Fredrick Sumaye leo anatarajiwa kuhutubia mkutano wa hadhara Temeke DSM katika uzinduzi wa kampeni za udiwani

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye leo anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa Hadhara Temeke DSM katika kuzindua kampeni za mgombea udiwani wa Chadema wa Kata ya Kijichi.

Mheshimiwa Sumaye ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu Chadema na Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani atafuatana na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salim Mwalimu na Mkurugenzi wa Mafunzo Benson Kigaila.

Pamoja na mambo mengine Sumaye anatarajiwa kupasua jipu kuhusu uvunjifu wa haki za Binadamu nchini ikiwemo kupigwa risasi kwa mwanasiasa maarufu zaidi Afrika Mashariki Tundu Lissu.

Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Kwa Tesha Kijichi mwisho.
 
Sumaye ndio nani?

Tusubiri hotuba za brother soon atapata nguvu.
Hao wengine wambieni wakae na unafiki wao huko huko.
 
Nimeona vipeperushi vya chadema huko. Aisee aibu. Hivi yale mabango makubwa makubwa nani alikuwa anatoa hela.

Yaani wasipoteze muda na kula hela tu za ruzuku. Wamsaidie huyu Bonge hata atoe mabango.
 
pamoja na mambo mengine, atazungumzia habari ya lisu kupigwa risasi!
hivi hakuna changamoto ambazo wananchi wa kata hiyo watahitaji zitatuliwe, ambazo mnaweza kuziweka ktk hoja zenu, ili wananchi wawape ridhaa ya kuongoza?
 
Changamoto hazitatuliwi na wapinzani. Zinatatuliwa serikalli iliyopo madarakani
 
Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye leo anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa Hadhara Temeke DSM katika kuzindua kampeni za mgombea udiwani wa Chadema wa Kata ya Kijichi.

Mheshimiwa Sumaye ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu Chadema na Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani atafuatana na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salim Mwalimu na Mkurugenzi wa Mafunzo Benson Kigaila.

Pamoja na mambo mengine Sumaye anatarajiwa kupasua jipu kuhusu uvunjifu wa haki za Binadamu nchini ikiwemo kupigwa risasi kwa mwanasiasa maarufu zaidi Afrika Mashariki Tundu Lissu.

Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Kwa Tesha Kijichi mwisho.
Oooh tena mkutano utasambalatishwa nae atakamatwa kwa kuhutubia mkutano kwenye jimbo lisilo lake, naogopa mwenzenu.
 
Back
Top Bottom