Freeman Mbowe na Dkt. Vincent Mashinji, waalikwa Ghana kuapishwa kwa rais Mteule Nana Akufo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa Chama, Dkt. Vincent Mashinji ni miongoni wa wageni mashuhuri walioalikwa kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais Mteule wa Ghana, Nana Addo Dankwa Akufo-‐Addo na Makamu wake, Dk. Alhaji Mahamudu Bawumia, itakayofanyika Jumamosi, Januari 7, mwaka huu jijini Accra.

Viongozi wakuu hao ambao wameondoka nchini usiku wa Januari 6, kuelekea Accra, pia watahudhuria kuapishwa kwa Spika wa Bunge la Ghana, pamoja na Wabunge 275, waliopatikana baada ya Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Aidha, Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Mashinji wamepewa heshima ya kufanya mazungumzo na Rais Nana Akufo-‐Addo yatakayofanyika Jumapili ya Januari 8, baada ya kupata chakula cha mchana pamoja.

Kabla ya hapo, mapema asubuhi ya siku hiyo, viongozi wakuu wa CHADEMA watakuwa sehemu ya msafara utakaomsindikiza Rais Nana Akufo-‐Addo, kwenda kwenye ibada ya asubuhi, itakayofanyika eneo la Kyebi, kisha jioni msafara utarejea jijini Accra kuendelea na ratiba zingine.

Huu ni mwendelezo wa urafiki na uhusiano wa karibu kwa muda mrefu sasa, kati ya Chama cha Rais Nana Akufo-‐Addo cha New Patriotic Party (NPP) pamoja na CHADEMA, tangu vilipokutanishwa kwenye Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Duniani (IDU) na ule wa Afrika (DUA).

Viongozi wengine mashuhuri kutoka Afrika walioalikwa katika sherehe hizo ni pamoja na Kiongozi wa Chama cha Forum for Democtratic Change (FDC), Kizza Besigye, kutoka Uganda.

Imetolewa leo Ijumaa, Januari 6, 2017 na;
Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA
 
HongeraGhana. Ahsanteni kwa kuonesha demokrasia kwa vitendo. Nasikia hata Dr cheni kaalikwa pia
 
Inapendeza kwa kuwatia moyo na matumaini ya siku moja upinzani wa Tanzania kuiongoza inchi.
Japokua wengine wanafikili wana hatimiliki ya inchi hii.
 
Viongozi wa Serikali ya Tanzania hawajaalikwa?Tuna mahusiano mazuri na Ghana tangu Enzi za Kambarage.Anyway,kuna rafiki zangu wa Ghana wanampa big up sana Rais wetu wa JMT.Juzi walikuwa wananiuliza kwenye WhatsApp kwa kushangaa eti "tumesikia Rais wenu anataka kujenga viwanda 1000?"
 
Hii kwa wazee wa Lumumba haijakaa sawa hata kidogo! Historia nzuri na mwanzo mzuri Demokrasia kuanza kushamiri kwa Nchi kama Ghana -Nchi ya kuigwa toka wakati wa kudai Uhuru.
Lumumba imeamua kuzika kabisa Ndoto ya JKR.
 
Ujinga tu...matumizi mabaya ya Ruzuku

Wanashindwa ku focus kwenye mambo ya msingi na wanataka washinde uchaguzi
Wanashindwa kujenga chama wanaharibu pesa kwa safari.Ujinga mtupu huo.
 
Angalau wenzetu wanatuonesha upande wa pili wa sarafu katika medani za siasa sio watu kama Yahya Abdul-Aziz Jemus Junkung Jamme na watu KAMA CCM
 
Hii kwa wazee wa Lumumba haijakaa sawa hata kidogo! Historia nzuri na mwanzo mzuri Demokrasia kuanza kushamiri kwa Nchi kama Ghana -Nchi ya kuigwa toka wakati wa kudai Uhuru.
Lumumba imeamua kuzika kabisa Ndoto ya JKR.
Wazee wa Lumumba hawana time na vitu vidogo vidogo
 
Sijawahi kusikia chausta, UDP, tlp, na vingine vya aina hiyo vimealikwa nje ya nchi
 
Back
Top Bottom