Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe: Kuna mamilioni ya wapiga kura hewa na maelfu ya Vituo bandia

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Freeman Mbowe amedai kuna Uvurugwaji Mkubwa wa daftari la wapiga kura.

Ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba, kuna Mamilioni ya Wapiga kura hewa na Maelfu ya Vituo hewa.

"Kuna uvurugwaji wa kutisha wa Daftari la wapiga kura. Mamilioni ya wapiga kura hewa & maelfu ya vituo bandia. Wapiga kura wengi wapinzani wamehamishwa vituo au kuondolewa kwa makusudi. NEC itoe maelezo & suluhisho haraka la sivyo uchaguzi huu utashindikana kuanzia hatua ya awali." amesema Freeman Mbowe.

28 Oktoba 2020, Wananchi wa Tanzania watapiga kura ya kuchagua Rais, Madiwani na Wabunge.

IMG_20201023_123215_047.jpg
 
wewe mzee umechanganyikiwa nini!!!! Kipigo cha jana pale HAI si mchezo lazima unene kwa lugha
 
Mbowe rudi kuendelea na biashara. Mwisho wako umefika katika siasa usitafute sababu za kuhalalisha kushindwa kwako. Uwezo wako wa kiuongozi ni finyu sana ulikuwa unabwebwa na upepo wa kisulisuli ambao sasa hauko tena cdm.
 
Saccos ya Ufipa kwishney, utafanya watu wajinga mara kwa mara, lakini haitokuwa siku zote bila kukubaini utapeli wako.
 
Wekeni hayo majina mtandaoni ....tunajuana kama sio mtu wa kituo husika
 
Chadema mtajuta kusimamisha msaliti wa Nchi Lissu apeperushe bendera ya Chadema Akiwaletea Chadema hata wabunge wawili mkatambike.
Umeshashiba makande. Wahi wahi kunakucha. Angalie usikate mafuta lakini. Mwenzako huko anazikwa leo.😅😅😅
 
Kwa hili la wapiga kura hewa na vituo vya kupigia kura visivyo rasmi... Tume ya uchaguzi imeonyesha ulaghai na kushindwa kuwa huru...
 
You often do not prepare breakfast for your better half, you are all the time behind keyboard. When do you serve you siblings ? Wishing you a good day.


You desire removing a splint from someone eye while leaving an iron bar laying in your eye.
 
We Mbowe umechanganyikiwa kwa hiyo NEC wakiangalia tu katika madaftali ya wapiga kura wanajua huyu chadema tumuhamishe na huyu ccm tumuache

Laana ya Dk Slaa itawatafuna sana na bodo subirini tarehe 28
 
Kumbe sio lazima uvue nguo ili uitwe kichaa, kwa uchaguzi huu naona vichaa wamekuwa wengi mnoo. Upinzani kweli unataabika kwa kujiaminisha na ushindi ambao haupo. Poleni.
 
Back
Top Bottom