Freeman Mbowe: CHADEMA kufanya Mikutano Nchi nzima kuanzia Mwezi wa nne. Bado tunahitaji kujua waliomuua Aquilina

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Mkutano wa Mwenyekiti wa CHADEMA NA WAANDISHI, Machi 16,2020.


====
Updates
FB_IMG_1584353721488.jpg


“Watanzania walifikiri mashtaka yetu yanahusika na kumuua Akwilina, hatuwezi kufunga faili la kesi ile bila kujua hatma ya Akwilina”.Mhe.Mbowe.

“Waliohusika wasiachwe wakacheza na maisha ya watanzania, hawa watu wachukue hatua mkononi kuwajua askari wote waliomuua Akwilina" Mhe.Mbowe.

“Mimi nikiwa jela kule nikiwa shambani zimepigwa risasi zaidi ya 13, za moto,wanapambana na Halima Mdee, Ester Bulaya, na Jesca Kishowa, hawa ni wamama, hata katika sheria za magereza wanaoruhusiwa kushughulika na wanawake ni wanawake tu, lakini hapa ni wanaume wenye vifua, wenye silaha, wanamshughulikia Halima wamemuweka mtu kati”. Mhe. Mbowe.

Mimi na viongozi wenzangu waandamizi tulipohudhuria sherehe za Uhuru uwanja wa Kirumba Mwanza nilipopewa nafasi ya kusalimia na nikamtaka rais aone ulazima wa kutengeneza maridhaino kuleta maridhiano… alisema nimesikia”.Mhe.Mbowe.

Sisi tulipoyataka maridhiano ya Kitaifa hayakuwa kielelezo cha uoga, ilikuwa kielelezo cha kuitaka amani katika nchi yetu kwa sababu tunaona tunakokwenda siko…”.Mhe.Mbowe.
''Natangaza rasmi kuwa kuanzia mwezi ujao wa nne tutaanza kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima bila kujali kuna katazo la Rais Magufuli na tuko tayari kwa lolote, tumekuwa waungwana vya kutosha na sasa hatutarudi nyuma kwenye hili'' - Freeman Mbowe

"Nawatangazia viongozi wote wa Chadema nchi nzima kuanzia Majimbo, Kanda, Kata, Vijiji na Mitaa kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima, kwanza ni kudai tume huru na pili ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu"
"Subira yetu, uvumilivu wetu na upole wetu umedharauliwa vya kutosha. Kama watatumia polisi na magereza kutufunga wote, watufunge. Tuko tayari kwa lolote. Kama wanafikiri mabomu, risasi na jela ni suluhu, basi wakatumie," Mbowe, Mwenyekiti Chadema
 
-
“Mimi nikiwa jela kule nikiwa shambani zimepigwa risasi zaidi ya 13,za moto,wanapambana na Halima Mdee, Ester Bulaya, na Jesca Kishowa,hawa ni wamama,hata katika sheria za magereza wanaoruhusiwa kushughulika na wanawake ni wanawake tu,lakini hapa ni wanaume wenye vifua,wenye silaha,wanamshughulikia Halima wamemuweka mtu kati”.Mhe.Mbowe.
 
Back
Top Bottom