Freelancing: Leo nimepata order/kazi yangu ya kwanza kama freelancer!

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
21,252
34,202
I salute y'all!

Ndugu zangu, miaka kadhaa sasa nilikua na sera binafsi ya uwekezaji katika maarifa hasa katika kusoma vitabu na kujifunza vitu ambavyo kwanza sijavisoma chuoni na pili niliamini vina demand kubwa huko majuu na hapa Tanzania.

Baadhi ya hivyo vitu ni website development, Search engine optimization (SEO) na digital marketing hasa kwenye mitandao ya FB na Instagram! Hizo ni baadhi tu ya fields ambazo niliwekeza muda wangu kujisomea/kujifunza!

Miaka miwili iliyopita nilisikia kwa mara ya kwanza juu ya freelancing na kwa kumbukumbu zangu ilikua hapa hapa JF kule kwenye jukwaa la ajira (too bad nimemsahau aliyeleta ule uzi)!

By that time nilianza na nilijisajili katika websites kadhaa lakini bahati mbaya sikufanikiwa, so nikakata tamaa!

Mwaka huu tena nikajaribu, bila bila! hamna mtu alifungua profile yangu au kukubali proposal yangu! so literally nikakata tamaa!

Basi mwaka huu nikarudi tena kwa mara nyingine! na leo ndio nimepata kazi yangu ya kwanza na client wa hii kazi anatokea huko majuu (Italy)!

Ilikua hivi...

Juzi huyu client alituma request na nikachelewa kujibu, (in fact nilikua siangalii sana meseji maana nilikua najua no one will even bother to view my profile!) sasa jana nikasema acha nipite niangalie kama kuna jipya!

Ndio nikakutana na meseji yake na anahitaji huduma yangu! Duh, nikaona nishapishana na gari la mshahara na wenda ashapata huduma kwa freelancers wengine!

Nikasema si mbaya acha nimjibu meseji asipojibu basi haikua riziki yangu! Nikajibu meseji nikaona yuko kimya nikapotezea nikajua ishakula kwangu...

Sasa leo ndio akajibu meseji yangu and finally nikapata order rasmi! order yangu ywa kwanza kwenye ulimwengu wa freelancing!

Hii kazi nimeipokea leo mchana na hela yangu nimelipwa!

Natakiwa niifanye kwa Siku Nne (4 days)!

Na mpaka sasa nimesha imaliza kwa zaidi ya asilimia 80%! Lengo langu ni kumaliza hii kazi mapema na kwa ubora wa kiwango cha juu iwezekanavyo hata kabla ya muda tulio kubaliana na mteja wangu haujafika!

So far nilichojifunza kwenye freelancing ni kwamba:

Kwanza lazima uwe online yaani usichelewe kujibu meseji za wateja kama wakija!

Pili lazima uwe mvumilivu!

Tatu Lazima uwe na Skills!

Bado nna mengi ya kujifunza ila kwa so far nimefikia hapa!

(Kwa sasa naachia hapa mengine nitajazia as time goes...)
 
Malipo yanalipwa kwa njia gani?

Sent using Intellectual Skills
Wana mfumo wao wa malipo, ukilipwa inabaki kwenye account then from there ndio unaweza ku withdraw kwa kutumia wire transfer au paypal!

Binafsi kwa sasa siwazi sana pesa, nahitaji kujenga trust kwanza kutoka kwa buyers!

Hii itaenda sambamba na kuwekeza zaidi kwenye UJUZI hasa kwenye kozi za kulipia (huko udemy, coursera), kufungua accounts kwenye freelancing websites nyingine na kuwekeza kwenye TOOLS (kama premium themes, host na plugins) baada ya hapo nitaanza kufikiria mambo ya kutoa pesa na kutumia!

Karibu!
 
Back
Top Bottom