Freeman Mbowe azindua siasa mpya za CHADEMA huku akitangaza idadi rasmi ya wanachama

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amesema baada ya kuzuiliwa mikutano ya hadhara kwa hila chama hicho kimeimarika maradufu.
1576152090637.png

Akihutubia mkutano mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema katija ukumbi wa Mlimani City kiongozi huyo amesema chama hicho kiliamua kufanya siasa mpya za kuzunguka kata zote nchini kuandikusha wanachama na kufanya mikakati ya ndani.

Mbowe amesema chama hicho hakitamani tena siasa za mikutano ya hadhara kwani wamegundua mikutano ya ndani ndiyo njia muhimu zaidi ya kujijenga kwani kuna uhalisia na unaweza kupima matokeo

Katika hatua nyingine Mbowe ametangaza rasmi idadi ya wanachama wa Chadema wenye kadi na kusema imefikia milioni 6.

Mbowe amesema chama kina database ya wanachama wote milioni 6 kwamba wapo wapi na jinsia yao ikiwemo idadi ya vijana,wazee,watoto,wanawake na wanaume.

Muda wote Mbowe alikuwa anashangiliwa kwa shangwe na mayowe na wanawake hao Bawacha kiasi kwamba wakati mwingine hotuba yake ilikuwa haisikiki vyema kwa kushangiliwa.


Kiongozi huyo wa Chadema amesema pia chama hicho siku ya mkutano mkuu tarehe 18 Dec kitazindua rasmi program ya chama ijulikanayo kama CHADEMA DIGITAL.Katika program hiyo wanachama watatumia simu zao kupata taarifa zote za chama na pia kulipia ada za uanachama.Pia Mbowe amesema ataliomba Baraza Kuu kuidhinisha ada ya uanachama kuwa shilingi elfu 2 badala ya elfu 1 kwa mwaka.
 
Kuhusu mikutano ya ndani sio wazo baya kama mikakati yao ni mizuri ili kuimarisha chama na kuelekeza ngumu kubwa ya darasa la uelewa wa itikadi, ilani na mwongozo wa chama kwa wanachama ndani na nje ya Tz. Mungu awaongoze
 
Wanachama njooni ccm bado tunalipa ada 100 kwa mwezi 1200 kwa mwaka.

Tupo kid8gitali tangu zamani. Karibuni sana wanachama wa chama cha mapinduzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom