Fredrick Mwakalebela aula, aitwa kuanza kazi shirika la makumbusho ya taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fredrick Mwakalebela aula, aitwa kuanza kazi shirika la makumbusho ya taifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shibalanga, Jul 2, 2011.

 1. Shibalanga

  Shibalanga Senior Member

  #1
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Fredrick Mwakalebela aliyewahi kuwa katibu mkuu wa TFF na Mgombea ubunge wa Iringa mjini (CCM) kabla hajawekewa mizengwe ya rushwa, amepata kazi shirika la makumbusho ya Taifa (National museum of Tanzania) kuwa AFISA UTUMISHI NA UTAWALA MKUU, ama kweli kama wasemavyo waungwana Mungu akifunga mlango moja hufungua mlango mwingine cha muhimu ni kutokukata tamaa. kila la kheri Mwakalebela katika majukumu yako mapya.

  Source: Mwananchi
   
 2. Jaxx

  Jaxx Senior Member

  #2
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa nchi hii hilo lilitegemewa maana baada ya kuchakachuliwa aliombwa ajumuike kwenye Kampeni na ili baadaye apate kijikeki na Mungu siyo Jaxx kapata kakeki kidogo angalau apunguze machungu; Tunasubiri wengine hata wale wa Mwanza maana watapewa ubunge viti vya rais....jiulize kwanini mpaka leo wakuu wa mikoa hawajateuliwa then ujiongeze....tunajipanga kulipa fadhili kwa umakini kabisa maana hii ndiyo kete yetu ya mwisho
   
 3. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Maajabu ya kikwete na ajira za mafisadi wenzie hayaishi
  huyu naye ni gamba gumu maslahi binafsi
  kumbe zile kesi ilikuwa ni kupoteza muda wa mahakimu na TAKURUKU
  kutudanganya wananchi kwamba wanafanya kazi,

  mbona kesi kashinda fasta na kazi kubwa tena kitengo muhimu
   
 4. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Hayo ya kawaida nji hii. Tumeyazowea Mkuu!
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Kupata kazi nchi ndio kuula??????
  Basi nchi hatuna
   
 6. Shibalanga

  Shibalanga Senior Member

  #6
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Mkuu ni kuula maana kama watu wanakutakia mabaya unafikiri ni kufanya nini? kazi zinapatikana kwa ugumu mkubwa siku hizi.
   
 7. Shibalanga

  Shibalanga Senior Member

  #7
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Ikiwa TAKUKURU walimpeleka mahakamani kwa tuhuma za rushwa basi wao ndo walikurupuka na hawakuwa na ushahidi wa kutosha au basi wakubali walitumiwa ili kumdhoofisha ili asiweze kugombea tena, nadhani CCM makao makuu na yule mama Monica Mbega ndo wa kulaumiwa kwa hili kwani wao ndo watakuwa walichora mchoro huu, lakini mimi nasema malipo ni hapa hapa Duniani, ndo maana hata yule mama naye hakupata hata huo ubunge wenyewe.
   
 8. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  huu ndio ukweli kapata kazi kaula wala hakuna maelezo mengine
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  mimi napenda sana resilience ya watu wa Mbeya na Iringa

  hawakubali kupelekwa kupelekwa bila mpango
   
 10. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwani unafikiri kapewa hiyo kazi bila usaili, msimwtike kila zigo Mzee JK, hilo nadhani ni suala la kazi ilitangazwa, na akaomba aka sailiwa na kuonekana nibora miongoni mwa wasailiwa. Ingekuwa kateuliwa na rais, labda tungeweka shaka lakini kwa hili acha umbea!!!
   
 11. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Acha kupotosha bana.........

  Mwakalebela alishinda kesi ya TAKUKURU kihalali na si fasta kama unavyodai,kesi imechukua karibu miezi 8 wewe unasema kashinda fasta?,kesi yenyewe ya kudaiwa kutia rushwa ya Tshs.100,000/=!!!!!!!!!!...

  Kuhus ajira,usiseme kwamba Mwakalebela amepewa,huu ni upotoshaji pia,Makumbusho walitangaza ajira kwenye magazeti na sehemu nyingine na watu wakaomba(akiwemo Mwakalebela),usaili ulifanyika na Mwakalebela akashinda.Kumbuka kwamba Mwakalebela ni msomi kwa kiwango cha shahada ya pili ya uzamili ya utawala wa biashara(MBA) na kabla hajawa Katibu mkuu wa TFF alikuwa ni Afisa utawala wa kiwanda cha mtibwa kule Manungu kwa kipindi kirefu tu so anazo sifa za kutosha kupewa nafasi hiyo na si kwamba kapewa kama unavyodai wewe.....

  Bala.
   
 12. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,311
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Hongera Mwakalebela unastahili kutokana na ujuzi wako na shule yako....fanya kazi jipange upya 2015 iringa yako tu
   
 13. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  mkuu nami naungana na wengi kumpongeza kwa kupata ajira mpya. Tangu mwez wa 4 alipoitwa kwa usaili niliwai kuandika apa jf kuwa lazima akwae icho kitengo kutokana na sifa alizonazo mwakalebela. Ila sikusita kutoa dukuduku pia kuwa iyo nafasi kawekwa,haijalishi kaombaje. Hii ni kwa kuwa haiwezekani mtu alikuwa ana kesi ya kujibu dhidi ya uyo mwajili mpya ila apo apo anatoka mahakamani kujibu kesi anaenda usaili National museums. Jina lake lilipitisha hata kabla hajashinda kesi,kitu kilichozua hisia kali kwa watu makini. Yani ni sawa na Jerry Muro sasa ivi alivo na kesi ila anaitwa kwenye interview mfano kuwa mkurugenzi wa Tbc1 shirika la uyo uyo anayekushtaki. Hapa watu makini walijadili hapa hapa jf kuwa kesi ya rushwa ya uchaguz ilikuwa usanii,pili walijua lazma awe huru alaf aende pale national museum. Siipingi ajira ya ndugu mwakalebela ila skeptical senses zilishajionesha mapema. Hongera ndugu Fred Mwaka.
   
 14. Queen Kyusa

  Queen Kyusa JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2011
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35  Acha kutuzuga nani asiye ijua serikali ya nchii unaitwa kwenye interview just kutimiza wajibu lakini mtu anakuwa ameishapangwa the same tu huyo mwakalebela kuna mkono wa jk hapo no doubt. Siku zinakuja mambo ya kulipana fadhila yatakomeshwa shame on you magambaz
   
 15. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hakuna cha kufunga wala kufungua mlango hapo. Huyo bwana amepewa hiyo kazi na chama chake. Hana proffesion yakumuweka hapo. Kabebwa!
   
 16. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nchi hii fedha zinachezewa, kila siku kesi zinaendeshwa halafu mwisho wake serikali inashindwa
   
 17. MANI

  MANI Platinum Member

  #17
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Kwa chama kipi hicho cha magamba walichomsaliti?
   
 18. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jamani tupeni CV ya Mwakalebela
   
 19. mchakachuaji192

  mchakachuaji192 JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hii ndio bongo bana, kwa chama cha magamba huwezi kukurupuka tu na kusema nagombea ubunge, lazima upitie hatua fulani fulani kufikia kwenye kugombea ubunge, haya apige kazi huko tutasikia tena ni wapi atapelekwa baada ya hapo safari ya ubunge ndio hiyo iko njiani kwa huyu jamaa
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mwakalebela na ujuzu gani na mambo ya kale/makumbusho? Yeye ni curator? Amesoma anathropology? or histrory? or anything close na makumbusho? Nahisi hii nafasi anaweza akawa amepewa kwa utashi wa kiasi, na hofu yangu ni kwamba Serikali achalia mbali Mwakalebela haiwaelewi fani hii ya makumbusho, na mbaya zaidi hawatambui 'potentials' za makumbusho kwenye uchumi wa Taifa!

  Nasema haya kwa sababu kubwa moja, ukitembelea jumba la makumbusho ya Taifa Dar es Salaam utaona how 'shallow it is' kuna vitu vingi sana bado hajikuwepo, na hata mazingira yake yamekaa hovyo hovyo pamoja na kwamba hela za misaada zimekuwa zinatolewa. Balozi wa EU hapa nchini (Tim Clarke) kwa muda alijitahidi sana kuonana na aliyekuwa mkuu wa makumbusho (Dr somebody) lakini kwa maajab ya musa kila walipopanga meeting huyu bwana mkubwa wa makumbusho akawa hatokezi na akipigiwa simu anasema 'kasahau'!!! Balozi Clarke alitaka ku-discuss namna ya KUSAIDIA kuinua hadhi ya jumba la makumbusho na kwa bahati nzuri mke wa Balozi (Mrs Clarke) kasomea mambo ya kale.

  Lile jumba pale mjini limekuwa na uzio wa mabati for years, ni marekebisho gani hayo yasiyoisha. Ukiingia ndani mambo hayajaa vizuri both presentation & contents wise. Ukitembelea mikoani suala zima la makumbusho ni kama hakuna kabisa. Sasa Mwakalebela anaweza akawa na jibu la kuridhisha kuhusu 'neglect' ya makumbusho Tanzania? tusubiri.
   
Loading...