Fred Mpendazoe: Uchumi wa nchi umo mikononi mwa familia tisa za matajiri! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fred Mpendazoe: Uchumi wa nchi umo mikononi mwa familia tisa za matajiri!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makaayamawe, Mar 26, 2009.

 1. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Godfrey Dilunga | Raia Mwema | Machi 18, 2009

  MACHI 12, mwaka huu, Mwandishi Wetu Godfrey Dilunga alifanya mahojiano na Mbunge wa Kishapu (CCM), Fred Mpendazoe kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa. Mahojiano hayo yalifanyika jijini Dar es Salaam na yafuatayo ndiyo yaliyojiri.

  Swali
  : Watalaamu na wananchi wanaonya kwamba matabaka yanazidi kuimarika na pengo kati ya masikini na matajiri linazidi kuimarika. Unakubaliana na mtazamo huo?

  Jibu
  : Ni kweli kumeanza kuibuka matabaka mbalimbali katika jamii yetu na chanzo kikubwa ni uporaji wa uchumi unaofanywa kwa njia mbalimbali za ufisadi.

  Swali
  : Umezungumzia kuibuka matabaka mbalimbali ni yapi hayo?

  Jibu: Kwa sasa matabaka manne yanaibuka na kuzidi kuimarika kila kukicha. Tabaka la kwanza linaundwa na matajiri. Tabaka hili linaweza kumiliki sehemu kubwa ya uchumi wa nchi kwa njia ya ufisadi…kwa Lugha ya Kigiriki tabaka hili linaitwa Oligaki.

  Inasemekana uchumi wa Tanzania kwa sasa unamilikiwa na familia tisa za matajiri. Hizi familia tisa zinaweza kutoa fedha ya kuendesha nchi.
  Tabaka hili la oligaki linatengeneza tabaka la pili ambalo ni tabaka la wateule wanaojiona bora kwenye jamii kwa Kigiriki linaitwa Aristokrasi.

  Oligaki wataweka watu wao kwenye sehemu muhimu na nyeti kwa ajili ya kulinda maslahi yao kwa mwavuli wa maslahi ya Taifa, mfano benki, wizara nyeti (fedha) na kwenye ofisi za mabalozi za nje. Wanaowekwa katika sehemu (ofisi) hizo ndiyo wateule, yaani aristokrasi


  Tabaka la tatu ni la watu wenye tamaa ya madaraka kwa Kigiriki tabaka hili huitwa Timokrasi. Hili ni tabaka linaloundwa na wanafiki wanaounga mkono hoja za oligaki (matajiri) na aristokrasi (wateule wa matajiri) kwa ajili ya kupewa chochote ili waseme lolote.


  Timokrasi ni watu wasio na msimamo wowote kwani wametawaliwa na tamaa na makuu, hivyo ni rahisi kuwasaliti wananchi.


  Tabaka la nne ni la wananchi wanaoishi kwa matumaini ya kupata maisha bora ambayo ni vigumu sana kuyapata kutokana na kuimarika kwa tabaka hizi.


  Swali
  : Kwa mujibu wa maelezo yako, uendeshaji wa siasa, uchumi na masuala mengine nyeti kwa Taifa umekwishaingiliwa?

  Jibu
  : Kwa sasa ni dhahiri wapo wananchi wachache matajiri sana na wapo wananchi wengi masikini kwenye nchi hii yenye utajiri mkubwa wa rasimali. Na chanzo kikubwa cha hali hiyo ni ufisadi kama alivyosema Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba, mwaka 2000, kwamba pengo kati ya matajiri na masikini limeongezeka, na siasa imetekwa na matajiri. Ufisadi na rushwa vimekuwa muhimu kwenye chaguzi.

  Naomba nimnukuu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere juu ya ufisadi na matokeo yake ambayo ni kuibuka kwa matabaka. Alisema; "Utajiri katika Tanzania unaweza kupatikana kutokana na rushwa kwa watumishi wa umma au kutokana na wafanyabiashara ambao wanawania nafasi za kisiasa ili wawe wadeni wa Rais aliyeko madarakani."


  Tafsiri ya maneno haya ni kwamba anaweza akapatikana Rais kwa kugharimiwa na matajiri na akiwa madarakani itabidi alipe fadhila kwa matajiri waliomfadhili yeye na chama chake wakati wa uchaguzi. Zipo dalili kwamba haya yameanza kutokea.


  Swali
  : Je, ni nini madhara zaidi ya kuibuka kwa matabaka haya nchini?

  Jibu
  : Kutokana na mwenendo unaoendelea kwa sasa wa kuibuka na kuimarika kwa matabaka, unaotokana na uongozi kununuliwa kwa fedha, matokeo yake ni nchi kuwekwa rehani kwa matajiri kama alivyosema Rais Jakaya Kikwete.

  Na nchi kuwekwa rehani kwa matajiri ni jambo hatari sana, maana yake serikali itaongozwa na matajiri na hivyo haitawajibika tena kwa wananchi na demokrasia itakoma na udikteta utaanza.


  Serikali haitakuwa ya watu na kwa maana hiyo haitachaguliwa na watu na haitawajibika kwa wananchi. Matajiri wataamua nani awe rais, nani wawe wabunge kwenye majimbo.


  Wananchi hawatachagua madiwani wanaowataka. Baadaye matajiri wataamua nani awe waziri, jaji na wakuu wa vyombo vya dola ili kuhakikisha maslahi yao yanalindwa sehemu zote kwa mwavuli wa maslahi ya Taifa.


  Na zipo dalili za kuelekea huko. Serikali inapochelewa kuchukua hatua haraka juu ya ufisadi unaotendeka si dalili nzuri. Nakubaliana na mtaalamu wa Hisabati na Mwanafalsafa, Albert Einstein, aliyesema kwamba ulimwenguni pamekuwa mahali pa hatari sana kuishi, lakini haitokani na ufisadi unaofanyika, bali inatokana na wale wanaouangalia tu uovu ukifanyika na hawachukui hatua yoyote.


  Swali
  : Kutokana na maelezo hayo ya Albert Einstein, Tanzania patakuwa mahali hatari pa kuishi?

  Jibu
  : Kulingana na Einstein, Tanzania patakuwa mahali hatari kuishi, lakini haitokani na ufisadi unaofanyika bali inatokana na serikali kuchelewa kuchukua hatua madhubuti juu ya ufisadi unaofanyika. Ni muhimu serikali kuchukua hatua mapema dhidi ya ufisadi unaofanyika.

  Swali
  : Katika moja ya vikao vya Bunge nakumbuka katika moja ya michango yako uligusia suala la kuwa na Katiba mpya. Je, Katiba ya sasa ina upungufu gani?

  Jibu
  : Katiba ni sheria kuu ya nchi, ni sheria mama ya sheria zote nchini kwa kuwa inagusa nyanja na mifumo yote ya utawala wa nchi kisiasa, kiuchumi na kijamii. Maliberali wenyewe wanasema Katiba ni ramani ya madaraka ya nchi inayoonyesha jinsi mamlaka ya nchi yanavyopaswa kusimamiwa na kuratibiwa ndani ya vyombo vya utawala.

  Kutokana na ufafanuzi huu, maoni yangu ni kwamba mfumo wa utawala tulionao unaotokana na Katiba hautoi fursa kwa watendaji kuwajibishana bali unatoa nafasi kubwa ya kulindana.


  Ni mfumo wa viongozi kulindana badala ya kuwajibishana inapobidi.


  Swali
  : Umesema ni mfumo wa viongozi kulindana badala ya kuwajibishana. Sababu gani zinazoambatana na maelezo yako hayo?

  Jibu
  : Katiba yetu inatambua mihimili mitatu, Bunge, Serikali na Mahakama. Bunge kwa niaba ya wananchi linaisimamia serikali na kutunga sheria, Mahakama inatafsiri sheria na serikali inatekeleza mipango na sera zilizopitishwa na Bunge kwa kufuata sheria za nchi.

  Kwa maoni yangu, ili Bunge liweze kuisimamia vizuri serikali ilipaswa taasisi kama TAKUKURU, Usalama wa Taifa, Tume ya Haki za Binadamu na Tume ya Maadili, watendaji wakuu wake wateuliwe na Rais, lakini waidhinishwe na Bunge na wawajibike bungeni kupitia Kamati za Kudumu za Bunge.


  Kwa sasa watendaji wakuu wa taasisi hizi huteuliwa na Rais na wanawajibika kwake. Kutokana na mfumo huu ni vigumu sana watendaji wakuu hawa wakatoa taarifa ambayo itaikosoa serikali na ikubalike.


  Utendaji kazi wa wakuu wa taasisi hizi hauwezi kuwa huru, bali utailinda serikali isionekane imeshindwa. Mfumo huu tuliourithi ni wa kulindana.


  Kulingana na Katiba yetu, mawaziri wanatokana na wabunge. Katiba inaeleza kazi ya mawaziri ni kumshauri Rais, lakini wametokana na wabunge wanaoisimamia serikali na wao ni sehemu ya Bunge.


  Swali
  : Katika mazingira haya, nafasi ya Bunge ikoje katika suala la kutimiza wajibu wake?

  Jibu
  : Hapa ni kwamba usimamizi wa Bunge unapunguzwa nguvu, unaegemea zaidi kwenye ushauri usioilazimisha serikali kutekeleza iliyoagizwa. Mfumo huu unasababisha mvutako kati ya Bunge na Serikali na matokeo yake ni kupoteza muda na kuchelewesha maendeleo. Ni vema mawaziri wasitokane na wabunge.

  Swali
  : Mgongano huo wa madaraka pia umo katika siasa. Rais ndiye mwenyekiti wa chama tawala, ambacho kina jukumu la kuisimamia serikali anayoiongoza. Hili unalizungumziaje?

  Jibu
  : Katika vyama vya siasa, nashauri Rais asiwe pia mwenyekiti wa chama tawala. Chama kinaposhinda uchaguzi kazi yake kubwa ni kuhakikisha ilani ya uchaguzi ya chama inatekelezwa ipasavyo na serikali yake. Hivyo chama huisimamia serikali.

  Mfumo tulionao, Rais ndiye mwenyekiti wa chama. Hivyo asipotekeleza vizuri ilani ya uchaguzi, hakuna kikao cha kumwajibisha.


  Kama ni Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama yeye ni mwenyekiti, atawasilisha taarifa ya utekelezaji kwa chama kama Rais, baadaye wajumbe wa NEC wataijadili yeye akiwasikiliza kama mwenyekiti wao.


  Ni mfumo wa kulindana si kuwajibishana. Na mawaziri wengi hugombea ujumbe wa NEC, hivyo waziri wa sekta atawasilisha taarifa ya sekta yake na yeye ataijadili kama mjumbe wa NEC na ikumbukwe waziri ni mshauri mkuu wa Rais katika sekta husika.


  Hapa kuwajibishana si rahisi. Hali hii ipo mpaka ngazi ya kijiji. Vijijini, wajumbe wa serikali ya kijiji pia wengi huwa ni wajumbe wa halmashauri ya chama tawala. Kwa hiyo halmashauri ya chama tawala ya tawi haiwezi kuiwajibisha halmashauri ya serikali ya kijiji kutokana na kwamba unaweza ukakuta wajumbe wa halmashauri ya tawi ya chama tawala pia ni wajumbe wa halmashauri ya serikali ya kijiji. Watalindana, lakini matokeo yake hakuna maendeleo.


  Taarifa za vikao hivyo huwa ni nzuri na hupigiwa makofi sana, lakini maendeleo hakuna. Ipo haja ya kubadili mfumo.


  Swali
  : Kuna malumbano kuhusu ruksa ya Katiba katika kumshitaki Rais aliyestaafu ambaye amebainika kufanya makosa. Hili unazungumziaje?

  Jibu
  : Ibara ya 46(2) ya Katiba inasema; "Rais mstaafu hawezi kufikishwa mahakamani kwa kosa la jinai alilolitenda wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais.

  Kuna haja ya kuiangalia Katiba yetu ili tujihakikishie kwamba ina nguvu za kutosha kuilinda nchi yetu dhidi ya viongozi au Rais mchaguliwa ambaye anaweza kuamua kupora au kuruhusu uporaji wa uchumi wa nchi.


  Uporaji wa uchumi wa Taifa letu unaofanywa na unaoweza kufanywa na watu wachache unatakiwa kudhibitiwa kikatiba kama tunataka nchi isalimike. Hali ya uovu inapoongezeka ndivyo tunapohitaji Katiba imara zaidi na sheria kali.


  Mwanafalsafa Plato anasema hivi juu ya kuwapo sheria; "Watu wema hawahitaji kuwapo sheria kwani wao huishi na kutenda kiungwana, wakati watu waovu siku zote hutafuta namna ya kuzizunguka sheria."


  Swali
  : Nini maoni yako kuhusu mjadala wa ununuzi wa mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Dowans?

  Jibu
  : Naunga mkono maoni yaliyotolewa na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, William Shellukindo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, na Makamu wake, Dk. Harrison Mwakyembe. Nasisitiza mambo matatu.

  Mosi, Kama Serikali ingekuwa imetekeleza maazimio ya bunge yanayohusu kuwawajibisha watendaji wa Tanesco na Wizara ya Nishati na Madini waliojihusisha na kuishauri vibaya serikali kuhusu mchakato wa Richmond, haya yalitokea yasingetokea.


  Walioishauri serikali wakati wa Richmond ni wale wale wanaoishauri serikali juu ya mitambo ya Dowans iliyokuwa ya Richmond. Hawajawajibishwa, wapo kwenye nafasi zile zile. Kilichofanyika ni kutaka kujisafisha na kashfa ya Richmond. Ni muhimu serikali iwawajibishe watendaji hao.


  Pili, suala alilotahadharisha Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco kwamba nchi inaweza kuingia giza kwa kutonunuliwa mitambo ya Dowans, Watanzania walichukulie kwa uzito wake.


  Inawezekana kweli nchi ikawa giza na kupata athari kubwa kijamii na kiuchumi kwa kukosa umeme, lakini si kwa kukosa kuinununua mitambo ya Dowans bali ni kwa hujuma au uzembe wa Tanesco.


  Nilitarajia Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco alipoona hoja yake haikukubalika angejiuzulu. Hajajiuzulu, basi, serikali itafute mkurugenzi mwingine mwenye maono mapya anayeweza kupata mipango mbadala wa Dowans.


  Swali
  : Kuna hatua zozote za ziada zinazoweza kuchukuliwa na Bunge na hata kwa upande wako?

  Jibu
  : Upo uwezekano kupeleka bungeni hoja binafsi kutaka viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini wawajibishwe kwa kuiacha Tanesco iendelee na suala la Dowans. Na serikali ifahamu Bunge linaisimamia kwa niaba ya wananchi.

  Hizo familia tisa ni akina nani?
   
 2. Lusajo

  Lusajo JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 451
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Na yeye mhe. Fred Mpendazoe yuko kundi gani? na huyo mwandishi Godfrey Dilunga mbona hakumbana kuhusu majina au anaongea mambo ya kufikirika? kama kasema kuna Familia tisa maana yake anazijua mbona hajazitaja? ni bora asingetaja hata namba maana hapo anaonekana anazijua na hakuzitaja na sikuona mwandishi akiuliza swali la mhe .kuzitaja hizo familia.
   
 3. c

  chibingo Member

  #3
  Mar 26, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 45
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Definitely ni among the '' 50 People Who Are Screwing Up Tanzania'' walioorodheshwa kwenye thread iliyopita
   
 4. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hawa waheshimiwa wanafikiri wataondoa umaskini wa Tanzania kwa kukimbilia kwenye vyombo vya habari kuwalaumu wengine. Dawa ni kwa wao kurudi kwenye majimbo yao na kushirikiana na wananchi wao kutengeneza mazingira ambayo yatawaongezea kipato chao.

  Uchaguzi unakaribia na tutasikia mengi sana mpaka kufikia 2010. Kuna wabunge wengi wanafikiri kwa kupiga kelele kwenye vyombo vya habari basi wananchi wao watawaona wao wanapigania maslahi ya wananchi. Ukweli ni kwamba wengi wao wameshindwa ku deliver kwenye majimbo yao na sasa wanatumii hii karata kama njia ya mwisho ya kujiokoa ili wasitupwe 2010.
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ... then wanakwenda dinner
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Jamaa alikuwa Mkurugenzi NEMC sehemu chombo chenye heshima kubwa kusimamia mazingiza Tz..akaacha akenda ktk siasa!

  Nadhani kuna haja kupunguza malipo na marupurupu ya wabunge ili tusiendeelee kupoteza wataalau wetu kwa taifa maskini na kukimbilia ktk siasa!
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,336
  Likes Received: 1,803
  Trophy Points: 280
  Jamani nifamisheni ni zipi hizo familia tisa anazozisema Mheshiwa mana sijawahi kufikiria kama kuna kitu kama hiki Tanzania. Nimesikia Italy, more especially Sicily mambo kule yanaendeshwa kifamilia familia.Familia zenyewe huwa ni za kimafioso.
   
 8. Mkereketwa

  Mkereketwa JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2009
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hi,

  Hapo ameeleza analysis ya uchumi unavyokuwa ndani ya nchi kinadgaria na siyo kuwalenga wale wanaomiliki uchumi physically kama ambavyo tungedhania.

  Woop!!!
   
 9. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hello fellows! Hivi hawa jamaa wanapohojiwa kwanini huwa hawatoi taarifa zilizo kamilika? Au wameamua kuja kutuchanganya? Maana mimi najua kuwa ukiesema familia tisa means unazijua! Na inatakiwa uzitaje! Sasa ukisema tu bila kutaja majini hapo ina maana habari yako haijakamilika.

  Mimi nafikiri sasa inabidi hawa jamaa wakiojiwa kama awatoi maelezo ya kueleweka ni vizuri hizo habari zikaachwa maana hazina kipya zaidi ya kuongeza maswali yasiyo na majibu.

  ATAJE MAJINA SIYO KUTUTAJIA NAMBA TU? ATOE NA VIDHIBITISHO KUONYESHA AMETUMIA NINI MPAKA KUFIKIA KUSEMA HIVYO....
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  The core is true, the rest is hoopla, hogwash, a bagful of hot air!

  Complete with a host of unwarranted Greek etymologies to make up for credibility.
   
 11. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi naona hakuna haja ya mtu yeyote kuwa kwenye kundi lolote ili kusema ukweli kuhusu jambo unaloliamini. Pamoja na wengi humu JF kuwa na misimamo inayofanana, haina maana wako kwenye kundi moja. Mtu anaweza kufanya tathmini yake mwenyewe na kumuweka Mheshimiwa Mpendazoe kwenye kundi analoona linamfaa. Nadhani kwa maelezo yake, ni rahisi kufanya hivyo.

  Vile vile, tumekuwa tukishutumu sana tabia ya baadhi ya viongozi kutaja majina ya watu (tukisema wamekuwa personal). Sasa kama huo ndio msimamo wetu na unaotokana na principles zetu, kwanini tunataka Mheshimiwa huyu aanze kutaja majina ya watu? Ama tunataka awe personal kwa watu hao kwa kuwa yeye ni tofauti na wengine? Nini hasa sababu ya kutaka huyu awe personal, na yule asiwe personal?
   
 12. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mkandara, ni kweli kwamba waheshimiwa hawa wanatakiwa kufanya juhudi zaidi ya maendeleo kwa kushirikiana na wananchi wao.

  Swali langu ni je, wanapokuwa wamefanya hivyo, hawana haja ya kuongea na waandishi wa habari hata kama waandishi hao wamependa kujua maoni yao kuhusiana na issues wanazotaka kujua kutoka kwao?

  Alichofanya Mbunge huyu ni sahihi na ni kizuri sana. Ameonyesha msimamo, ufahamu na ametoa mtazamo wake kuhusiana na mambo muhimu aliyoulizwa. Ameyajibu vizuri sana.

  Mambo mengi ni kweli kuwa yakifanyika kama anavyosema, nchi inaweza kupiga hatua katika za uhakika na kuleta tija kwa Taifa. Kauli hizi zinaweza kuleta changamoto mpya katika kuchukua maamuzi mazuri kwa Taifa, na ni jambo jema nadhani kuliko yeye kwenda na kushirikiana tu na wananchi wake kutafuta maendeleo ambayo ni ya kukisiwa zaidi ya maendeleo ya kweli.

  Maoni haya yakifanyiwa kazi, maendeleo yatakayopatikana ni ya kweli kuliko maendeleo yoyote yaliyokwisha patikana hadi sasa. Tatizo letu ni la kimfumo na hilo ni tatizo kubwa sana. Tutakuwa tukipiga kwata tu kama hatubadilishi mfumo wetu wa uongozi.
   
 13. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  The Rupias, Mkapas, Bakhresas, WAburushi wale RA et al., The Zanzibari Sultanate:House of KARUME, The Mwinyis, JK-hayupo sema by 2015 atakuwa 11th sema tuu hana watoto wenye akili..lol... ENDELEzeeni.. Marealles (definitely aristocratic family:sijui wakoworth how much at the moment though),................. Kinachenge ndio wateule wa wenyewe wenye nchi yao... The Kenyattas of TZ.
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Inabidi tuwe specific, kama tunataka maendeleo tunataka tuwe personal, ikibidi.

  Kinachoharibu nchi yetu ni principles mbovu no doubt, lakini kama hizi principles zinakumbatiwa na watu, na hawataki kuziacha, kwa nini tusi wa call out?

  Mara nyingine huwezi ku separate the person from the principle, especially if the person himself does not want to separate himself from the principle. Hatuwezi kuishi katika utopia ya kusema "tunawapenda mafisadi lakini hatupendi ufisadi" wakati mafisadi hao hawataki kuachana na ufisadi.

  Mara nyingine, ili kutoa cancer isienee katika mwili mzima, inabidi ukate kiungo.Hii ni kwa sababu huwezi kuzitenganisha cells zenye cancer na cells nzima.Vivyo hivyo katika case ya watu wenye principles mbovu ambao hawataki kuachana na principles hizi.

  Unawa blast live tu, I thought we dared talk openly here, so whats this I hear about not getting personal?
   
 15. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Kiranga, Mimi nakubaliana na wewe kabisa katika hayo.

  Ila sikubaliani tukiwa na double-standard katika principles hizo. Juzi juzi tu hapa JF kuna baadhi ya watu ambao walipinga na kulalamikia uamuzi wa Dr. Mwakyembe kutaja jina la mtu anaemtuhumu kumchafulia jina. Watu hao waliona kuwa haikuwa uungwana kwa Dr. yule kufanya hivyo. Iweje leo, iwe tofauti? Ama kila jambo na wakati wake na watu wake?
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Kama vile uchumi wa USA ulivyo chini ya familia 500 tu, huku ikiwa na wananchi millioni 400, sisi millioni 40 familia tisa, au?
   
 17. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #17
  Mar 26, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  In that case, the outrage should be on why did Mwakyembe not name names. I also deplore double standards, but what I deplore more than double standards is the habit of lowering high standards toward low standards in order not to have double standards.

  Kama tunataka "Ukweli na Uwazi" na tulishaukubali under magirini ya Mkapa kwa nini kufichana fichana?

  Kama issue ina warrant watu kutajwa watajwe tu, na mimi nafikiri kusema "uchumi unaendeshwa na familia tisa tu" bila kuzitaja ni irresponsible, kwa sababu una fuel speculations.Sasa kila mtu aliye katika top echelon ya business na politics anaanza kuzungumziwa, Je ni Bakhresa? ni Rostam? ni Mengi? majina yatazidi hayo tisa aliyosema muheshimiwa na wengine watanaswa na mtego wa panya.

  Waandishi wetu hata hawajamuuliza amepata wapi hizi data? Familia hizo tisa ni zipi na zinawezaje ku control uchumi hivyo? Kihalali au isivyo halali?

  Unakuta mtu ana quote Greek gods wote Aristotle, Einstein na sijui nani pamoja na etymologies za Greek rooted words, lakini anashindwa kuelezea kitu so central, au hata kusema "siwezi kutaja majina kwa sababu hii na hii".Kauli mtu bado issue, journalistic integrity na competencu bado issue.
   
 18. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #18
  Mar 26, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  And they are the ones effin up our country.
   
 19. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Kwani is there a problem uchumi wa taifa kushikiliwa na familia 9 tu, au kuna more than that statement?
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Mar 26, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Hakuna cha watu tisa wala nini kushikilia uchumi wa nchi. Hii ni attempt ya kuwafanya au kujifanya kujisikia au kujiona uko wa muhimu. Hawana lolote hao. Ni watu wengi tu wanaochangia katika uchumi na sio wachache.
   
Loading...