Freeman Mbowe kuongea na vyombo vya Habari Machi 18, 2022

View attachment 2154363

Hii ndio Taarifa ya sasa iliyosambazwa kote duniani .

Freeman Mbowe , ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa ataongea na vyombo vya habari kwenye ofisi za Makao Makuu ya Chama , Nje ya Jiji la Dar es Salaam Kinondoni , mtaa wa Ufipa , Tarehe 18/03/2022 kuanzia saa 5 asubuhi .

Kaa tayari kupewa taarifa za maamuzi mazito yaliyotolewa na Kikao cha Kamati Kuu kilichoketi hivi Karibuni .

Wote Mnakaribishwa .

Mungu ibariki Chadema
Chadema hamna mwenezi au katibu wa chama, kila kitu mnamuachia mwenyekiti
 
K
View attachment 2154363

Hii ndio Taarifa ya sasa iliyosambazwa kote duniani .

Freeman Mbowe , ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa ataongea na vyombo vya habari kwenye ofisi za Makao Makuu ya Chama , Nje ya Jiji la Dar es Salaam Kinondoni , mtaa wa Ufipa , Tarehe 18/03/2022 kuanzia saa 5 asubuhi .

Kaa tayari kupewa taarifa za maamuzi mazito yaliyotolewa na Kikao cha Kamati Kuu kilichoketi hivi Karibuni .

Wote Mnakaribishwa .

Mungu ibariki Chadema
kila la kheri tegemeo la watanzania ni Chadema tu
 
Hapo unamaanisha ulichokiandika au uliteleza?
Kwa mujibu wa Magufuli Jiji ni Ilala tu , yaani Chanika , Vingunguti , Buguruni kwa Mnyamani , Karakata na Pugu Kajiungeni ndio Jiji , Masaki , Mikocheni , Oysterbay , Kinondoni , Temeke ni nje ya jiji .

Sasa sina hakika wakati haya yanafanyika ulikuwa nchi hii au hukuwepo .
 
Hongera mkuu kwa namna unavyotupa taarifa za chama CDM kiukweli ni moja wa watu unawakilisha vema chadema Jf, unastahili pongezi,

Ila naomba nikushauri usipende kutumia neno maskini katika ukosoaji wako hasa kuwasilisha hoja za chama unachokitetea, utaleta mgawanyiko mkubwa, na kuvunja moyo wengi wanaofutilia habari za chama
Watanzania wengi ni maskini
Ndo wako kwenye harakati za kujikomboa na umaskini ili kufikia hatua za maisha bora.
Kama wewe umeshavuka hapo ni vema, ila usitengeneza vibaya taswira ya chama kwa watanzania wengi wanaondelea kujitoa kwenye umaskini
Nakushukuru kama utanielewa
Nimekuelewa sana na nakushukuru kwa kutambua mchango wangu wa habari za Chadema hapa jf , ila naomba ieleweke kwamba umasikini au unyonge si jambo la kujivunia , siyo sifa njema , ni lazima tupige vita na tukemee na kukataa umasikini kwa nguvu zote kabisa , japo kwenye hoja hizi za hapa jf kwa hawa wanaonitukana huwa namaanisha ni Masikini wa Fikra .
 
Hahaaha sawa mkuu ni ushauri mzuri umempa
 
Mbowe ana mvuto kuliko makamu wa rais mbowe ni rais mwenza na samia tofauti ni mdogo sana mbowe hajakabidhiwa dola.
Kwenye Mvuto naweza kukupinga. Labda useme wewe unapenda mtu calibre ya Mbowe.

TL ni ngao ya siasa na intelijensi
 
✋.....au basi....🤫
1647547424329.jpg
 
Nimekuelewa sana na nakushukuru kwa kutambua mchango wangu wa habari za Chadema hapa jf , ila naomba ieleweke kwamba umasikini au unyonge si jambo la kujivunia , siyo sifa njema , ni lazima tupige vita na tukemee na kukataa umasikini kwa nguvu zote kabisa , japo kwenye hoja hizi za hapa jf kwa hawa wanaonitukana huwa namaanisha ni Masikini wa Fikra .
Nashukuru kama umenielewa,

Ila nategemea kama chama ambacho tunafikiria kinaweza kuwa mbadala na makada wake wakubali kwanza kuna tatizo la umaskini

Pili waje na mipango na mikakati mbadala iliyo wazi kabisa ya namna kuondoa tatizo la umaskini,
Na ndicho watanzania wengi wanategemea,

Na siyo kukemee na kukutaa kwa maneno matupu tu !

Tuonyesheni njia mbadala ya kuvuka
kama unamanisha umaskini wa kifkra ,basi specify clearly

Ieleweke
 
Mbowe Mwamba Kama Mwamba tunakusubiri kwa shauku
Nahisi harufu ya taharuki.

Mbowe akicheza vibaya na Covid 19 kwa kuamua kuwafukuza basi anakipasua chama mapande 2!

Mbowe utakuwa salama ukicheza vizuri na Covid 19 kwa kubalance mambo vinginevyo utaharibikiwa.

Waitwe, waombe msamaha, wasamehewe, wapewe masharti na Chama, waendelee kupiga siasa za chama bungeni.

Utakuwa umeshinda, CHADEMA itakuwa imeshinda, Covid 19 watakuwa wameshinda na CHADEMA inabaki salama na kufanya siasa bila wasiwasi.

Mbowe, Mbowe, Mbowe nimekuita mara 3: cheza na busara unusuru chama.
 
Back
Top Bottom