yote hayakufanyika lakini baada ya Rais aliyepo madarakani kutoa uhuru wa kisiasa kwa vyama vya siasa kinachoonekana sasa ni matumizi mabaya ya uhuru huo.

Tafsiri ya haraka haraka niliyoipata kutoka kwa chama cha CHADEMA ni kwamba madai ya katiba mpya imechukuliwa kama agenda ya kukirusha chama katika uhai pamoja na kukijenga chama hicho baada ya kubanwa kwa miaka mitano chini ya uongozi wa mwandezake JPM na akili ya Mbowe na wasaidizi wake walijua kuwa kwa vile aliyepo sasa ni mpya na nguvu yake katika siasa ni mpya na ngeni basi kwa araka haraka kalianzisha vuguvugu hilo la madai ya katiba mpya akifikiri kuwa Rais Samia Suluhu atafungua milango hiyo kwa haraka haraka kama alivyofungua katika mambo mengine ambayo nayo yamepigiwa kelele kwa kipindi kifupi baada ya yeye kukamata nchi mfano wa mambo hayo ni kufungua akaunti zako zilizokuwa zimefungwa kwa mda mrefu na kurejesha fedha zake zilizozuiliwa kwa muda mrefu , kuachilia baadhi ya wananchama waliokuwa wamefungwa akina Mdude Nyagari, kuachilia wafungwa waliofungwa kwa kubambikiwa kesi za Uhujumu uchumi ikiwa pamoja na kuzingatia mambo mengine ya haki na sheria.

Nimshauri Mbowe na wanachama wake kuwa unapoomba maji na ukapewa maji basi husitake kuondoka na kikombe , rudisha kikombe na ukikitaka kikombe anza mchakato wa kuomba hicho kikombe na sio kutaka kuondoka na kikombe kwa vile tu umepewa maji , ukifikiri kuwa na kikombe ni mali yako pia, kiukweli mnyonge mnyongeni haki yake mpeni katika kipindi cha muda mfupi sana Rais Samia amejitahidi kurudisha matumaini kwa watanzania mbalimbali ikiwa pamoja na kurudisha amani na huru mbalimbali tofauti na kipindi cha JPM mfano mzuri ni kwa wewe Mbowe hivyo basi kama chama chako kinadai katiba mpya kwanini chama chako kisifuate taratibu husika kama maelekezo kutoka mamlaka husika zinavyoelekeza mana hii katiba mpya unayoidai sio mali ya chadema ni mali ya taifa na kama ndivyo kwanini ufanye harakati kama vile unadai katiba ya chama chako?

Ni vyema tukatambua kuwa hili ni taifa na kila kitu kinaenda kwa mfumo sio maamuzi ya chama fulani au kikundi cha watu fulani ni vyema pia tukatambua kuwa mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya ni jambo la mfumo ambao tena ni mtambuka sio ajenda ya chama fulani au kikundi cha watu fulani , tunapotaka kutengeneza picha ya madai ya katiba mpya kwa vikundi basi tutambue kuwa tunakarisha yale ya Jacobu Zuma na wafuasi wake kama yanavyoendelea hivi sasa.

KUHUSU KESI YA UGAIDI
Hii kesi Mbowe umeitafuta mwenyewe kwa udi na uvumba na nikwambie tu kuwa kesi hii ni kaa la moto kwako na chama chako, kuna mambo mengi ya kukirudisha chama katika uhai lakini sio kwa mambo ya mihemko kama haya, serikali ipo na vyombo vya ulinzi na usalama vipo, usifikiria kuwa kwa vile yupo mwanamama katika ngazi ya Urais ukafikiri utafanya mambo yako kama unavyotaka, taifa hata likiongozwa na jiwe juwa kuwa kuna mifumo inayofanya kazi usiku na mchana.

Muwe na siku njema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom