Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe amewasili jijini Mwanza leo.
Kiongozi huyo mkuu wa upinzani nchini amewasili jijini Mwanza mchana huu akiwa na siri nzito moyoni kuhusu uteuzi wa nafasi ya Katibu mkuu wa chama hicho
Kiongozi huyo mara baada ya kuwasili alilakiwa na wajumbe wote wa Kamati Kuu wakiongozwa na Kaimu Katibu mkuu Salim Mwalim.
Mbowe aliwasalimia kwa furaha viongozi walioenda kumlaki huku akiwa na uso wa tabasamu muda wote.
Kuwasili kwa kiongozi huyo ni ishara mambo yamekamilika tayari kuongoza kikao cha Baraza kuu na Kamati Kuu.
Tayari mitandao yote ya kijamii,radio,televisheni na vyombo mbalimbali hapa nchini habari kuu ni Katibu mkuu mpya wa Chadema anayetarajiwa kujulikana Jumamosi wiki hii.