MISHAHARA- walimu 200000/= - Madaktari 957000/=+marupurupu kidogo - Wabunge 2700000/=+ Shangingi+allowance nyingi SABABU- Walimu ni wengi kuliko madaktari na madaktari ni wengi kuliko wabungeMIKOPO VYUO VIKUU-wanafunzi sayansi -FIRST PRIORITY (100%) - wanafunzi wengine-NON PRIORITY (unreliable) SABABU -Tuna wanafunzi na wataalamu wachache wa sayansi kuliko wengineITIKADI YA TAIFA- Ubepari (Capitalism) ni mzuri kwa maendeleo yetu hasa ubinafsishaji na uwekezaji kutoka nje. Ujamaa ( Socialism) umepitwa na wakati na hautufai kwa nchi yetu ambayo wengi wetu ni wavivu. SABABU- Ubepari rasilimali nyingi huwa mikononi mwa wachache lakini Ujamaa rasilimali ni za woteMITAZAMO YA WATU- watu wachache: Tanzania ni nchi yenye maziwa na asali watu wengi : Tanzania ni kana jangwani kusikokuwa na maji,chakula wala matumaini yoyote. watu wachache: Tunajivunia kuwa watanzania watu wengi : Tunavumilia kuwa watanzania UKWELI -mkiwa wachache mtanufaika lakini mkiwa wengi mtajuta MTAZAMO WANGU-walimu wangekuwa wachache kuliko wabunge wangelipwa mishahara mikubwa kuliko wabunge SWALI- Je, mlio katika kundi la watu wengi mnaweza kuamia kwenye kundi la watu wachache hili na nyinyi mnufaike?