Freeman Mbowe: Kupona kwa Mhe. Lissu ni Mpango wa Mungu, Watanzania tuendele Kumuombea

10 M kwa siku ni za kutengenez mtu mpya maabara si hospitali. Na Mbowe hataondoka huko pengine asikie ruzuku imetoka tena, aje achukuwe.

Endelea kumchangia watanzania wezangu.

Hongera sana Mkuu nilitegemea uwe Arusha ambako wanadanganya ati Barabara zimejengwa na CCM,CCM inavitega uchumi vingapi na vipi vya kuiwezesha kujenga barabara??Mwambieni Mwenyekiti asiwe MUONGO kwa kiasi hicho,barabara zetu zimejengwa kwa kodi zetu.

Msalimie mamsap yako
 
Wengi wanatamani kuchangia ila mtihani ni namna hela inavyo kusanywa katika majanga kama haya tungependa viongozi wetu wafungue ankaunti maalumu kwa ajili ya kupokea mchango na kuwe na watu maluum wa kwenda kuchukua ili wachangiaji wajue ile pesa imelenga kuuguza sio tunachangia kwenye mifuko ya watu au chama maana pesa zinazo ingia ankaunt ya chama lazima ziwe zinahusu shughuli za chama
 
Matibabu gani hayo yanachukua zaidi ya 500M sijawahi kuona ,hii ni zaidi ya Deci na kikombe cha Babu

Hata marekani hakuna gharama hizo

Sawa tunamuombea ila kuna harufu ya kuliwa kwa hela zetu za rambirambi
hata ikitumika bil1 tutatoa tu we kaa ivyo ivyo ukifikiri lissu anaumwa maralia na yupo dispensary
 
Kipindi cha utawala wa awamu 5 ndicho kipindi mtu Kama Lissu na Mbowe wanahitajika zaidi kuliko katika tawala zote zilizopita na watu wengine walio na msimamo thabiti unaofanana Kama msimamo Wao.
 
Matibabu gani hayo yanachukua zaidi ya 500M sijawahi kuona ,hii ni zaidi ya Deci na kikombe cha Babu

Hata marekani hakuna gharama hizo

Sawa tunamuombea ila kuna harufu ya kuliwa kwa hela zetu za rambirambi
Si kosa lako, akili zako ndipo zilipoishia
 
Hichi chama cha wanasheria
Kina mapesa mengi kwanini wasimtibu raisi wao wanaachia upande mmoja
 
Ugua pole TL.
Mbowe inabidi afahamu kitu kimoja,kama mabalozi wenyewe wakienda ikulu wanakunywa juisi na pipi,maana yake huko wapinzani hamna tena zile zama za kwenda kunywa maziwa na cocoa ikulu ,hela zote zinaenda kwenye miradi.
Hela zote zinaenda kulipa madeni ya kujitakia kavunja mikataba ovyo
 
Wameiweka hii milioni 10 sababu kuna operations zinazoenelea kila wakati wanapoona sasa operation hii inastahili au muda wake umefika.Kuna operations nyingine ni ghali zaidi,na hapo inaendana na vipimo vyake vinavyochukuliwa kila siku au baada ya siku kadhaa.

Ukitaka kujua gharama ya private hospital kubwa na yenye ufanisi jaribu kumpeleka mgonjwa wako hapo Aghakhan,usipoangalia vipomo peke yake inaweza kukugharimu milion sita na ushee.Tuwe wavumilivu.Afya ya Lissu kwanza
nilikuwa namjibu huyo anae uliza gharama kwanini zifike 500M ''What we want is for him to recover well, others are busy here trying to know about expenses. They have not even contributed a single sent''
 
Nimeiona.Unajua wengine wako kwa ajili ya kuhakikisha Lissu hapati michango ya kutosha na mawazo yao makubwa kuishi kwake kwao ni adhabu.

Hivyo wenye moyo wa kuchanga tutaendelea kuchanga
 
Magu anataka tatizo la umeme liwe historia baaada ya miaka 3,yaani umeme ukikatika unawapeleka tanesco kortini
Wazabuni 66 wajitokeza mradi wa umeme wa Stiegler’s Gorge — Ministry of Energy and Minerals
Zitto aliongea sana kuhusu hii makitu.

Ujue gharama za kuleta gas dar kutoka msimbati imetugharimu sana?
Unajua tumeambiwa ni swala la kuzalisha umeme ndio ilikuwa sababu kuu?
Unajua tuliambiwa kukatika umemw itakuwa historia?

Hatushangai mtoto akitembea bali tunashangaa mtoto akishindwa kutembea!
 
Wengi wanatamani kuchangia ila mtihani ni namna hela inavyo kusanywa katika majanga kama haya tungependa viongozi wetu wafungue ankaunti maalumu kwa ajili ya kupokea mchango na kuwe na watu maluum wa kwenda kuchukua ili wachangiaji wajue ile pesa imelenga kuuguza sio tunachangia kwenye mifuko ya watu au chama maana pesa zinazo ingia ankaunt ya chama lazima ziwe zinahusu shughuli za chama

Kuna siku utamuuliza Mungu ZAKA yangu inatumikaje kanisani.Kama unaweza kutoa mchango wa harusi na bado ukaambulia beer moja na Sahani ya wali bila mboga na huulizi,sembuse mgonjwa??

Ukishatoa unasahau kama umetoa utakuwa salama.Maana SADAKA uitowayo hakikisha hata mkono wako wa kuume hautambui umetoa kiasi gani.
 
Zitto aliongea sana kuhusu hii makitu.

Ujue gharama za kuleta gas dar kutoka msimbati imetugharimu sana?
Unajua tumeambiwa ni swala la kuzalisha umeme ndio ilikuwa sababu kuu?
Unajua tuliambiwa kukatika umemw itakuwa historia?

Hatushangai mtoto akitembea bali tunashangaa mtoto akishindwa kutembea!

Na akishindwa kutembea unampeleka kwa TABIBU ili atembee.
 
Kupona kwa Mhe. Lissu ni mpango wa Mungu, nawaomba Watanzania wenzetu waendelee kumuombea kwa Mungu pamoja na kuchangia gharama za matibabu, kwa kuwa gharama zake ni kubwa ambazo chama pekee hakiwezi kuzimudu bila ya misaada kutoka kwa watu mbalimbali.

Unajua ahueni humtokea mgonjwa taratibu taratibu na ndivyo inavyotokea kwa Lissu, ingawa sisi wote tuna hamu apone mara moja aje aendelee kupigania haki za wanyonge kama alivyokuwa akifanya.

Sisi tunatoa taarifa za maendeleo ya Lissu kulingana na Madaktari wanavyotuambia, hatuwezi kusema chochote nje ya wataalam hao, kwa kuwa ndio wenye ujuzi wa kumtibu na kujua maendeleo ya mgonjwa husika.

UOINZANI NI KAZI NGUMU

Kazi ya Upinzani ni ngumu, hasa katika zama za utawala wa awamu ya tano, ambae inaonekana hatambui na kuthamini mchango wa Wapinzani kama walivyokuwa watangulizi wake.

Licha ya vitisho na kila aina ya hujuma tunazofanyiwa kamwe hatuwezi kurejea nyuma, bali tutafanya kazi zetu kwa tahadhari kubwa kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo tulikuwa na Uhuru mkubwa wa kujieleza na Serikali kufanyia kazi mambo tunayosema.

Huwezi kuendesha nchi bila kuruhusu ukosoaji, iwe kutoka upinzani au kwenye chama unachokiongoza, unapowazuia watu wasipumue na kutoa madukuduku yao, unatenegeneza hasira kubwa ndani ya jamii.
 
Matibabu gani hayo yanachukua zaidi ya 500M sijawahi kuona ,hii ni zaidi ya Deci na kikombe cha Babu

Hata marekani hakuna gharama hizo

Sawa tunamuombea ila kuna harufu ya kuliwa kwa hela zetu za rambirambi
Unazungumzia marekani gani isiyo na matibabu ya ml 500?
 
UPINZANI NI KAZI NGUMU Kazi ya Upinzani ni ngumu, hasa katika zama za utawala wa awamu ya tano, ambae inaonekana hatambui na kuthamini mchango wa Wapinzani kama walivyokuwa watangulizi wake.

Licha ya vitisho na kila aina ya hujuma tunazofanyiwa kamwe hatuwezi kurejea nyuma, bali tutafanya kazi zetu kwa tahadhari kubwa kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo tulikuwa na Uhuru mkubwa wa kujieleza na Serikali kufanyia kazi mambo tunayosema.
Binafsi naamini Mkulu anachuki sana na upinzani pamoja na kujitangaza kila siku kuwa hajali chama!!

Pamoja na kina Slaa kugomea kumtambua 2010, mwisho wa siku JK aliwaita wapinzania na kukaa nao Ikulu!! Hii kitu haielekei kutokea kwenye awamu hii!!
 
Matibabu gani hayo yanachukua zaidi ya 500M sijawahi kuona ,hii ni zaidi ya Deci na kikombe cha Babu

Hata marekani hakuna gharama hizo

Sawa tunamuombea ila kuna harufu ya kuliwa kwa hela zetu za rambirambi

Hiyo rambirambi mlimchangia nani?! Acha mambo ya kipumbavu, yaan mlikua mnasubiri Lisu afe na hamna taarifa kuwa anapona!!! Hadi leo unawazo la rambirambi kwa mtu aliehau? Na kuna watu wamekupa like! Safura inakusumbua aisee, huwezi kusubiri kifo cha mwenzako kwa ham namna hivyo!
 
MUNGU AMTANGULIE LISSU NA MBOWE NA WENGINE WOTE WANAOPIGANIA HAKI ZA WATAZANIA

MUNGU NI MWEMA WAKATI WOTE ILA PIA MUWE NA TAHADHARI
 
Kama upo Dar nenda hapo Again Khan uulizie kupima tu saratan, kufanyiwa operation yoyote ile then urudi. Nahisi nalinganisha Mwananyamala Landa!!
10 M kwa siku ni za kutengenez mtu mpya maabara si hospitali. Na Mbowe hataondoka huko pengine asikie ruzuku imetoka tena, aje achukuwe.

Endelea kumchangia watanzania wezangu.
 
Back
Top Bottom