Fredrick Mchauru - Mtanzania wa kwanza kupata scholarship atimiza miaka 100. Alikuwa Katibu Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Tanganyika

Ngwanakilala

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
774
1,456
Mzee Fredrick Mchauru ambae ni mtanzania wa kwanza kuwai kupata scholarship nchini Tanzania ametimiza miaka 100 leo April 25. Mzee Mchauru alizaliwa tarehe 25 April mwaka 1920 huko Newala Mtwara na alisoma Sekondari ya Chidya na Minaki.

Mzee huyu alikua katibu mkuu katika serikali ya kwanza ya Tanganyika chini ya Rais Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kwasasa makatibu wakuu wa serikali ya Kwanza ya Tanganyika walioko hai ni wawili tu – Mzee Mchauru na Mzee Cleopa David Msuya

1587836136670.png


Mwaka 1944 Mzee Mchauru pamoja na Mangi Mkuu Thomas Marealle ndio walikua kati ya watanzania wa kwanza kuwai kupata scholarship kutoka kwa serikali ya mkoloni muingereza kwenda kusoma London School of Economics.

Walipofika uingereza walikuta chuo chao kimegeuzwa kua kambi ya wanajeshi wanaopigana vita kuu ya pili ya dunia hivyo walilazimika kwenda kuishi katika chuo kingine huko Birmigham mpaka vita ilipokwisha. Walisoma degree na kumaliza mwaka 1948. Walirudi nyumbani pamoja mwaka 1948 ambapo Mzee Mchauru aliajiriwa kama afisa maendeleo ya jamii mkoani Tabora wakati Marealle aliajiriwa nafasi hiyo hiyo mkoani Morogoro
1587839034240.png

Mzee Mchauru alikua mume wa Katibu Mkuu wa Zamani wa UWT mama Tecla Mchauru, - aliekua rafiki mkubwa wa mama Anna Abdallah - Mrs Msekwa

1587836165670.png


Kuanzia mwaka 1962 Mzee Mchauru alifanya kazi kama Principle wa kwanza wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru. Mwanzo chuo hiki kilijengwa kama Polish refugee camp yaani kambi ya wakimbizi wakipolish wa vita kuu ya dunia.

Wakimbizi hao wapolish walifungua ranch ya mifugo hapo Tengeru ambayo baadae ilibadilishwa n akua Chuo cha Tengeru ambacho kipo mpaka leo. After the refugees departed, the government used the site to develop an agricultural research station with soil conservation services. The Game Department was also added to the site.

Picha hapa chini inamuonyesha Mzee Mchauru akiwa Principle wa Chuo cha tengeru akimsikiliza naibu waziri alietembelea chuo hicho mwaka 1962 mama Lucy Lamerk

1587836187951.png


Baada ya Uhuru mwaka 1965 Mzee Mchauru alichaguliwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kua Katibu Mkuu wa iliyokua Wizara ya Ustawi wa jamii, Ushirika na Utamaduni.

Wakati huo Serikali ya Mwalimu Nyerere ilikua na Makatibu Wakuu 19 chini ya Chief Secretary Joseph Augustine Namata. Makatibu wakuu hao walikua Bwana Dunstan Alfred Omari, Dan Nkembo, Paul Sozigwa, the two Mulokozi’s –Bernard Kyaruzi and his brother Dr. Vestadus Kyaruzi, Cecil Kalaghe, Cleopa Msuya, Obed Katikaza, Amon Nsekela, Dr. D. Mtawali and Chief Mwinamila Lukumbuzya. The Attorney General was Mark Bomani
1587836204460.png



Pichani hapa chini Mzee Mchauru akiwa na Waziri wa Ulinzi bwana Edward Sokoine na rais wa Korea bwana Kim IL Sung (wakati kati)

1587836219905.png



Picha ingine hapa chini ikimuonyesha mzee Mchauru akisalimiana na waziri mkuu wa china bwana Chou Enlai huko China mwaka 1972

1587836235808.png


Baada ya hapo Mzee Mchauru aliteuliwa kua Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Ndani ya nchi toka mwaka 1968 to 1971 akifanya kazi na IGP Elangwa Shaidi & Hamza Aziz (Hamza Aziz ni kaka wa Dossa Azi – wote ni Watoto wa Aziz Ali aliekua anamiliki eneo lote la Mtoni kwa Aziz Ali estate). Pichani hapo chini Mzee Mchauru na IGP Elangwa Shaidi wakimsikiliza rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume


1587836253555.png


In 1972 President Julius Kambarage Nyerere established the Ministry of Defence and National Services and Mchauru was appointed to become its first Permanent Secretary and Hon. Edward Moringe Sokoine as its Minister.

Mzee Mchauru retired government services in 1973 and become either adviser or Board Member to several government and private entities. Aliwai kua Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta na Simu na Shirika la Geita Gold Mines Ambalo baadae lilikuja kua Ashanti Gold Mine (mashirika haya yalianzishwa kwa ushirikiano wake yeye na Mr Niven Sinclair wa uingereza – pichani hapo chini)

1587836283033.png


Pichani hapo chini Mzee Mchauru akiwa kwenye sherehe ya kumuaga IGP Elangwa Shaid na Kumkiribisha IGP Hamza Aziz watatu kutoka kulia

1587836327191.png


Mzee Mchauru is a true statesman and a civilian servant who worked for the colonial government and the free Tanganyika all his life. He worked for the government for 26 years from 1947 to 1973 and continued on as an advisor and board member to private & government institutions for another 26 years from 1973 to 1999 making a total of 52 year of service and excellence.

This autobiography is an extraordinarily candid portrait of a humble man who decided early in life to devote his life & intellectual gifts, and his astonishing capacity for hard work, to serving his country.

Indeed, the life and times of Mzee Fredrick Mchauru is the life and times of Tanzania First Phase Government of Mwalimu Nyerere.

Kwasasa Mzee Mchauru anaishi na familia yake jijini Dar es salaam huko Upanga Magharibi Mtaa wa Kitonga Plot 121 nyuma ya hospitali ya Tumaini.

Happy Birthday babu, happy birthday baba. Tunakuombea Maisha marefu zaidi yenye afya na fanaka.. Hakika tunayo kila haki ya kumshukuru Mungu kwa upendo wake mkuu
 
Interesting!
Huyu mzee ana uhusiano wowote na kijiji kimoja kule Masasi kunaitwa Mchauru?

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndio kijiji hiko ndiko familia yake ilikotoka

Pia Geita Gold Mines kuna either Library au Lunch room iitwayo Mchauru Library kwa ukumbusho wake

Mzee ni Nyerere type ndio maana sio bilionea na ndio maana hajulikani. Hakuiba hata shillingi na anafurahia hilo sana sana. Anasema hajawai kua na tamaa ya mali wala utajiri bali yeye alipenda utumishi wa umma tu
 
Ndio kijiji hiko ndiko familia yake ilikotoka

Pia Geita Gold Mines kuna either Library au Lunch room iitwayo Mchauru Library kwa ukumbusho wake

Mzee ni Nyerere type ndio maana sio bilionea na ndio maana hajulikani. Hakuiba hata shillingi na anafurahia hilo sana sana. Anasema hajawai kua na tamaa ya mali wala utajiri bali yeye alipenda utumishi wa umma tu
Safi sana...kizazi cha dhahabu hicho....kinaaga
 
Hongereni kwa babu kutimiza miaka hiyo..miaka mia ni nadra sana.

Bila shaka wewe utakuwa ni mmoja wa wanafamilia. Kukamilisha hitoria yake ingependeza kama ungempamba na maua yake(watoto na wajukuu)..wangapi?
 
Ndio kijiji hiko ndiko familia yake ilikotoka

Pia Geita Gold Mines kuna either Library au Lunch room iitwayo Mchauru Library kwa ukumbusho wake

Mzee ni Nyerere type ndio maana sio bilionea na ndio maana hajulikani. Hakuiba hata shillingi na anafurahia hilo sana sana. Anasema hajawai kua na tamaa ya mali wala utajiri bali yeye alipenda utumishi wa umma tu
Kipindi cha nyuma (kwenye 2007) nilikuwa nasomaga makala za viongozi wa zamani ktk gazeti la Mwananchi yaani karibia wote maisha yao yanafanana watu wa kawaida sana na kweli walikiwa wazalendo haswa.
 
Back
Top Bottom