Freeman Mbowe lazima afungwe ili Uhuru wa kweli upatikane

Huu sio wakati wa kumlilia Mbowe Wala sio wakati wa kuwalaani ccm. Ili Uhuru wa bandia wa akina Kingai na Mahita wa kuteka, kutesa na kuua raia wema Kama akina Moses Lijenje na wengineo uondoke ni lazima Mbowe afungwe na sio Mbowe tuu na wale wote wazalendo wa kweli wapite katika tanuru la Moto Kama alivyo pita Tundu Lissu na wabakie kuwa waaminifu hata kufa.

Ccm hawaleti Mateso hayo kwa hiari yao bali wanalazimishwa na wakati uliopo. Hiki ndicho kipindi Cha mwisho kwao kutupa kete ya mwisho ya kupigania uhai wa matumbo yao. Wamejaribu kete ya vitisho ikabumba, wakajaribu kete ya bunduki ikabumba Sasa kete yao ya mwisho ni kufunga wapinzani. Kama ulisoma kile kitabu cha profesa Rostow akielezea hatua zinazotakiwa kufuatwa kufikia maendeleo ya kweli,hatua ya kisiasa tuliyopo Sasa Tanganyika ni ile hatua ya nne kabla ya mwisho akiita "Drive to Maturity.

Mbowe akifungwa ni faida kwa nchi na ni hasara kwa CCM. Watu wakifumbuliwa macho kuwa hawapo huru kiuchumi, kisiasa kijamii na kiutawala huwa raia wazuri Sana. Hii ni fursa kubwa kwa Chadema sasa kutumia jukwaa la kisiasa la ndani ya nchi hii na kimataifa.

Naiona Chadema inaenda kuwa Chama kikubwa na kinacho kubalika zaidi kitaifa na kimataifa kwa sifa ya kujali utu demokrasia na haki za Binadamu. Hata maandiko yanasema mkipigwa kwa ajili haki shangilieni kwakuwa thawabu yenu ni kubwa na imeandikwa mbinguni.

Huu ndio wakati wa kutenganisha maji na mafuta. Wakati wa kujua vyama halisi vya siasa vya upinzani na na vile vyama vya upinzani vikiwa ni CCMB. Ni wakati wa kujua mashirika halisi ya kutetea Haki za Binadamu na Yale ya kutetea matumbo yao. Ni wakati wa kujua viongozi halisi wa Dini ya Mungu wa kweli na viongozi wa Dini halisi wa shetani.

Kule Msumbiji na Afrika kusini sifa moja wapo ya mgombea urais inayo muongezea Imani kwa wapiga kura ni kuwa alishiriki kikamailifu ktk vita vya ukombozi wa nchi hiyo akiwa vitani ndani ya nchi hiyo au wakiwa nje ya nchi. Fuatilia viongozi wote wa Msumbiji na Afrika kusini utagundua walikuwa sehemu ya mapambano dhidi ya Uhuru wa kilaghai wa akina Kingai na Mahita nchini mwao. Hii taenda kutokea hata Tanzania. Chadema inaenda kushika dola na kumuondoa mkoloni mweusi CCM.

Makaburu hawakumfunga Mandela kwa hiari yao. Hoja zake zilikuwa hazijibiki hata ukitumia bunduki au Mateso, kuteka na kupoteza watu. Waliona kete yao ya mwisho ni tumfunge tu gerezani. Dunia ikapiga kelele wakati huo tukiwa shule ya msingi tukawa tunaimba nyimbo za kushinikiza Mandela aachiwe huru tukiwa tunakimbia mchaka mchaka.

Japo Mandela tulikuwa hatumjui lakini uzalendo wake kwa nchi yake ilitufanya tumuimbe. Hilo ndilo taifa ambalo Nyerere alijaribu kulijenga linalo jali utu wa watu wengine. Mandela mpya anaenda kuzaliwa Tanganyika na Dunia itampigania tukishirikiana na wazalendo wa nchi hii na kila aina ya silaha nawahakikishia itatumika kumlenga adui CCM.

Hii teua teua ya viongozi kutoka Chadema mnayo iona sio bure, ni uhalisia wa Mambo kuwa Chadema inakubalika na wananchi wote hata ndani ya CCM wenyewe. Huko Mbele tunako enda CCM itakuwa imekufa rasmi itakuwa ni vigumu mtu kuwa kiongozi Kama hakuwa mwana Chadema au hakuwa sehemu ya mapambano ya kudai Uhuru toka kwa mkoloni mweusi CCM.
Maendeleo hayana Chama.
Tupo kwenye kipindi cha udhalimu lakini utapita tu.
 
Kiroho statement yako ipo sahihi ila kimwili inagoma, Mbowe ana maisha pia at his @60. Hakuna njia nyingine ya kulikomboa Taifa kutoka hawa wakandamizaji zaidi ya hii.
Hapo umetumia falsafa kuona ktk maumivu anayopitia Mbowe Kuna mwanga Mbele unakuja,huwezi kuona hayo kwa akilili za Kingai ngai tuu.
NOTE: Kingai ngai=ujinga
 
Kufungwa kwa Mbowe kumeshapangwa, lakini hali hii litaleta mabadiliko makubwa ndani ya Chadema. Naiona Chadema ikiangukia kwenye mikono ya vijana wenye msimamo tofauti na wasiokuwa na subira kama Mbowe. Ole wa amani ya nchi yetu maana wosia wa Nyerere kuwa Tanzania tusijione kisiwa umepuuzwa na wenye hati miliki ya taifa hili.
 
Kufungwa kwa Mbowe kumeshapangwa, lakini hali hii litaleta mabadiliko makubwa ndani ya Chadema. Naiona Chadema ikiangukia kwenye mikono ya vijana wenye msimamo tofauti na wasiokuwa na subira kama Mbowe. Ole wa amani ya nchi yetu maana wosia wa Nyerere kuwa Tanzania tusijione kisiwa umepuuzwa na wenye hati miliki ya taifa hili.
Wakati ni mwalimu mzuri, hata wale Makaburu wa Afrika kusini au Wareno kule Msumbiji hawakuwaza kuwa Tanzania itakuwa kituo Cha kunoa wapigania uhuru.
Nakuhakishia kikinuka CCM haifui dafu hata wiki moja tuu ya mapambano. Wapo watu ndani ya mfumo huu dharimu wanatafuta wapi kwa kutokea ili inchi ipumue.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom