Freeman Mbowe na wenzake watuhumiwa kula njama na kumdhuru Lengai Ole Sabaya

Ukifuatilia muenendo wa kesi ya Sabaya utaelewa nini kiko ndani na hukumu yake pia itafanywa ili kuharalisha mashitaki na hukumu dhidi ya Mbowe...

Arusha: Mahakama yatupa pingamizi la utetezi kesi ya Ole Sabaya​

Jump to newIgnoreWatch
[IMG alt="mshale21"]https://secure.gravatar.com/avatar/3921549a33911fcaacc92a646220792a?s=96[/IMG]

mshale21

JF-Expert Member​

Arusha.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imetupilia mbali pingamizi lililowasilishwa na mawakili wa utetezi wanaomuwakilisha mshitakiwa wa pili Sylivester Nyegu katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili.

Uamuzi huo umetolewa leo Agosti 23, 2021 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo ambaye aliahirisha shauri hilo la jinai namba 105,2021 mwishoni mwa wiki baada ya mawakili Edmund Ngemela na Sylvester Kahunduka kuweka pingamizi.

Mawakili hao walipinga mteja wao asihojiwe kwa maelezo ya awali ambayo hayajapokelewa mahakamani kama kielelezo.

Akitoa uamuzi huo mdogo Hakimu Amworo amesema kwa kuwa maswali ya dodoso huwa na kikomo shahidi ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo anaweza kuulizwa maswali yoyote.

"Kwa kuzingatia kifungu cha 154 cha sheria ya ushahidi shahidi anaweza kuulizwa kwenye hiyo nyaraka hata kama haijatihibitishwa ni ya kweli,"amesema.

Baada ya uamuzi huo Wakili wa Mkuu, Tumaini Kweka aliendelea kumhoji shahidi huyo kwa kutumia nyaraka hiyo.

Agosti 20, 2021 mshitakiwa wa pili Nyegu alikuwa akiendelea kuhojiwa na Mawakili wa Jamhuri mabishano ya kisheria yalitokea baina ya Mawakili wa Upande wa Jamhuri na Mawakili wa Utetezi wakati mshitakiwa huyo akihojiwa maswali ya dodoso na Wakili Kweka.

Akimuhoji mshitakiwa huyo Wakili Kweka aliiomba mahakama chini kifungu cha 154 cha Sheria ya ushahidi,kumuuliza shahidi maswali kupitia maelezo yake aliyoandika polisi wakati anahojiwa.

Baada ya Wakili Kweka kutoa ombi hilo Wakili Edmund Ngemela anayemtetea Nyegu aliweka pingamizi na kuieleza mahakama kuwa kifungu hicho kinataka ili nyaraka iweze kutumika kumhoji shahidi ni lazima nyaraka hiyo iwe imeandikwa naye na imepokelewa kama kielelezo.

Wakili Ngemela alieleza mahakama kuwa wakati mshitakiwa huyo anatoa ushahidi wake wa msingi mahakamani hapo alidai hajawahi kuhojiwa na hakuna shahidi hata mmoja wa jamhuri aliyefika mahakamani hapo kusema alimhoji shahidi huyo.

Wakili Sylvester Kahunduka ambaye pia anamtetea mshitakiwa huyo wa pili katika shauri hilo alidai mahakamani hapo kuwa kifungu hicho walichotumia jamhuri kumhoji shahidi kwa maelezo hayo hakijafuata matakwa ya kifungu hicho.

"Katika ushahidi wa msingi wa shahidi anasema hakuwahi kuandika maelezo wala kuhojiwa alichokuwa anamuuliza wakili ni particulars zake ambazo mtu yoyote anaweza kuandika, sasa wakili anatoa maelezo anasema ni ya shahidi,"alidai na kuongeza

"Tunaamini kwamba mteja wetu hatatendewa haki kama hicho kinachosemekana ni maelezo kitaumika kumuuliza maswali kwa sababu hana nafasi ya kuthibitisha kama ni yake, maombi haya yatupiliwe mbali."

Akiwasilisha hoja za nyongeza baada ya mawakili hao wa mshitakiwa wa pili, Wakili Kweka aliieleza mahakama siyo takwa la kisheria kutaka maelezo yapokelewe kama kielelezo mahakamani.

"Mheshimiwa Hakimu, mawakili wasomi katika uelewa wa sheria ukisoma kifungu namba 154 ,unaposema 'made by him' haimaanishi lazima wewe uchukue karatasi uandike, inamaanisha ni maelezo yake au yanamhusu yeye yakaandikwa,"alidai.

"Siyo lazima maelezo hayo aonyeshwe, hayo ndiyo matakwa ya kisheria.Tulichonacho sasa hivi kwa hadhi aliyonayo ni shahidi siyo mshitakiwa na suala la ushahidi linaongozwa na Sheria ya Ushahidi Sura ya sita na hata mwenyewe wakati namuuliza nimuite nani aliniambia nimuite shahidi au jina lake,"amesema na kuongeza

"Tunachoomba kimekidhi matakwa ya kifungu cha 154 cha Sheria ya Ushahidi na nilishaanza kumuuliza maswali kuhusu yeye ni nani, ana hadhi gani katika jamii, siyo takwa la kisheria kutaka maelezo yapokelewe kama kielelezo mahakamani na ni kifungu kingine kabisa,"

"Katika muktadha huo na katika kuokoa muda wa mahakama hoja hiyo itupiliwe mbali na upande wa mashtaka turuhusiwe kuendelea kufanya mahojiano kwa shahidi namba mbili kwa upande wa utetezi, kwani unaweza kuhoji kitu chochote ila ukomo wa anga ndo ukomo wako."

Chanzo: Mwananchi

Thanks Quote Reply
Report
[IMG alt="test man"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/380/380855.jpg?1477543230[/IMG]

test man

JF-Expert Member​

wamuachie tu

Thanks Quote Reply
Report
[IMG alt="EvilSpirit"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/438/438998.jpg?1615986163[/IMG]

EvilSpirit

JF-Expert Member​

Naomba mwenye picha ya Odira Amworo aitupie humu tumfahamu.Tunataka tumuone mtu anayemfanya sabaya awe anaachia vijambo visivyo na sauti kwa kutetemeka

Thanks Quote Reply
Report
[IMG alt="THE BIG SHOW"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/109/109760.jpg?1358417525[/IMG]

THE BIG SHOW

JF-Expert Member​

Senselessness

Thanks Quote Reply
Report

BoldItalicMore options…

Insert linkInsert imageMore options…
UndoMore options…
Preview

Font sizeText colorFont familyListAlignment
  • Align left
  • Align center
  • Align right
  • Justify text
Paragraph formatStrike-throughUnderlineInline spoilerInline code
SmiliesQuoteInsert videoMediaInsert tableInsert horizontal lineSpoilerCodeSubscriptSuperscript
RedoToggle BB codeRemove formattingDrafts

Write your reply...
Post reply

Attach files Insert quotes…

Similar Discussions​

Arusha: Mahakama yamkuta Lengai Ole Sabaya na kesi ya kujibu
6 7 8
Replies 149 Views 7,430
Shahidi awatambua Sabaya na wenzake ndio waliwavamia dukani
2 3
Replies 55 Views 2,040
Arusha: Ole Sabaya na wenzake wamefikishwa Mahakamani, kesi yaahirishwa
16 17 18
Replies 343 Views 13,187
ARUSHA; MAHAKAMA yamwachia huru Mshitakiwa wa uhujumu uchumi Lucas Mdeme
2
Replies 20 Views 1,147
Mahakama ya Afrika Mashariki Arusha: Muendelezo wa kesi ya kuhoji uhalali wa muungano
14 15 16
Replies 311 Views 72,982
Share
Issa SLuu
Edit

Issa SLuu

JF-Expert Member
Messages2,294Reaction score1,779Trophy points2,00

1629715721821.png
 
tulishangiliana sana kesi ya Sabaya kumbe ilikuwa ndoano ile...tusifanye masikhara sana unawezakuta majamaa yanaushahidi mtu akaoga miaka hapa...tusiwaamini sana wanasiasa na kujiaminisha sana kwao..
Itakuwa sawa pia maana zile video za Sabaya kuvamia nyumbani kwa Mbowe ni wakati wake mzuri wa kujua ilikuaje na Sabaya itabidi aieleze mahakama
 
Naona kibatala akiwabana kwa swali dogo sana ".......................................?" ningelisema lakini nimekumbuka kuwa kesi iko mahakamani haturuhusiwi kuijadili
Kwamba kibatala hajawahi shindwa kesi?
 
hao walinzi wake tangu wakamatwe hajawahi kuwaongelea popote ndiyo maana wameamua kumchoma boss wao na haowatakuwa mashahidi pia utaona
Hii kesi mbona ilikuwepo toka siku matokeo yanatangazwa..... Na alikamatwa Mbowe na kina Boniface Jacob eti siku ya maandamano walitaka kulipua vituo vya mafuta. Ila baada ya JPM kuapishwa kesi ikaisha hewani tu.... Kadai katiba naona kesi imefufuliwa.

Hata Akwilina mliwahukumu kifungo mbona Mahakama ya rufaa imebatilisha hukumu?? Vipi Mdude na Sugu wote walionekana hawana hatia!! So sio mara ya kwanza kubambikia upinzani kesi.
 
Hii kesi mbona ilikuwepo toka siku matokeo yanatangazwa..... Na alikamatwa Mbowe na kina Boniface Jacob eti siku ya maandamano walitaka kulipua vituo vya mafuta. Ila baada ya JPM kuapishwa kesi ikaisha hewani tu.... Kadai katiba naona kesi imefufuliwa.

Hata Akwilina mliwahukumu kifungo mbona Mahakama ya rufaa imebatilisha hukumu?? Vipi Mdude na Sugu wote walionekana hawana hatia!! So sio mara ya kwanza kubambikia upinzani kesi.
watanyooka tu walinzi aliwatelekeza walipo kamatwa wametoa siri zooooooooooooteeee
 
Mitanzania ndivyo tulivyo yaani sabuyer huyuhuyu aliyeonekana kwenye video na mabunduki na magari ya namba za UN mpaka UN wenyewe wakatoa tamko, hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaa nacheka kama mazuri, basi sawa
 
Huyo huyo mkuu. Sasa anatakiwa kuwa shahidi namba moja kwenye kesi ya Mbowe.

Kule kisongo yuko chuo cha kupangua hoja . Anajifua aje amalizane na Mbowe huku Dar.

Kuna viini macho vingine vinafurahisha sana. Anyway, baada ya JPM kuaga dunia, kuna la kujifunza. Alipokuwa hai kuna waliotetemesha sana. Na alipokufa, kuna watu walikimbilia haraka kufikiria muda umefika sasa wa kufanya lolote wanalotaka.
It has become a double edged sword.
Inakata ya kale na inakata ya sasa. Haijalishi
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom