Inevitable

Member
Apr 27, 2012
82
159
Wakuu,

Muda huu M/Kiti wa CHADEMA na viongozi waandamizi 9 wa chama hicho wapo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Tutarajie jambo gani jipya? Ndo ukurasa mpya wa Siasa za Tanzania?

UPDATE:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha majadiliano pamoja na Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Mei, 2022.

Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA waliohudhuria Kikao hicho ni Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Saidi Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya Chama hicho.

ikulu_mawasiliano-20220520-0002.jpg
FB_IMG_1653070823516.jpg

IMG-20220520-WA0014.jpg
IMG-20220520-WA0012.jpg
IMG-20220520-WA0006.jpg

75536C30-5825-4AF6-8512-8D6A7132481F.jpeg

To open up a new chapter as a nation haijawahi kuwa dhambi...

Hili kama ni kweli bac ni jambo jema kwa kila mwenye pumzi..

Narudia tena Political reconciliation ndiyo njia pekee ya kujenga taifa imara lenye umoja na nguvu kiuchumi kisiasa na kiutamaduni.

Nchi haiwezi kujengwa na mawazo ya upande mmoja.
 
Tangu Mbowe aanze kwenda huko hakuna hata jambo moja lililowahi kufanyiwa kazi na serikali, sijui ugumu wa Samia kufanya hivyo unatoka wapi, na sijui uvumilivu wa Mbowe utaendelea mpaka lini, naona utani unazidi.

- Lissu bado hajarudi nchini, hii inawezekana bado hajahakikishiwa usalama wake.

- Mikutano ya vyama vya siasa bado haijaruhusiwa japo ni takwa la kisheria.

- Wale wahujumu uchumi 19 bado wanakumbatiwa na Spika kule bungeni kinyume cha sheria.
 
To open up a new chapter as a nation haijawahi kuwa dhambi...

Hili kama ni kweli bac ni jambo jema kwa kila mwenye pumzi..

Narudia tena Political reconciliation ndiyo njia pekee ya kujenga taifa imara kiuchumi kisiasa na kiutamaduni.

Nchi haiwezi kujengwa na mawazo ya upande mmoja.
It is only chadema who can see this, wengine ni Rubbish minds
 
Ngoja kwanza tusikie kuhusu Katiba Mpya
Katiba mpya itoke wapi? We endelea kufanywa mpira wa dana dana huku mwenyekiti na genge lake wakiendelea kuupiga mwingi kupitia mialiko ya raisi. Mmeshaambiwa siku zote hakuna mkate mgumu mbele ya chai. Jamaa anatengeneza pesa ndefu kupitia siasa uchwara, huku akiwaacha watu wenye misimamo thabiti na chama wakiendelea kutokwa mapovu huko belgium na canada. Endelea na kazi ya kuwarubuni wana mbeya ili itapokuwa inaanzishwa michango ya chama wawe mstari wa mbele kukichangia.
 
Tangu Mbowe aanze kwenda huko hakuna hata jambo moja lililowahi kufanyiwa kazi na serikali, sijui ugumu wa Samia kufanya hivyo unatoka wapi, na sijui uvumilivu wa Mbowe utaendelea mpaka lini, naona utani unazidi.

- Lissu bado hajarudi nchini, hii inawezekana bado hajahakikishiwa usalama wake.

- Mikutano ya vyama vya siasa bado haijaruhusiwa japo ni takwa la kisheria.

- Wale wahujumu uchumi 19 bado wanakumbatiwa na Spika kule bungeni kinyume cha sheria.
Official talk on all these Ni leo! Hakujawahi kuwa na mazungumzo ya delagation
 
Back
Top Bottom