Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Freeman Mbowe, kada mtiifu wa CCM aliyepewa uenyekiti Chadema.
Igwe wana JF,
Japo wengi hawaelewi hadi siku yawatokee wao kuna haja ya kuweka kumbukumbu sawa. Wengi wanamjua Freeman Mbowe kama kiongozi wa CHADEMA na KUB ila kwa uhalisia wa mambo kuna kazi zaidi ya hiyo, Mbowe huyu ni zaidi ya wengi wamjuavyo.
Ni ngumu kung'amua haya kama uwezo wako kifikra ni wa kawaida au chini ya wastani lakini kwa watu walio timamu wanalijua hili. Mbowe aliyeshiriki uchaguzi mwaka 2005 aliushangaza umma wa watanzania pale alipohudhuria kuapishwa kwa JK huku akicheka kwa bashasha na kutoa vijembe kwa Lipumba ambaye hakuridhika na matokeo.
Mbowe huyu ni mwanachama wa makundi maarufu ndani ya CCM amabapo mara nyingi amekuwa akipigia chapuo baadhi ya wagombea anaowapenda. Mbowe, ni Team Lowassa, Team Membe.......nk anachokifanya ni kuchanga karata zake vema ili yeyote akitokea mambo yake yanakwenda sawa. Mbowe huyu huyu ndiye aliyemtabiria urais Magufuli huko Hai wakati akizindua barabara...alitamka hadharani anataka ''chuma'' mithili ya Magufuli.
Kwa sasa kazi yake kubwa ndani ya Chadema ni kukwepesha malengo ya Chadema, anahakikisha Chadema inapoteza ''focus''. Hapa pia ni wachache walio timamu wataelewa. Ukada wa Mbowe ni hakika. Kwa sasa ni dhahiri Chadema imegeuzwa tawi la CCM.