TANZIA Fredy Sam, mmiliki wa Rose Garden Dodoma afariki Dunia

Hivi hii kauli ya kila nafsi itaonja mauti huwa ina maanisha nini na huwa mnaitoa wapi?


كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۖ فَمَنْ زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ۗ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ

Kila nafsi itaonja mauti. Na bila ya shaka mtapewa ujira wenu kaamili Siku ya Kiyama. Na atakaye epushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu. Na maisha ya dunia si kitu ila ni starehe ya udanganyifu. Al-'Imran, Aya ya 185
 
Utajiri wa kiafrika mara nyingi unaambatana sana na pressure, kisukari, shambulio la moyo nk.

Sijui tunakosea wapi.
Rest well mr. business man.
Unaambiwa hela yako mwenyewe ndio inakuua. Sweken hata mambo ya UVIKO barakoa hawajali wanadunda tu.
 
Tajiri ambaye pia ni Mmiliki wa Rose Garden Dodoma na ukumbi wa sherehe wa Kikimanj Ndugu Fredy Sam amefariki Dunia jana usiku akiwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya Aghakan Jijini Dar es salaam.

Bwana Fredy alifikishwa hospitalini hapo wiki tatu zilizopita akiwa anasumbuliwa na pressure iliyopelekea kupata stroke.

Mipango ya mazishi inafanyika Dodoma, Dar na Moshi
Related news
 
Back
Top Bottom