Mtini
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 1,491
- 2,355
Wakati wa kupendekeza Jina la katibu mkuu, Mbowe alisema watoto wake wanashindia maharage, kitu ambacho hakina uhalisia bali ni kuuadaa umma wa CHADEMA ili waamini kiongozi wao anajitolea kila senti anayoipata kwa ajili ya chama na anabakisha kidogo sana kwaajili ya familia yake kiasi cha kushindwa kumudu nyama robo.
Kipindi cha uchaguzi mkuu Slaa naye alisema anashindia mihogo hadi tukambatiza jina la DOKTA MIHOGO, lakini baada ya muda mfupi tunaona kahamia ughaibuni na kufunga ndoa huko. Hivi kweli mlo mihogo anaweza afford hayo?
Sina lengo la kuingilia maisha ya Mbowe ila nahoji uadilifu wa kusema kweli mbele ya Watanzania, kama unashindwa kusema kweli kwa lililo dogo unawezaje kuwa mkweli kwa jambo kubwa?