Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe na Halima Mdee wanavyomhujumu Tundu Lissu

kudamademede

Member
Jan 1, 2020
62
241
Kwanza kabisa tukubaliane kwamba mtanange wa uchaguzi umepamba moto huku kila chama cha siasa kikijitahidi kunadi wagombea wake na kushawishi wananchi kuwachagua.

Kwa namna nyingine tumeona vituko vingi vya wagombea wakiwa kwenye harakati za kutafuta kura majimboni na kwenye kata zao. Wakati mgombea wa uraisi kupitia CCM akiendelea kuchanja mbuga kusaka kura za wananchi, mgombea wa CHADEMA naye anazisaka kwa nguvu zote kura hizohizo katika upande mwingine wa nchi.

Je, nani alipiga picha ya Tundu Lissu akiwa ameachama (amepiga miayo) ambayo kwa jinsi wengi tulivyozoea hiyo huwa ni ishara aidha ya njaa, usingizi au uchovu? Ikumbukwe wazi kuwa wapiga picha wanaoambatana na mgombea ni wa chama husika na huweza kunasa matukio yote ya mgombea popote anapokuwa. Nimejithibitishia pasina shaka kuwa picha hiyo imepigwa na kusambazwa na mpiga picha maalum wa mgombea urais Tundu Lissu.

Nitarudi nyuma kidogo kuweka mtiririko sawa kutokana kile kilichotokea kwenye uzinduzi wa kampeni za ubunge Jimbo la Kawe zilizofanyika tarehe 29.08.2020 Tanganyika Packers, Kawe Dar es Salaam.

Siku ya uzinduzi wa kampeni kulikuwa na makabrasha yaliyojaa uzushi mwingi kuhusu mgombea ubunge wa jimbo la Kawe kupitia CCM, Askofu Josephat Gwajima yenye lengo la kumchafua na kuharibu taswira yake kwenye jamii. Makabrasha hayo ambayo yaliandaliwa na Absalom Kibanda pamoja na mwenzake ambaye hana hadhi ya kuongelewa wakiwa wamepewa kazi hiyo na Halima Mdee yaligonga mwamba jukwaani baada ya Tundu Lissu kukataa kabisa kuyasoma alipokaribishwa kuongea.

Mtu mmoja aliye karibu na Halima ambaye nalihifadhi jina lake kwa sasa alinitonya kuwa Halima alisikika akiongea na watu wake wa karibu kuwa amechukizwa na kitendo cha Lissu kutokumsaidia kumshambulia mshindani wake Askofu Gwajima anayegombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Kawe. Katika maongezi hayo Halima alimshutumu Lissu kuwa ana urafiki wa muda mrefu na Askofu Gwajima na sababu ya kutokumshambulia Askofu Gwajima ni kutokana na urafiki huo.

Katika maongezi hayo Halima alihoji iweje mgombea Urais ashindwe kumwongelea mgombea mbunge wa chama chake na kumwombea kura sambasamba na kuwaonyesha wapigakura kuwa mpinzani wake hafai hata baada ya kuwa ameandaliwa mambo ya kumponda mgombea wa chama pinzani. Halima alijiapiza kulipiza kisasi kwa kutopigania kura za Lissu katika jimbo la kawe akisema kila mtu abebe msalaba wake.

Mkutano huo wa Kawe ulikuwa na watu wachache sana waliojitokeza kushangaa kile kinachoendelea baada ya picha ya uzinduzi wa jana yake uwanja wa Zakhiem Mbagala kusambaa ikiwa na watu wachache sana mpaka kupelekea TBC kufukuzwa uwanjani.

Kwa upande mwingine taarifa zilizothibitishwa zinasema kuwa kumekuwepo na mvutano na kuhujumiana kati ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA na mgombea urais wa chama hicho Tundu Lissu. Mikutano mingi inayofanywa na Tundu Lissu imekuwa ya hali dhaifu yenye maandalizi duni mpaka kupelekea picha za uchaguzi wa 2015 ambao Lowasa aligombea kutumika kuhadaa umma kuwa mikusanyiko ni mikubwa kwenye mikutano yao.

Mvutano mkubwa uliopo kati ya Tundu Lissu na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe unatokana na majibu ya hovyo yanayotolewa na Mbowe pindi anapoombwa kutoa fedha kwa ajili ya kampeni ambazo ni makusanyo ya makato ya mishahara ya wabunge kwa kipindi cha miaka mitano. Hii ndio sababu kubwa ya miayo anayopiga Tundu Lissu huku mpiga picha wake akiwa tayari kusambaza picha hiyo ambayo inapeleka ujumbe unaosema UTAKULA JEURI YAKO.

Ni jambo lililo wazi kuwa kampeni za Tundu Lissu zinafanywa katika mazingira magumu sana ya kifedha na kupelekea kampeni hizo kukosa sura ya mgombea uraisi. Majukwaa anayotumia Tundu Lissu pamoja na PA system vyote ni hadhi ya chini sana kana kwamba anafanya kampeni za ubunge. Ukata wa fedha pia umedhihirishwa na tabia ya omba omba inayofanywa kwenye mikutano ya Tundu Lissu ambapo wananchi wanaohudhuria mikutano hiyo huombwa kuchangia fedha ili kusaidia gharama za kampeni kana kwamba chama kimeshituliwa na hakikuwa kimejiandaa kufanya kampeni za uchaguzi mkuu.

Ni jambo la fedheha kuwa Tundu Lissu katika hotuba zake akiwa kwenye majukwaa anasema wananchi ni masikini kwa sababu serikali ya Magufuli imeharibu uchumi lakini baada ya hapo anatembeza bakuli kuwaomba mchango wananchi hao anaowaita masikini.


Dr Alphonce Mwang'onda

alphoncejohn@gmail.com

IMG-20200924-WA0099.jpg
 
Let's face it; Dr!
Kupiga miayo au kuachama ni hulka ya binadamu timamu.

Kula mahindi hadharani tena bila kunawa ni uchafu na si hulka ya binadamu timamu.

Michango ya Lissu ipo very strategic... Nyie si mmekausha account zao na kuzuia misaada toka maeneo mbalimbali duniani..

Kuna busara inasema moyo wako upo hazina yako ilipo... Hao wananchi wanaweka hazina na mioyo yao kwa TL....Hawajali cha PA systems wala wingi wa wasanii.

Najua inawauma Sana wananchi wakijitoa kumchangia mtu wao... huku mtu wenu akiwafokea fokea ovyo.

Kama mlitegemea mtauangusha upinzani kwa mipango yenu miovu this time mambo ni tofauti sana.

Rekebisheni tofauti zenu ndani ya chama ndo mje mrekebishe madeni mnayodaiwa na wananchi...!

NB: Hiyo title ni PhD au ni dokta kama dokta...??
 
Nilitaka kushangaa kwanini hii picha imeingia mtaani kumbe ni hujuma? Alafu nashangaa kwanini mwenyekiti ndugu Freeman Mbowe hahudhulii mikutano ya Mgombea urais wa chama chake? Wana Chadema wenzangu Mgombea wetu anahujumiwa wazi wazi naona bado wanaleta ukanda kwasababu hajatokea njia za Arusha.

Halima mdee wewe Leo ndio wakumfanyia Mgombea wetu hujuma?? Kwenye kampeni zako sijakusikia ukimuuza Mgombea wetu sehemu yoyote unajinadi wewe tu naomba Wana Chadema tuamke
 
Nilitaka kushangaa kwanini hii picha imeingia mtaani kumbe ni hujuma? Alafu nashangaa kwanini mwenyekiti ndugu Freeman Mbowe hahudhulii mikutano ya Mgombea urais wa chama chake? Wana Chadema wenzangu Mgombea wetu anahujumiwa wazi wazi naona bado wanaleta ukanda kwasababu hajatokea njia za Arusha...
Nafahamu kuwa Mbowe anapambana jimboni na mhujumu anayetumia nguvu ya serikali ambaye no DC Sabaya. Ikatokea aondoke tu wiki moja atakuta hujuma za ajabu dhidi yake. Lazima abakie jimboni.

Nafahamu hali ni hiyo kwa Mdee, Msigwa, Lema, Sugu na wengine. Nafahamu pia Lissu ataenda Kilimanjaro na atafika Hai. Hayo mengine ni sumu anayojaribu kumwaga mleta uzi!
 
Nilitaka kushangaa kwanini hii picha imeingia mtaani kumbe ni hujuma? Alafu nashangaa kwanini mwenyekiti ndugu Freeman Mbowe hahudhulii mikutano ya Mgombea urais wa chama chake? Wana Chadema wenzangu Mgombea wetu anahujumiwa wazi wazi naona bado wanaleta ukanda kwasababu hajatokea njia za Arusha...
Yaani Hii in First Half CCM 3- CHADEMA -1
 
Nilitaka kushangaa kwanini hii picha imeingia mtaani kumbe ni hujuma? Alafu nashangaa kwanini mwenyekiti ndugu Freeman Mbowe hahudhulii mikutano ya Mgombea urais wa chama chake? Wana Chadema wenzangu Mgombea wetu anahujumiwa wazi wazi naona bado wanaleta ukanda kwasababu hajatokea njia za Arusha...
Lumumba mmefeli kwa propaganda hizi za kitoto
 
Nilitaka kushangaa kwanini hii picha imeingia mtaani kumbe ni hujuma? Alafu nashangaa kwanini mwenyekiti ndugu Freeman Mbowe hahudhulii mikutano ya Mgombea urais wa chama chake? Wana Chadema wenzangu Mgombea wetu anahujumiwa wazi wazi naona bado wanaleta ukanda kwasababu hajatokea njia za Arusha...
Propaganda hizi nyepesi sana
 
Uzi wa wana Lumumba kujitekenya halafu kucheka wenyewe. Kweli Lissu kawashika pabaya dadeki 😂😂😂
 
Propaganda hizi nyepesi sana
Wanajitekenya na kucheka wenyewe lumumba.

Wanaumia sana shujaa wa Mungu Tundu Antiphas Lissu anafanya kampeni na Team ya kampeni tu alafu amewakimbiza vibayaaaaa.
Wao kuanzia mwenyekiti, katibu, mwenezi , Makamu wenyeviti wote wako kwenye kampeni alafu bado wanapelekwa mputa hadi ulimi wote nje 😂😂😂😂😂

Lissu ni mwanasiasa na nusu dadeki 😂😀😀
 
Back
Top Bottom