BAVICHA Taifa
Senior Member
- Jul 25, 2013
- 117
- 661
BARAZA la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) limeandaa kongamano kubwa la vijana tarehe 09/12/2013 Jumatatu jijini Dar es salaam kwenye ukumbi wa Landmark mahususi kwa maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanzania
Mgeni rasmi wa kongamano hili litakaloanza saa tatu asubuhi atakuwa FREEMAN AIKAEL MBOWE (MB) Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Kiongozi wa Kambi ya upinzania bungeni.
Mh Mbowe atatumia fursa hii kuzungumza na vijana wa Tanzania ya mustakabali wao ndani ya Taifa na ataambatana na wageni wazungumzaji ambao ni Tundu Antipas Lisu (MB) mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika (MB), Mabere Marando Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na gwiji la sheria nchini, Halima James Mdee (MB) na Dr KAmilius Kasala guru la masuala ya uchumi nchini.
Vijana na wanachni kwa ujumla mnakaribishwa kwenye shughuli hii ambayo itakuwa ni mbadala wa mizinga ya uwanja wa taifa siku hiyo kwa kuitafakari zaidi Tanzania yetu.