Upelelezi wa kina na wa kitaalamu ufanyike maana huu mtandao wa kigaidi ambao kiongozi wake ni Mbowe ulisambaa kila eneo la nchi yetu, hivyo tunaomba upelelezi wa kitaalamu ufanyike na unase mtandao wote ulio kuwa ukiratibu shughuli za kigaidi kwa maelekezo ya Mbowe.
 
Hayawi hayawi sasa yamekua, waswahili wanasema mchelea mwana kulia hulia mwenyewe....!
Kuna watu wapo tayari kuisaidia serikali kuhusu ugaidi wa mbowe. Wapo tayari kuisaidia serikali kuondoa magaidi yote nchini, nchi ibaki na amani...
Watu wengi wameonyesha kuwa tayari na hii inatokana na pengine mambo yake alikuwa akifanya akijua watu wanapenda kupenda kuna wazalendo wa nchi walikuwa wanamuangalia tu.
Huku mtaani nilipo kila mtu anashukuru serikali kwa hatua imazochukua kupambana na magaidi na pia wanasema nao wapo tayari kutoa ushahidi endapo serikali itahitaji.
Kwa kifupi ni kuwa safari hii hakuna jiwe litasalia juu ya jiwe.
Pia nitoe rai kwa watu wengine kama pia Wana ushahidi wamiminike zaidi kwenda kutoa ushahidi.
Ugaidi ni mbaya, ugaidi ni laana dunia nzima Hadi nchi zilizoendelea zinapiga vita ugaidi, hivyo yatupasa hapa kwetu pia kuunganaa na serikali kiyaapiga vita magaidi yote yaliyojificha kwenye kivuli cha siasa.
Pia niwaombe serikali hakuna kuonea huruma gaidi yoyote yule, serikali inapaswa kuwashughulikia ipasavyo.
Bila shaka wewe ni naibu shetani. Hakuna mtu mwenye akili asiyejua hii sanaa. Watu kama wewe, waabudu shetani, wasiokuwa na hofu ya adhabu baada ya mauti yao, pale wataposimama mbele za Mungu, hata kama hawamtaki, hamuwezi kushindwa kutunga matukio na kutoa ushahidi wa uongo. Hata Yesu Kristo alitungiwa mashtaka na mashahidi wa uwongo. Hakuna jipya unalolifanya.

Unaweza kutuambia matukio gani ya ugaidi aliyoyafanya ama kuyaasisi Mheshimiwa Mbowe? Mwogopeni Mungu. Matumbo yenu ni mifuko ya funza. Maisha ni mafupi. Mungu anaowaona na anachukia hila zenu.

HAKI HUINUA TAIFA. NCHI YANGU INAMASUALAL MENGI YA KUJIVUNIA BADALA YA MIKAKATI HOVYO YA KUUMIZA WATU WASIO NA HATIKA KWA JINSI ISIYO HALALI. SHAURI LENU!
 
Sio watu wanasema, sukuma Gang wapo wa kutoa huo ushahidi wa kupika, na hakimu wa kuendesha hiyo kesi yupo, na ameshapangwa hukumu iweje. Ila ukweli tunaujua. Yaani hizi mbinu mnazofany nyie majizi ya kura ni marudio tu, zote zimeshayika. Tena hapo ndipo ni kama mnachelewa, kesi ianze j3 kufika jumatano hukumu iwe imeshatoka.
Mkuu kwani sukuma gang si walishakomesha na mama kwa mujibu wa Malisa
 
Mkuu kwani sukuma gang si walishakomesha na mama kwa mujibu wa Malisa

Kwa sasa mama wa kambo hana jinsi zaidi ya kuwaridhisha sukuma Gang baada ya kuanza kumchimba. Hayo ndio matatizo ya urais wa kurithi.
 
Kwa sasa mama wa kambo hana jinsi zaidi ya kuwaridhisha sukuma Gang baada ya kuanza kumchimba. Hayo ndio matatizo ya urais wa kurithi.
Urais wa kurith vipi wakati ana power yote na mnasema anatawala kwa katiba ambayo ina mpa nguvu kubwa sana rais? Kwamba anaweza kutamka lolote mpaka hao sukuma gang wakapoteana?
 
Kukamatwa kwa Mwamba wa siasa za Tanzania Freeman Mbowe kwa tuhuma za uongo za ugaidi , kumekishangaza kituo cha Television cha CNN cha nchini Marekani , huu hapa ndio ujumbe wao

Askofu_Benson_Lwakalinda_Bagonza_(PhD)_Ameandika_... more.jpg
 
Mh Rais bila shaka humzima wa afya.

Naandika haya nikijua pengine polisi wanazo sababu za msingi kumshikilia Mh Mbowe na kumtuhumu kwa kile wanacho kiita "ugaidi" lakini ukweli ni kwamba Mh Mbowe ni mmoja wa watu wema ambao unaweza usiwe na shaka nao kabisa kuwa wanaweza fanya uhalifu wowote wa kudhulu viongozi au mtu fulani.

Mh Mbowe kama binadamu wengine ana madhaifu yake mengi katika kutekeleza shughuli zake za kisiasa lakini ni mmoja wa wanasiasa wasikivu, mvumilivu na mwenye upendo sana hata katika nyakati watu uona ni nyakati mbaya ambazo wengine wasingeweza kufikiwa au kusikiliza ya wengine lakini yeye amekuwa mtu wa tofauti siku zote.

Mh Rais, Mbowe anaweza akaonekana ana chochea vurugu au kuhatarisha amani ya nchi lakini ukweli ni kwamba Mh Mbowe ninayo hakika kabisa awezi kuruhusu mwanachadema yeyote kuhatarisha amani ya nchi yetu.

Mh Rais, Mbowe ni mmoja wa viongozi wenye busara sana pamoja na muda mwingine kuteleza kama binadamu.

Mh Rais unayo nafasi ya kusamehe na kuonesha uelekeo tena. Mh Mbowe ni msikivu atasikia na ni mtu ambaye anaweza ruhusu majadiliano hata katika nyakati ambazo si njema kama hizi.

Mh Rais, mimi sio shabiki wa Mbowe lakini mimi ni mmoja wa shabiki yake kwenye busara zake ambazo nimewai kuzishuhudia katika kushabikia siasa zetu hapa nchini nimeyaona mabaya na mazuri ya Mh Mbowe lakini nadiriki kusema Mh Mbowe ni mmoja wa viongozi wema na kamwe awezi kuwa na ubaya wa kufanya ugaidi.

Mh Rais nina imani utatafakari sana mazuri nas mabaya ya Mbowe lakini nina hakika utakubaliana nami kuwa ana stahili msamaha ana stahili kuachiwa huru.

Wasalaam
Hakika umeandika vizuri na kwa busara ya hali ya juu. CDM bado ni chama imara, ilq kinakosa agenda za kuungwa mkono kama ilivyokuwa miaka ya 2010s. Viongozi wa juu wa chama chao wanalazimika kutumia nguvu nyingi, pamoja na drama kurudisha attention yao kwenye jamii. The way wanafanya, watawala wanawaona kama tishio, hasa kwenye ustawi wa amani juu ya nchi, ukiona yaliyoyokea south Afrika, serikali ya Tanzania inakua na la kujifunza.

Ushauri wangu kwa CDM, waangalie namna mpya ya ku capture mioyo ya vijana, ambao ni wengi na wana hali ngumu ya maisha, pamoja na kukosa ajira kulikokithiri. Waje na ajenda zinazogusa maisha ya watanzania moja kwa moja na namna bora ya kutatua hizo changamoto.

Hakuna kijana aliyokosa ajira na kua na maisha duni, ataenda kuandamana kudai katiba mpya na uhuru wa kutoa maoni. Vijana wataandamana kudai ajira na mazingira mazuri ya kujenga uchumi wao. CDM badilikeni.
 
Urais wa kurith vipi wakati ana power yote na mnasema anatawala kwa katiba ambayo ina mpa nguvu kubwa sana rais? Kwamba anaweza kutamka lolote mpaka hao sukuma gang wakapoteana?

Anaweza kufanya lolote, lakini sio dhidi ya sukuma Gang. Anaweza kufanya lolote kwenye kuminya haki, lakini sio kwenye kulinda maslahi ya majizi wenzake wa kura. Pamoja na nguvu zote wanazopata kupitia katiba hii, ukweli wa kuwa yuko madarakani kwa wizi wa kura haufichiki, hivyo ni aidha asimamie kwenye haki ile kwake, au alinde maslahi ya majizi wenzake. Na kwa sasa ameamua kusimama na upande wa majizi wenzake.
 
Mkuu kwani kwa mujibu wako huyu mama si siyo dhalimu kama Magufuli?

Sasa haya ya sukuma gang yanatoka wapi?

Yeye ni muungwana sana kwa mujibu wako,
Kwa mujibu wako halindwi na mabunduki kama dhalimu wako, kwa sababu yeye siyo dhalimu kwa hiyo haogopi chochote.

Na kwa vile siyo dhalimu kama unavyosemaga si anaweza kuifutilia mbali hiyo sukuma gang yako unayoisema?
 
Mh Rais bila shaka humzima wa afya.

Naandika haya nikijua pengine polisi wanazo sababu za msingi kumshikilia Mh Mbowe na kumtuhumu kwa kile wanacho kiita "ugaidi" lakini ukweli ni kwamba Mh Mbowe ni mmoja wa watu wema ambao unaweza usiwe na shaka nao kabisa kuwa wanaweza fanya uhalifu wowote wa kudhulu viongozi au mtu fulani.

Mh Mbowe kama binadamu wengine ana madhaifu yake mengi katika kutekeleza shughuli zake za kisiasa lakini ni mmoja wa wanasiasa wasikivu, mvumilivu na mwenye upendo sana hata katika nyakati watu uona ni nyakati mbaya ambazo wengine wasingeweza kufikiwa au kusikiliza ya wengine lakini yeye amekuwa mtu wa tofauti siku zote.

Mh Rais, Mbowe anaweza akaonekana ana chochea vurugu au kuhatarisha amani ya nchi lakini ukweli ni kwamba Mh Mbowe ninayo hakika kabisa awezi kuruhusu mwanachadema yeyote kuhatarisha amani ya nchi yetu.

Mh Rais, Mbowe ni mmoja wa viongozi wenye busara sana pamoja na muda mwingine kuteleza kama binadamu.

Mh Rais unayo nafasi ya kusamehe na kuonesha uelekeo tena. Mh Mbowe ni msikivu atasikia na ni mtu ambaye anaweza ruhusu majadiliano hata katika nyakati ambazo si njema kama hizi.

Mh Rais, mimi sio shabiki wa Mbowe lakini mimi ni mmoja wa shabiki yake kwenye busara zake ambazo nimewai kuzishuhudia katika kushabikia siasa zetu hapa nchini nimeyaona mabaya na mazuri ya Mh Mbowe lakini nadiriki kusema Mh Mbowe ni mmoja wa viongozi wema na kamwe awezi kuwa na ubaya wa kufanya ugaidi.

Mh Rais nina imani utatafakari sana mazuri nas mabaya ya Mbowe lakini nina hakika utakubaliana nami kuwa ana stahili msamaha ana stahili kuachiwa huru.

Wasalaam
Bila kupinga maelezo yako mengine mazuri, unataka Mbowe asamehewe kwani amefanya kosa gani? Au asamehewe kubambikiwa kesi? Sioni msingi wowote wa yeye kusamehewa wakati hana kosa. Tusitake kuwapa wahalifu haki ya kuhukumu wenye haki, yaani watu kuwa viongozi haimaanishi wasemacho ni kweli, maana huko kubambikizia kesi sio jambo geni, ila tutawapa uhalali hao walevi wa madaraka kutaka wamsamehe mtu wanayemuonea.
 
Mkuu kwani kwa mujibu wako huyu mama si siyo dhalimu kama Magufuli?

Sasa haya ya sukuma gang yanatoka wapi?

Yeye ni muungwana sana kwa mujibu wako,
Kwa mujibu wako halindwi na mabunduki kama dhalimu wako, kwa sababu yeye siyo dhalimu kwa hiyo haogopi chochote.

Na kwa vile siyo dhalimu kama unavyosemaga si anaweza kuifutilia mbali hiyo sukuma gang yako unayoisema?

Narudia tena, huyo mama sio dhalimu kama yule ibilisi, ila amekubali kuridhisha hilo kundi la wadhalimu kwani ana cheo cha urithi, tena cheo cha wizi wa kura. Hivyo hana namna zaidi ya kutumikia kundi la waouvu, kwani utawala wake umepatikana kwa uovu hata yeye hilo analijua. Angekuwa yuko madarakani kwa kura halali angeweza kulifuta hilo kundi la sukuma Gang, ila sio kwa namna madaraka hayo yalivyopatika. Habari ndio hiyo boss.
 
Ana power yote inayosapotiwa na katiba mnayotaka ibadilishwe!

Vyombo vyote vya usalama vinamtii yeye!
.
Sasa inakuwaje hana hiyo nguvu ya kuvunjilia mbali hilo genge wakati yeye siyo dhalimu kama yule dhalimu wako?
 
Baada ya upekuzi wa Polisi kukamilika nyumbani Kwa M.Kiti Mbowe, tumepokea taarifa za kushtua na kushangaza kuwa Polisi wamemwambia kuwa ataunganishwa kwenye kesi ya Ugaidi na watuhumiwa walioko gereza mojawapo DSM. Tutaendelea kutoa taarifa za kina hapo baadaye.

View attachment 1862953

====

UPDATES;

=====

TAARIFA KWA UMMA

JESHI LA POLISI LAMTUHUMU MWENYEKITI WA CHAMA
MHE.FREEMAN MBOWE NA "MAKOSA YA UGAIDI"

Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Freeman Mbowe alifikishwa Dar es Salaam jana majira ya saa tatu usiku chini ya ulinzi wa Polisi , walimpeleka nyumbani kwake Mikocheni Kwa ajili ya kumfanyia upekuzi ambao ulichukua takribani saa mbili na nusu.

Baada ya upekuzi huo Polisi waliondoka na Kompyuta mpakato (Laptop) na Vishikwambi (tablets) za watoto wake, Kompyuta mpakato moja ya kwake na modem ya Internet Kwa ajili ya uchunguzi wao.

Leo majira ya saa Saba mchana Polisi walimfikisha Mhe. Freeman Mbowe Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano na kuchukua maelezo yake.

Polisi walitaka maelezo kutoka Kwa Mhe. Freeman Mbowe kuhusiana na kosa waliloliita 'KULA NJAMA ZA KUTENDA KOSA LA UGAIDI'

Baada ya maelezo hayo ya Polisi Mhe. Freeman Mbowe alitumia haki yake ya kisheria na aliamua kutokutoa maelezo yoyote Polisi kwa mujibu wa Sheria. Baada ya maelezo hayo Polisi wamemrejesha Mhe. Freeman Mbowe katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay ,Jijini Dar es Salaam.

Aidha , viongozi wengine waliokuwa wanashikiliwa Mkoani Mwanza wameendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi na baadhi yao walifanyiwa upekuzi nyumbani kwao na vyumba vya hotel ambako walikuwa wameshukia .

Waraka wa Mbowe kwa Watanzania
Mwenyekiti Taifa Mhe. Freeman Mbowe ametuma waraka kwa Watanzania kama ifuatavyo;
"Hatimaye madai ya Katiba Mpya yamenisababishia kesi ya ugaidi, nipo tayari kwa mashtaka ya kuchongwa siogopi. Ninaamini Dunia itaujua ukweli wa kile kinachoendelea Tanzania na kile tunachokipitia Watanzania. Lakini pia itajua ukweli juu ya makosa haya ya kuchongwa.

Natoa wito kwa watanzania kuendeleza mapambano, haki hutafutwa” Mhe.
Freeman Mbowe.”

Imetolewa leo Alhamisi tarehe 22 Julai, 2021.

John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.

=====

UPDATE:

View attachment 1863559
View attachment 1863560
UGAIDI, hata Maana ya UGAIDI hamjui, mpo shabikia tu, twende tu
 
Back
Top Bottom