Freeman Mbowe kuitwa Mandela wa Tanzania ni sawa?

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,291
Kwanz kabisa napenda kuwasalimu kwa jina la alietuumba, ambae ni muweza wa visivyowezwa. Ama baada ya salam napenda nijielekeze katika mada yangu ili kila mwenye uwezo thabiti wa kuchangia aweze kuchangia.

Mada hii ni nzito na inawafaa zaidi wale ambao akili zao zipo huru, hazijafungwa wala kuhifadhiwa ndani ya mfuko wa mwanasiasa yoyote. Maana kuna watu ambao tayari wameshawakabidhi wanasiasa akili zao, kiasi kwamba hawawezi kuwa na wazo lolote kinyume na wale wanaomiliki akili hizo.

Twende sasa... Ndugu zangu kuna baadhi ya watu wamekuwa wakijaribu kumfananisha mwenyekiti wa Chadema taifa mh Mbowe na aliekuwa mpambanaji wa kweli na mpigania uhuru wa Afrika kusini hayati Nelson.

Ingawa kila mtu anaweza kuwa na mawazo au mtizamo wake lkn kwangu mimi naona kuwa watu hao wanakosea sana. Naweza kutaja baadhi ya sababu zinazofanya nikatae kukubaliana na watu hao.

Sababu hizo ni :

[1] Hayati Nelson alikuwa tayar kuwapambania wa South Africa wote bila kujali rangi zao, makabila yao, dini zao, vyama vyao na itikadi zao. Wakati mh Mbowe anaonekana kupambania zaidi masilahi yake, masilahi ya baadhi ya ndugu zake, watoto wake na tumbo lake.

[2] Hayati Nelson alihamasisha mapambano akiwa mstari wa mbele na familia yake. Mh Mbowe alikuwa na tabia ya kuhamasisha mapambano au maandamano, huku yeye na familia yake wakitimkia Afrika kusini au Dubai kula bata nk.

[3] Hayati Nelson alijitolea kila alichonacho kusaidia mapambano, ili wananchi wake wapate uhuru wao. Mh Mbowe akitoa hata sh1000 ujue siku ruzuku akiingia tu anakata hela yake kwa kisingizio cha kukidai au kukikopesha chama.

[4] Mwisho kabisa wakati mzee Nelson amefungwa jela takriban miaka 27, wananchi wake na wanaharakati mbali mbali wa ndani na nje ya nchi yake walionekana kuguswa, na kumpambania kwa njia mbali mbali. Bongo toka mh Mbowe afungwe ni week ya tatu tu sasa, lkn tayar ashaanza kusahaulika mapema sana utafikiri hakuna mwanasiasa anaeitwa mbowe nchini.

So hizo ndio sababu za mimi kupingana na watu hao wanaojaribu kufananisha nguvu za gari na treni. Haya ndugu zangu mwenye vigezo vya kumlinganisha mh mbowe na aliekuwa mzee wetu hayati Nelson anakaribushwa kuchangia na kuweka vigezo vyake hapa. Asanteni.
 
Kwani ndugu inakupunguzia nini katika maisha yako ya kila siku pale mbowe anapoitwa mandela wa Tanzania? Je kwani baada ya mbowe kuitwa mandela ndipo bei za vitu zilipopanda au kodi kwenye kila huduma zilianzishwa?
No mkuu tunajadili tu ili kujua kama sifa anazopewa zinamfaa au la.
 
Back
Top Bottom