Frederick Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu, ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,072
114,557
FREDERIC Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu, ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA – Taifa amekiambia Kikao cha Kamati Kuu jana kuwa, anampendekeza Sumaye kuwa mjumbe wa CC kwa lengo la kuimarisha chama hicho.

Amesema, dhamira ya CHADEMA ni kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi ujao, kwa kutumia kila mwanachama kufanya kazi ya uenezi.

Kamati Kuu imeridhia uteuzi wa Sumaye kuwa mjumbe wa Kamati Kuu.

Naye Sumaye amemshukuru Mbowe kwa kumteua kushika nafasi hiyo na kuahidi kukitumikia chama hicho kwa nguvu zake zote.
 
Yaa ngoja akawafundishe jinsi ya kuendesha ofisi,manake alisema nia ya kujiunga upinzani ni kuwafundisha jinsi ofisi zinavyoendeshwa.Safi sana.Hongera Sumaye wape utaalamu.Naona siasa za kupayuka na wapayikaji wakienda kudhibitiwa.Taratibu tunaiona CHADEMACCM"...na maono ya CHADEMA yakiondoshwa kwa spidi mia mbili kwenye kona.Sina neno Mzee Lowasa fanya yako! wanasema "ukinunua ardhi umenunua na vyote vilivyomo"
 
FREDERICK Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu, ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anaandika mwandishi wetu kutoka Dodoma.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema – Taifa amekiambia Kikao cha Kamati Kuu jana kuwa, anampendekeza Sumaye kuwa mjumbe wa CC kwa lengo la kuimarisha chama hicho.

Amesema, dhamira ya Chadema ni kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi ujao, kwa kutumia kila mwanachama kufanya kazi ya uenezi.

Kamati Kuu imeridhia uteuzi wa Sumaye kuwa mjumbe wa Kamati Kuu.

Naye Sumaye amemshukuru Mbowe kwa kumteuwa kushika nafasi hiyo na kuahidi kukitumikia chama hicho kwa nguvu zake zote.
piga makofi kwa mzee wa kubadilishia gia angani! masikini Haji Duni...alishiriki kuuwa CUF zanzibar ....sasa Kambare wenye masharubu wanazidi kunenepa!! tunaomba majina ya wajumbe wa kamati kuu na kanda wanazotoka kabla hatujaanza kudadavua na kujaji?
 
Hahahahahaha bado Lowasa kupendekezwa kuwa mwenyekiti! Hahahaha ho ndio wenye chama...

Aisee hiki cham kweli ni cha Mbowe..na hakuna wa kupinga kwenye hayo mapendekezo...ukipinga wewe ni msaliti! Ni wakati sasa na Sumaye akampeleka baby wake bunge!

Ina maana hiki chama hakina watu mpaka sumaye aje kuki okoa?
 
Hapo safi ataongeza ujuzi ndani ya chama, na kuwapa techniqes mbalimbali za ushindi na kupata siri za ficcm na serikali nahii itasaidia kujipanga vyema ktk uchaguzi ujao
 
Hapo safi ataongeza ujuzi ndani ya chama, na kuwapa techniqes mbalimbali za ushindi na kupata siri za ficcm na serikali nahii itasaidia kujipanga vyema ktk uchaguzi ujao
atawapa siri za ufisadi wake alipokuwa waziri
 
piga makofi kwa mzee wa kubadilishia gia angani! masikini Haji Duni...alishiriki kuuwa CUF zanzibar ....sasa Kambare wenye masharubu wanazidi kunenepa!! tunaomba majina ya wajumbe wa kamati kuu na kanda wanazotoka kabla hatujaanza kudadavua na kujaji?
Kwa upakushina tu hujambo, huo ubaguzi na ubinafsi ulionao ni hatari sana
 
Kuna wahuni humu jf wanatoa points za kishabiki na kiuongo zaidi kwa mfano huyu anayesema chama kimetekwa na Lowasa hana uhakika wowote ni uzuzu uliopitiliza. na kama tungekufahamu wewe inawezekana kuna vitu wanafaidi ndani ya CCM
 
Hivi watu mnasomaga Katiba ya CHADEMA au tunajiandikiaandikia tu.Mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ana mamlaka ya kuteua wajumbe wasiozidi 6 .Hiyo ni constitutional Right hata kama Mwenyekiti angekuwa Mwingine. Anaweza kutumia nafasi hizo kuongeza wajumbe wenye ujuzi au utaalamu na uzoefu fulani Kamati Kuu.

Lengo sio kutimiza Idadi tu ni kuongeza kitu katika consoldation ya Struggle.
 
Najua wengi CCM mnachukia na hamkupenda hawa watu wawili sumaye na Lowasa watoke huko ndo maana mnatokwa povu na hamna point ya kusimamia kilichopo mnaandika uzuzu. Hapa inatengenezwa team ondoa CCM madarakani mchwa wakubwa.
 
Huyu aliyekula mshahara na posho za pm miaka kumi leo anasema wawakufanya kitu
 
Kwa upakushina tu hujambo, huo ubaguzi na ubinafsi ulionao ni hatari sana
Haya Mimi Naanza Kuwataja ....
1) Mzee wa kubadilishia GIA Angani - HAI Moshi
2) Waziri Mkuu Mstaafu awamu ya Tatu - Manyara
3)Elly Marco Macha
 
Sioni sababu ya watu wa CCM na huko Serikalini kumwaga OMO hapa.Yaani uteuzi ndani ya CHADEMA uwatoe povu na Chozi CCM....Maumivu na maradhi ya kujitakia haya.
 
Back
Top Bottom