Freeman Mbowe (KUB): Bajeti hii ya Serikali haitoi nafuu kwa mwananchi...

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
490
2,471
Akihojiwa na Kituo cha TBC baada ya kikao cha bunge jioni hii ambapo Serikali imewasilisha Taarifa yake ya Mwaka wa Fedha (bajeti kuu), Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe amesema bajeti ya mwaka 2014/2015 kwa ujumla wake, haitoi nafuu yoyote kwa mwananchi.

Amesema kuwa Serikali inapoamua kuongeza vyanzo vya kodi kwa lengo la kupanua wigo wa mapato, inategemea imegusa maeneo gani, kwa sababu vyanzo vingine vilivyoongezwa mwaka ujao wa fedha vitaendelea kuongeza mzigo kwa mwananchi.

Kuhusu kuondoa au kupunguza misamaha ya kodi, KUB Mbowe amesema ni matokeo ya hoja za Kambi ya Upinzani Bungeni ambayo imepigia kelele suala hilo kwa zaidi ya miaka 2 sasa, lakini siku zote Serikali ilikuwa haitaki kutekeleza.

Hata hivyo amesisitiza kuwa Serikali ilipaswa kusema kwa misamaha ambayo imeondolewa au kupunguzwa, kiasi gani cha fedha kitaokolewa na kitaelekezwa kwenye matumizi gani.

Amesema inashangaza kuona kwamba Serikali bado imeendelea kutegemea kodi kwenye pombe, mvinyo, sigara etc.

Kuhusu suala la kodi ya PAYE, amesema kuwa punguzo la kutoka asilimia 13 hadi 12 bado ni kiwango ambacho kitawaumiza wafanyakazi nchini, akisema kuwa kwa muda mrefu sasa, Kambi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikiitaka serikali kushusha hadi asilimia 9, jambo ambalo linawezekana.

Mjadala wa bajeti utaanza Jumatatu ijayo, ambapo Kambi ya Upinzani Bungeni itawasilisha bajeti mbadala pamoja na Taarifa ya Hali ya Uchumi na Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2014/2015.
 
Alichosema ni kweli kabisa wafanyakazi kwa kupunguziwa 1% kwa mbwembwe na majigambo kibaao sioni kama kweli Serikali imedhamilia kuinua naisha ya wafanyakazi.
 
Ndio maana kuna budget ya kambi rasmi ya upinzani.hayo yote anatakiwa awasilishe
 
Tusubirie bajeti kivuli kwanza, ila ubunifu bado tatizo sio kwa serikali tu hata KUB tungependa kuona wakati huu wanakuja kitofauti zaidi na kupendekeza njia mbadala za mapato pamoja na kuona kwa picha kubwa ni namna gani serikali inatenga pesa za maendeleo kwa watu wakati huu tofauti na utaratibu wa kawaida wa kuona maendeleo ni kujenga barabara na madaraja.

Maendeleo kwa watu namaanisha bajeti itenge pesa kwa shughuli za uzalishaji mali kwa vikundi vya vijana na wanawake vijijini na mijini ili kuwaweka watu wengi kazini wazalishe mali. Serikali wakati huu ione harakati zilizofanywa na NGOs katika kuendeleza watu na ibebe huo mzigo kwenye bajeti sasa na kupunguza ruzuku kwa vyama vya siasa na posho za vikao ili pesa nyingi iende kwenye uzalishaji mali.
 
Ndugu yangu siku zote sijajua ccm hasa walio katika jukwaa hili huwa wanachangia kwa kutumia nn na sijajua ni jinn la aina gani limewafunga. Kwasababu ya ukombozi wa watanzania sasa tumejipanga kutoa semina misikitin na makanisani ili waumini watambue na ccm waanze kujiandaa kisaikolojia kwa kweli
 
Mfanyakazi hana njia ya kukwepa kodi kamwe! Serikali ingepunguza kodi kwa wafanyakazi angalau ingefika asilimia 10! Pia kitendo cha serikali kuongeza kodi kwenye vinywaji baridi sio sawa!
 
tumeshamchoka huyu mbowe naye,kila kitu anataka mtaji wa siasa na wajinga lazima wam-support tu,nchi zilizoendelea watu wanahamasishwa na kuhamasika na zaidi wanatamani walipe kodi zaidi kwa maendeleo ya mataifa yao yeye kila siku porojo bila ya kuja na jibu na sio jibu tu,jibu litakalowezekana kulitoa kwenye nadharia na kulipeleka kwenye vitendo na likatekelezeka.na sio. kusema tu mfano deep sea,watu wasipokuja Kuvua je itakuwaje? au tutakuwa tunaendeshwa kwa kubahatisha? Mara nyingine awe +ve kama tunapenda kumchagua tutamchagua tu na kama hatutaki basi.
 
Msitegemee ccm kuwa na bajeti itakayowapunguzia ukali wamaisha wananchi...wao wanawaza dili tu za kunufaisha matumbo yao....tuwaondoe sasa kwa umoja wetu chama cha kishetani hiki
 
Mbowe angesema kwa kifupi tu yeye na Serikali yake wangefanya nini katika masuala hayo hayo ambayo CCM wameshindwa. He should've provided a clear and bold contrast between the failed policies of the ruling part and those of the opposition. Na kwanini Watanzania wanaolalamika na kuumizwa na matokeo ya bajeti hii wafikirie kwa uzito unaostahili kuwaingiza wao madarakani.
 
tumeshamchoka huyu mbowe naye,kila kitu anataka mtaji wa siasa na wajinga lazima wam-support tu,nchi zilizoendelea watu wanahamasishwa na kuhamasika na zaidi wanatamani walipe kodi zaidi kwa maendeleo ya mataifa yao yeye kila siku porojo bila ya kuja na jibu na sio jibu tu,jibu litakalowezekana kulitoa kwenye nadharia na kulipeleka kwenye vitendo na likatekelezeka.na sio. kusema tu mfano deep sea,watu wasipokuja Kuvua je itakuwaje? au tutakuwa tunaendeshwa kwa kubahatisha? Mara nyingine awe +ve kama tunapenda kumchagua tutamchagua tu na kama hatutaki basi.
mweuu...mweuu...
 
Mbowe angesema kwa kifupi tu yeye na Serikali yake wangefanya nini katika masuala hayo hayo ambayo CCM wameshindwa. He should've provided a clear and bold contrast between the failed policies of the ruling part and those of the opposition. Na kwanini Watanzania wanaolalamika na kuumizwa na matokeo ya bajeti hii wafikirie kwa uzito unaostahili kuwaingiza wao madarakani.
ya umenena
 
mweuu...mweuu...

haujielewi na usipobadilika utabaki hivyohivyo huku ukimsubiria mtu/chama fulani kikuletee maendeleo unayoyataka,utasubiri sana na utakuja kumbuka shuka imeshakuwa asubuhi.nikukumbushe kuwa kiongozi yeyote anayetaka nafasi ni kama sales person tu, he has to win sales/person by different techniques(avoiding objections).so mambo mengine unatakiwa ujiongeze mwenyewe kwa akili yako ya kawaida aliyokupa mwenyezi,na hiyo haimaanishi wewe uhame chadema ila usiwe kama mtu aliyerogwa na aliyekuroga akawa ameshakufa.
 
Back
Top Bottom