Freeman Mbowe: Mwasisi wa harakati za vijana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Freeman Mbowe: Mwasisi wa harakati za vijana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kigugumizi, Nov 13, 2009.

 1. k

  kigugumizi Member

  #1
  Nov 13, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  FREEMAN MBOWE MWASISI WA HARAKATI ZA VIJANA.

  Akiwa amezaliwa kwenye Familia ya Kitajiri, tarehe 9 Disemba 1961, alipewa jina la Freeman "Mtu Huru". Baba yake alikuwa mfadhili mkubwa wa harakati za Uhuru, akiwa na Sykes, Rupia na wengine wengi.

  Akiwa ni kijana mdogo kabisa, alijiunga na CHADEMA kama mwasisi kijana akiwa ni Mwenyekiti wa kwanza wa Vijana wa CHADEMA. Licha ya utajiri mkubwa, hakuweza kujilisha kwa anasa kitambo za CCM, wala kuendeleza Ufisadi wa CCM alijiunga katika harakati za wapenda haki (Mageuzi).

  Baada ya kulelewa vyema kisiasa na Edwin Mtei, na Bob Makani na wengine, alipendekezwa kugombea Uenyekiti wa CHADEMA 2004, ambapo alishindwa.

  Mwaka 2005 akitumia ubunifu wa hali ya juu kwa kampeni za kisayansi, na gharama nafuu, CHADEMA ilionekana Chama mbadala chenye haiba nzuri kwa vijana wote wa Tanzania.

  Akiwa na Imani kubwa kwa Vijana, alianza harakati za kuwalea vijana, akiwemo Zitto Kabwe, John Mnyika, Mwakagenda, John Mrema, na wengine huku akiwaandaa kuja kushika Chama na Nyadhifa za Kiungozi Serikali.

  Leo vuguvugu lote la Vijana, ni matokeo ya Freeman Mbowe. Ukimwona Zitto anaongea elewa kuwa amelelewa na kufundishwa siasa na Freeman Mbowe.

  Mbowe siyo mchu wa madaraka kama Lipumba na Mrema, tayari amedeclare rasmi kugombea Ubunge Jimbo la Hai mwaka 2010 akitaka kuwapisha wengine wagombee.

  Mbowe angetaka kuwa Fisadi angejiunga CCM toka zamani sana! Angekuwa msaliti angejiunga CCM toka akiwa mdogo! Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!!

  Ni Charismatic leader!! Mwenye mvuto mkubwa sana! Asiyechoka kusikilizwa pindi aongeapo!! Uongozi wake makini wenye dira ndipo ilipoifikisha CHADEMA kuwa Chama mbadala na tumaini Jipya la watanzania!

  Alipokuwa Mbunge wa Hai 2000 - 2005 aliwahi kusema kuwa Bunge la Tanzania ni Rubber stamp ya Serikali, akalazimika kuacha kuingia Bungeni kwa muda kitambo kwa kuchoshwa na kura za ndiyo Mzee za Wabunge wengi wa CCM.

  Ana siasa za zaidi ya Vyama!! Wakati baadhi vyombo vya habari vya Mafisadi vikimtuhumu kumuua Chacha Wangwe, Mbunge wa Tarime! Ndiye Kiongozi wa Kwanza kuweka historia ya mapokezi ya Kifalme katika Wilaya ya Tarime!! Ni Rais wa Tarime! Alimshinda Kikwete Tarime kwenye Kura za Urais!!
   
 2. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mbona yote hayo tunayajua na mengine zaidi?. Sasa hii ni mada ya kujadiliwa au ni Information only?
   
 3. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mijitu mingine bana inakera kweli,mbowe hana hata sifa moja ya hizo ulizozitaja endelea kuwadanganya wanajamvi maana najuwa mko wengi sana jamvini.

  Kuhusu kugombea jimbo la Hai hiyo nayo ni sifa au amebaini Urais maji yako shingoni.Mbona hata Mzee wa Kiraracha naye keshatangaza atawania ubunge.

  Tuambie shule ya Mbowe imeishia wapi nasikia alikuwa anachukua Degree mbili kwa wakati mmoja ?.

  Mbowe hana historia ya maana katika siasa za Tanzania sana sana kuzusha Chopper angani.
   
 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Umesema ukweli wote hapa sina cha kuongeza wakuu
   
 5. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  sasa mbona kuhusus ELIMU yake hatuambiwi ?
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  I cant wait kuona wangapi watatoa "THANKS" kwa hii post
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Nov 13, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  Kigugumizi unaamini upinzani as whole, au wapinzani individuals? unaamini chadema kama chama au mmoja mmoja katika chadema? maana kama unaamini individual unawabeba baadhi ya wapinzani , huku ukiwaponda wengine, ndani ya chama kimoja, then we may have big problem here!

  Kigugumizi, kuhusu wangwe una hakika?
   
 8. B

  Boca1 Member

  #8
  Nov 13, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama kufahamu elimu yake kutatusaidia. Chakujiuliza nikwamba can he deliver good end results
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Nov 13, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Duh! kumbe Tz kuna maprez wa majimbo! Utumbo mtupu!
   
 10. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #10
  Nov 13, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo kwa CHADEMA elimu si muhimu sio?
   
 11. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #11
  Nov 13, 2009
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Inawezekana tukapeana taarifa na kuelimishana kwa pamoja kuhusu ujenzi wa chedema hiyo ni dhahiri labda tuambiwe kuhusu kumalizia hiyozo degree
   
 12. M

  MahinaVeterani JF-Expert Member

  #12
  Apr 1, 2014
  Joined: Aug 8, 2013
  Messages: 714
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mkuu bado una-wait kuona wangapi watatoa "THANKS" kwa hiyo post? Leo ni miaka kadhaa kadhaa THANKS kwahiyo post = 0. The bottom line is you may have to wait for a lifetime because the post was full of "pumba"!
  :biggrin:
   
 13. b

  bujash JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2014
  Joined: Aug 9, 2013
  Messages: 3,473
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mbona huna jipya zaidi ya povu tuu! unadhani elimu ndiyo busara??? hao wasomi wako magamba wamelifanyia nini taifa zaidi ya wizi wa raslimali zetu kupitia mikataba ya kimangungo????? kapuya ana nn zaidi ya ubakaji?? maccm yote hata yake masomi,akili zipo maka.lioni!
   
 14. b

  bujash JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2014
  Joined: Aug 9, 2013
  Messages: 3,473
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wewe una elimu gani? imetusaidia nini??? Karume aliye muasisi wa Zenji alikuwa na elimu gani??? na kwa nini tunamkumbuka???
   
 15. MUSSA ALLAN

  MUSSA ALLAN JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2014
  Joined: Oct 13, 2013
  Messages: 18,964
  Likes Received: 7,718
  Trophy Points: 280
  Mbowe hana upeo wa kuona mbali, ndio huyu huyu amechangia asilimia kubwa kuimaliza CHADEMA.
   
 16. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2014
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 44,523
  Likes Received: 25,349
  Trophy Points: 280
  wewe mburula chadema itakutoa kibyongo safari hii , wewe wa kumfahamu TAJIRI MBOWE ? ANAPOKUWEPO , FUKARA KAMA WEWE HURUHUSIWI KUWAPO , UMEMJULIA WAPI , UNAPIGA FIKSI KWA MANUFAA YA NANI ?
   
 17. M

  Man tindwa JF-Expert Member

  #17
  Apr 1, 2014
  Joined: Aug 3, 2013
  Messages: 305
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu sina uhakika kama mbowe amemlea zito nazan zito alianza kujulikana kabla ya mbowe na ndo aliyewapa passion vijana weng wa.tz kupenda siasa
   
 18. Kibo10

  Kibo10 JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2014
  Joined: Aug 20, 2013
  Messages: 11,243
  Likes Received: 3,395
  Trophy Points: 280
  Umeeleweka mkuu!
   
 19. Kibo10

  Kibo10 JF-Expert Member

  #19
  Apr 1, 2014
  Joined: Aug 20, 2013
  Messages: 11,243
  Likes Received: 3,395
  Trophy Points: 280
  Wewe ni zuzu toka humu kwenye siasa unafanya nini na uzuzu uliyonao.
   
 20. majaar

  majaar JF-Expert Member

  #20
  Apr 1, 2014
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 1,357
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Baba yako ndio mwenye historia ya maana Tanzania.
   
Loading...