Freeman Mbowe na Mr.II Sugu wafanya kweli Iringa!

Gagurito

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
5,600
803
Jana Mh. Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM pamoja na Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini walifanya kweli katika mji wa Manispaa ya Iringa.

Shughuli hii inafuatia kuwapo kwa Uchaguzi mdogo katika kata tatu za Kitanzini, Gangilonga na Kihesa zilizopo hapa mjini.

Katika Mkutano ule Mbowe alinukuliwa akisema kuwa Kinachotea sasa SI MPANGO MZIMA TU BALI NI MPANGO WA MUNGU, Kwamba kumekuwepo njama za kutaka kukatisha harakati za Kupigania Mabadiliko zifanywazo na Chadema lakini kwa Kudra za Mwenyezi Mungu Harakati zinasonga mbele.

Mbowe pia alitumia nafasi hiyo kuwataka wanachama wa chama cha mapinduzi wawaunge mkono chadema kwani ndicho chama haswa chenye nia thabiti ya kutaka kuleta mabadiliko kwa maendeleo ya watanzania, Mwenyekiti Mbowe alimalizia kwa Kuwaombea Kura madiwani wake.

Mh. Sugu kama kawaida alifunga mkutano kwa Mistari na kusisitiza kuwa Chadema ni dume la mbegu kweli na kuahidi kudhihirisha hili katika shughuri ya Igunga coz kwa mpango wa chama Muziki rasmi utaanza trh 25 Sept 2011 timu ya Makamanda itakapo wasili rasmi kwa Kazi!
 
Mbona kuna mtu humu jamvini huwa anasema eti Sugu alipata division four mtihani wa form four sasa hii thread ina ukweli gani?
 
This is good. pilika pilika zienee mpaka kwa madiwani na hatimaye wajumbe wa shina c kukomaa na ubunge tu. Ujumbe utawafikia wananchi tu hatimaye kuweka pembeni njaa za muda mfupi (za kuhongwa buku10 na ubwabwa) na kuchagua mabadiliko
 
Jana Mh. Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM pamoja na Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini walifanya kweli katika mji wa Manispaa ya Iringa.

Shughuli hii inafuatia kuwapo kwa Uchaguzi mdogo katika kata tatu za Kitanzini, Gangilonga na Kihesa zilizopo hapa mjini.

Katika Mkutano ule Mbowe alinukuliwa akisema kuwa Kinachotea sasa SI MPANGO MZIMA TU BALI NI MPANGO WA MUNGU, Kwamba kumekuwepo njama za kutaka kukatisha harakati za Kupigania Mabadiliko zifanywazo na Chadema lakini kwa Kudra za Mwenyezi Mungu Harakati zinasonga mbele.

Mbowe pia alitumia nafasi hiyo kuwataka wanachama wa chama cha mapinduzi wawaunge mkono chadema kwani ndicho chama haswa chenye nia thabiti ya kutaka kuleta mabadiliko kwa maendeleo ya watanzania, Mwenyekiti Mbowe alimalizia kwa Kuwaombea Kura madiwani wake.

Mh. Sugu kama kawaida alifunga mkutano kwa Mistari na kusisitiza kuwa Chadema ni dume la mbegu kweli na kuahidi kudhihirisha hili katika shughuri ya Igunga coz kwa mpango wa chama Muziki rasmi utaanza trh 25 Sept 2011 timu ya Makamanda itakapo wasili rasmi kwa Kazi!

umetujuza thx
 
Mbona kuna mtu humu jamvini huwa anasema eti Sugu alipata division four mtihani wa form four sasa hii thread ina ukweli gani?
Ngereja alipata division one kwani ametusaidia nini? Kufaulu darasani pekee sio kipimo cha uadilifu na utendaji. Unaweza kutueleza Hayati mzee kawawa alikuwa na elimu gani? Aren't we we proud of him? Unajua Ludovic alivyofaulu kwa alama za juu na unaweza kuusemeaje ufaulu wake leo? Bila kumsahau Luhanjo those people walifaulu vizuri sana what have they done for us? Think deep bro
 
Mbona kuna mtu humu jamvini huwa anasema eti Sugu alipata division four mtihani wa form four sasa hii thread ina ukweli gani?

sasa si angalau ya sugu hata iyo form four kaigusa vipi kuhusu lameck airo mbunge wa rorya na livingstone lusinde wanaotetea vyeo vyao kwa kushikwa masaburi na magamba.
 
Mbona kuna mtu humu jamvini huwa anasema eti Sugu alipata division four mtihani wa form four sasa hii thread ina ukweli gani?
Na prof.maji marefu nasikia aligonga div. 1, ole sendeka akataga la mbuni! Kuna ukweli gani hapo wajameni?, Ova!
 
Mbona kuna mtu humu jamvini huwa anasema eti Sugu alipata division four mtihani wa form four sasa hii thread ina ukweli gani?
Huyo mtu ni Mwita25 ambaye ndiyo philanderer mwenyewe.Thread yoyote ya sugu huyu mtu lazima aweke chuki zake binafsi dhidi ya Sugu!Huwa hana hoja za kupingana na sugu zaidi ya kuleta historia yake ya elimu na jinsi alivyokwenda majuu.Hajui kwamba hiyo ni historia ambayo hata Obama anayo ya kwake lakini la muhimu ni jinsi gani kiongozi anadeliver kwa anaowaongoza baada ya kuwa kiongozi.Watu wote wamtaa huu wanajua kuwa wewe ni mwita25 na bado kuna ID zako zingine nitakwambia siku nyingine.
 
Mbona kuna mtu humu jamvini huwa anasema eti Sugu alipata division four mtihani wa form four sasa hii thread ina ukweli gani?

Mimi nina amini sana elimu husadia katika mambo mengi pamoja na mafanikio na uwezo mkubwa wa kufikiri na kutoa maamuzi. Ila kuna Elimu ambayo ukiipata inaweza kukupa uwezo mkubwa wa kufikiri na utendaji. Sugu ana elimu kubwa sana ya kuweza kutosha kuwa mbunge mzuri na kiongozi mzuri tu. Ana onyesha ana utashi , ameishi sehemu mbali mbali duniani akifanya kazi na kujifunza mazingira. Ameona tawala za kidemokrasia na uchumi halisi akiwa mwananchi wa kawaida kwenye nchi nying. Ameishi na watu wa aina zote na kujua matatizo yao na mahitaji yao.

Tumekuwa na maprofesa na wenye Phd bungeni na kwenye tawala zetu ila wametuletea aibu tu. Angalia kina Chenge, Balali, Mbilinyi wote hawa na wengine wengi wana elimu za kutukaka ila hawana maadili wala utu na huruma kwa waliowatawala. Imefika wakati Elimu tusiione kwenye vyeti ila kwenye maisha ya kila siku na utendaji na matumizi yake. Elimu ni mkusanyiko wa vitabu unavyoelezea jinsi watu wengine walivyopambana na mazingira yao na kufanikiwa. Kwa hiyo nasi tunahitaji watu watakaoandikwa kwa matendo yao na uongozi wao. Wasomi wetu wengi wamekariri bila kujua elimu hubadilika na inahitaji uwezo wa pekee kuboresha maisha ya mazingira uliyopo.

Sugu aliweza mengi na anaweza mengi, ameonyesha anaweza kuwa mbunge mzuri na kufanya kazi na wana mbeya kuwaletea maendeleo ya kweli, hilo ndilo tunalotaka, Elimu bila karama ni bure.
 
Mbona kuna mtu humu jamvini huwa anasema eti Sugu alipata division four mtihani wa form four sasa hii thread ina ukweli gani?

Mbona kuna mtu humu alituambia kuwa Mbunge wa Njombe Jah People,Mbunge wa Korogwe vijijini Prof Maji Marefu,Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde na Mbunge wa Rorya Lameck Aiko wote kupitia CCM HAWANA FORMAL EDUCATION ikiwa na maana kuwa hawajasoma hata darasa la kwanza!

Ile thread ina ongea ukweli au inawachafua tu hawa wabunge mtz mwenzangu philanderer?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom