Freeman Mbowe azindua siasa mpya za CHADEMA huku akitangaza idadi rasmi ya wanachama

Mh Mbowe ni Jabari la siasa, Lumumba wanahaha kumbe kufungia mikutano haikuwa dawa ya kuwadhoofisha hawa jamaa kabisa, sijui tuwaruhusu tu.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
hizo data ni za uongo. kila siku wana CHADEMA wanahamia CCM halafu huyu dj anasema chama kimeimarika? utapeli huu
Unaona wanaotangazwa lkn wasio tangazwa ni wengi kwelikweli!! ccm mshukuruni JPM vinginevyo kuta za ofisi zenu zingekuwa zimejaa makohozi.
 
Wote warembo, sio wale wa ccm majizee matupu na machangudoa ya kutupwa, yale yanayopakaa wanja unashuka mpaka kwenye shavu. Halafu cdm wajitahidi kutunga wimbo mpya wa hamasa, uwe na mashahiri mazito.
Siasa isikufanye ukashifu watu acha izo kijana kwani ukitengeneza hoja yako bila kukashifu watu unapungukiwa na Nini?
 
Wanachama njooni ccm bado tunalipa ada 100 kwa mwezi 1200 kwa mwaka.

Tupo kid8gitali tangu zamani. Karibuni sana wanachama wa chama cha mapinduzi

Sent using Jamii Forums mobile app
kafie mbele na mtumba wako wa CCM ,wenyewe unawajua?
Maiti mkubwa weee.
CCM imekwishaaa,hivisasa inapumulia gesi, na kama si mashine ya kusaidia mapigo ya moyo,basi zamani tungelikwisha izika 2015.
Hivi sasa iko ICU,na kama huamini,tazama nguvu wanazotumia kwenye chaguzi ili washinde kwa mabavu,haiungwi tena nkono na watanzania waliowengi
Mafisadi ndo wenye ccm yao.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amesema baada ya kuzuiliwa mikutano ya hadhara kwa hila chama hicho kimeimarika maradufu.
View attachment 1289779
Akihutubia mkutano mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema katija ukumbi wa Mlimani City kiongozi huyo amesema chama hicho kiliamua kufanya siasa mpya za kuzunguka kata zote nchini kuandikusha wanachama na kufanya mikakati ya ndani.

Mbowe amesema chama hicho hakitamani tena siasa za mikutano ya hadhara kwani wamegundua mikutano ya ndani ndiyo njia muhimu zaidi ya kujijenga kwani kuna uhalisia na unaweza kupima matokeo

Katika hatua nyingine Mbowe ametangaza rasmi idadi ya wanachama wa Chadema wenye kadi na kusema imefikia milioni 6.

Mbowe amesema chama kina database ya wanachama wote milioni 6 kwamba wapo wapi na jinsia yao ikiwemo idadi ya vijana,wazee,watoto,wanawake na wanaume.

Muda wote Mbowe alikuwa anashangiliwa kwa shangwe na mayowe na wanawake hao Bawacha kiasi kwamba wakati mwingine hotuba yake ilikuwa haisikiki vyema kwa kushangiliwa.


Kiongozi huyo wa Chadema amesema pia chama hicho siku ya mkutano mkuu tarehe 18 Dec kitazindua rasmi program ya chama ijulikanayo kama CHADEMA DIGITAL.Katika program hiyo wanachama watatumia simu zao kupata taarifa zote za chama na pia kulipia ada za uanachama.Pia Mbowe amesema ataliomba Baraza Kuu kuidhinisha ada ya uanachama kuwa shilingi elfu 2 badala ya elfu 1 kwa mwaka.

namba za simu zote zimesajiliwa kwa mfumo wa NIDA zina ratibiwa na TCRA hivyo ni rahisi wanachama wao kufuatiliwa na kujulikana wanaishi wapi na wanapanga nini, hapa ni kuwatia majaribuni wanachama hasa wenye nyadhifa, sidhani kama ni njia sahihi kwa chadema labda kama wanatafuta njia rahisi ya kukusanya mapato na tozo mbalimbali kutoka kwa wanachama.
 
Back
Top Bottom