Ni takriban wiki 3 zimesalia pekee kushuhudia mpambano wa kukata na shoka kati ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu kukalia kiti cha Chama kikuu cha Upinzani Tanzania CHADEMA.
Kumekuwa na mpambano mkali kwenye mitandao ya kijamii hasa nani anafaa kuchaguliwa kuongoza chama hicho katika uchaguzi wa Januari 21
Katika uchunguzi uliofanywa na Molemo Media Tundu Lissu anaonekana kuungwa mkono kwa wingi na makundi ya watu yaliyo nje ya chama hicho kama vile wanaharakati na Watanzania waishio nje ya nchi wanaojulikana kama Diasspora.
Freeman Mbowe anayetetea kiti chake anaonekana kuungwa mkono na wapiga kura wengi ndani ya chama hicho.Mpaka sasa ana uhakika wa kupata walau robo tatu ya kura zote zitakazopigwa kwenye mkutano mkuu.
Uchunguzi wa Molemo Media umegundua Freeman Mbowe anaweza kuzoa kura zote za Unguja na Pemba kutokana na kile wajumbe wanachodai matamshi tata ya Tundu Lissu kuhusu Muungano na kuonekana hapendelei sana upande wa Zanzibar.
Pia uchunguzi unaonyesha Freeman Mbowe anaungwa mkono na idadi kubwa ya wajumbe katika Kanda za Nyasa, Kusini, Kaskazini, Magharibi, Victoria na Kanda ya Kati.
Tundu Lissu anaonekana amejikita zaidi Kanda ya Serengeti na kwa uchache Kanda ya Pwani.
Uchunguzi zaidi uliyo huru wa Molemo Media unaonyesha wajumbe wengi wa mkutano mkuu wanaamini kumpigia kura Freeman Mbowe ni kukibakisha chama katika mikono salama na kumchagua Tundu Lissu ni kukiweka rehani kwa wanaharakati na watu waishio nje ya nchi.
Katika mahojiano yasiyo rasmi yaliyofanywa na Molemo Media pamoja na watu maarufu ndani ya Chadema, wamemshauri Freeman Mbowe endapo kama atachaguliwa kuwa Mwenyekiti basi amteue Tundu Lissu kuwa mjumbe wa Kamati Kuu.
Wachunguzi wa mambo wanadai kumteua Tundu Lissu kuwa mjumbe wa Kamati Kuu kutasaidia kuimarisha umoja ndani ya chama hicho na pia kutaendelea kuwavuta wanaharakati waendelee kukiunga mkono chama hicho ambao wamekuwa wakikishabikia miaka mingi.
Yote kwa yote kilichobaki ni siku tu ya kupiga kura kwani inaonekana tayari idadi kubwa ya wajumbe wa mkutano mkuu wameshachagua upande wa kuunga mkono.