Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,787
- 30,080
FRED MERCURY NA MIMI NA MAGIC JOHNSON NA MIMI
Ilikuwa katika miaka ya mwanzoni ya 1990 naishi mji mmoja mdogo Uingereza unaitwa Cardiff.
Nyumba ninayoishi ni ya wanafunzi na jirani yangu anakaa gorofa ya juu yangu ni kijana wa Kigiriki anaitwa Panothiakis George Foundas.
Mdogo sana kwa umri kwangu.
Baba yake huyu kijana, Giorgos (George) Foundas ni mmoja wa waigizaji maarufu duniani katika miaka ya 1960s viwango vya Anthony Qinn na Irene Papas.
George Foundas alicheza movie, ''Zorba the Greek,'' na Anthony Quinn na Irene Papas mwaka wa 1964.
Panos kama tulivyopenda kumwita alinipenda toka siku ya kwanza aliponiona naingia nyumba ile.
Akinihurumia kuwa mimi "siishi."
Weekend niko ndani.
Siku za kawaida niko ndani.
Anashangaa kwa nini sichezi mchezo wowote wala hajaniona kwenye lile ''discotheque,'' ambalo Panos ananiambia vijana kutoka Greece muziki ukinoga wanavunja sahani.
Akanieleza kuwa hiyo ni mila ya kwao Ugiriki kuwa muziki ukikolea wanavunja sahani.
Panos ana msichana wake Mwingereza akimtembelea basi atamleta kwangu aje apige keyboard organ yangu.
Mimi na Panos tukawa marafiki wakubwa.
Siku moja jioni nasikia mlango wangu unagongwa kwa kishindo utadhani nyumba inawaka moto.
Kumfungulia Panos anaingia ndani anatweta.
"Mohamed Fred Mercury is dead."
"Who is Fred Mecury?"
Namuuliza kwa kuwa sijapata kusikia jina hilo.
Panos kachoka kuwa mimi simjui Fred Mercury ilhali kazaliwa Zanzibar na usitoshe a ajulikane dunia nzima.
Siku nyingine tena kanibishia hodi kunipa, "Breaking News," kutoka BBC taarifa za Magic Johnson kuwa kakutwa na virusi vya UKIMWI.
Nikamuuliza, "Who is Magic Johnson?"
Nina hakika hapo ndipo alipojihakikishia pasi na shaka yoyote kuwa mimi hakika sina moja nilijualo ulimwenguni.
Picha ya kwanza ni Fred Mecury akiwa mtoto na yaya wake wako Zanzibar na pcha ya pili kulia ni Giorgos Foundas baba yake rafiki yangu Panos na huyo mwingine ni Anthony Quinn.