Fred Vunjabei ni fisi aliyejivika ngozi ya kondoo

mapessa

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
611
1,042
kitendo cha Mwenyekiti wa UVCCM Heri James Kumteua Fred Ngajilo maarufu kama Fred Vunjabei kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Uchumi na Fedha UVCCM ni kulipa fadhila baada ya kusaidiwa kumaliziwa ujenzi wa nyumba anayojenga huko Mwanza.

Fred Vunjabei ni mfanyabiashara janjajanja anayetafuta nafasi ya kufanya Biashara zake chafu Bila bugudha ndani ya CCM.

Mwandishi kaka yangu Ogaro Anduru Mungu Amrehemu aliwahi kuandika kijarida kilichoitwa "Mwanaharamu", ambacho kilizungumzia namna ambavyo nchi inatafunwa na wafanyabiashara Janjajanja akina Vunjabei.

Fred anataka kujifunza umafia katikati ya Fisi wenye njaa UVCCM ya Heri James kwa leo mimi namtazama Fred kuwa kuwa ni kiini cha uporaji mkubwa wa rasilimali za nchi unaotaka kufanyika kupitia kivuli cha UVCCM.

Fred ni mbunifu mkuu na nahodha wa mikakati ya biashara nyingi haramu chini ya mwamvuli wa Vunjabei Group of Company.

Baada ya kufanikisha mipango mingi ya kuchukua tenda ya Jezi kwa timu ya Simba sasa anaitaka UVCCM katika jaribio jingine la kumiliki sehemu ya Chama.

Wameshindwa kuikamata Serikali, ya Mama Samia Suluhu ambayo kwasasa haitabiriki baada ya Mama kuvunja Idara nyingi za mifumo ya Usalama sasa wanataka kutumia fursa ya UVCCM kukamata Vijana na baadae Chama kwa Ujumla.

KWANINI UVCCM

- UVCCM ni sehemu ya Idara ya Jumuiya ya chama cha Mapinduzi yenye idadi kubwa ya Wanachama Na sehemu ya wajumbe wake ambaye ni mwenyeweketi ni mjumbe wa kamati kuu. Kazi ya UVCCM ni kutoa ushauri kwa serikali na kuisimamia Serikali kutekeleza mipango yake ya maendeleo, ukiwa na UVCCM hasi yenye njama baina ya Mwenyekiti na Wajumbe kadhaa, watakuwa na nafasi kubwa na ya kipekee ya kuhujumu utendaji wa serikali.

-Nguvu ya Kimamlaka ambayo
Mwenyekiti wa UVCCM anayo kulingana na Katiba ya chama … Mwenyekiti ni mtu ambaye anaingia kwenye Mikutano mikubwa ya chama hasa katika Kamati kuu ya CCM. Ukiwa na Mwenyekiti aina ya Heri James ambaye amekuwa akijinadi ni Magufuli Forever na watu wanaoingia vikao nyeti vya kujadili ‘’Siri kuu ya Chama’’ wasipokuwa watiifu ni hatari kwa Uhai wa chama.

MAHUSIANO YA HERI JAMES NA FRED NGAJILO (FRED VUNJABEI).

Kwa lugha ya kawaida, wawili hawa ni familia, ni ndugu walio na mahaba ya ndani kabisa baina yao. Undugu wao una historia ndefu, lakini kwa ufupi wake tuanzie katika kile kilichoitwa “MTANDAO” Uenyekiti wa Heri James UVCCM 2017 uliratibiwa na mtandao chini ya ufadhili wa Fred Vunjabei.

Fred Vunjabei amepiga hesabu kwenye Jengo la UVCCM Tower Na majengo mengi ambayo ataweza kufanya uwekezaji bila tabu maana akipoulizwa Heri James Kwanini Fred Vunjabei aliwajibu Wajumbe kuwa Chama kinahitaji mtu madhubuti katika nafasi ile je ni Fred mwenye nguvu hiyo ya kulinda mali za UVCCM ama kuzitafuna mali za UVCCM.

-•CCM inatajwa kuwa ni chama kinachosimamia misingi yake na chenye kujisahihisha kila pale kinapogundua kuwa kilifanya makosa yenye kukigharimu. CCM ilifanya makosa mengi huko nyuma kosa kubwa lilikuwa ni kitendo cha kuruhusu kuishi na NYOKA.

Ni kosa kwa Chama kuruhusu vitoto vya Nyoka kuanza kumea upya ndani ya Chama hicho.

Zaidi, soma:
- Fred Vunja Bei ateuliwa kuwa Mwenyekiti kamati ya Uchumi na fedha UVCCM Taifa
 
kitendo cha Mwenyekiti wa UVCCM Heri James Kumteua Fred Ngajilo maarufu kama Fred Vunjabei kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Uchumi na Fedha UVCCM ni kulipa fadhila baada ya kusaidiwa kumaliziwa ujenzi wa nyumba anayojenga huko Mwanza...
Mfumo huu tulionao wa kisekula na mwanae ubepari unamruhusu ndugu Fred kwenda far miles
 
kitendo cha Mwenyekiti wa UVCCM Heri James Kumteua Fred Ngajilo maarufu kama Fred Vunjabei kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Uchumi na Fedha UVCCM ni kulipa fadhila baada ya kusaidiwa kumaliziwa ujenzi wa nyumba anayojenga huko Mwanza...
Mkuu habari za umbea hazifai

Hakuna sababu ya msingi uliyoitoa

Biashara ni za kwake Fred na hajaanza Leo biashara

Huyo ni mkinga, Mbona maduka yote kariakoo kwa sasa wanamiliki wakinga

Wakinga wa sasa ni tofauti, Hapo kati wakinga baada ya kuwa matajiri wamepeleka watoto wao shule wawasaidie

Hao akina Fred ni zao la wakinga wale wa zamani ambao walikuwa matajiri lakini hawakusoma

Wakinga wa kariakoo sasa ni kizazi kipya hata kama wanatumia uchawi lakini wapo vizuri kichwani

Fred ni mkinga na mfanyabiashara, Mbona huongelei ndugu zake pale kariakoo?

Tuendako wakinga nao wataingia Bungeni ku influence agenda zao za biashara.

Ni muhimu wizara ya Afya ikasimamiwa na Dakatari wa afya

Ni muhimu kazi ya Fedha ikasimamiwa na mfanyabiashara

Tatizo zamani hiyo kazi walipachikwa watu wenye vyeti lakini hawajawahi hata kufanya biashara ya kuuza pipi kifua
 
Mapesa una chuki na huyo mkinga huyo mkinga ni mtaalamu aliyesomea aliyekaa darasani akasoma kuhusu usimamizi wa pesa kasome cv yake kama ameweza simamia biashara zake na zikasimama vizuri kwann asipewe nafasi ya kusimamia mali za chama chake.

Heri akuwahi kushinda kinyanganyiro alikuwa ni mtu wa tatu sema alishinda kwa amri ya mjomba wake Ili kukamilisha kitu kiitwacho sukuma gang kushika kila idara.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom