Fred Mpendazoe amejiondoa CHADEMA?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,481
Papa Pamoja na Mkulima ni Bora Kuliko Papa Pekee. Lakini....

Wanasaikolojia na wanasayansi ya Jamii wanatukumbusha Kwamba, kila mtu ana haki na maoni yake. Na Kwa vile hakuna watu wenye maoni yanayofanana kabisa, Kwa hiyo hakuna watu wawili wanaofikiri sawawa.

Aida, Mwanasaikolojia Eric Brumethal anasisitiza Kwamba, Kila binaadamu anayo haki ya kujenga mitazamo yake binafsi, kwani hata mapacha wanatofautiana Kwa hili. Hivyo, wakati unapotoa maoni yako au kukundi kimoja kinapotoa maoni yake, no muhimu kukumbuka ukweli Kwamba, unapodhani upo sahihi au kikundi chenu kiko sahihi haina maana una haki ya kupuuza maoni ya wenzako na kuwakemea hadharani.
Napenda kutoa maoni yangu kulingana na hatua zilizochukuliwa na UKAWA na maoni yao kuhusiana na hatua ambazo serikali inachukua katika kuondoa changamoto zinazoikabili jamii.

Katika Nchi zenye mfumo wa vyama vingi, vyama vya siasa huwa na itikadi zinazotofautiana. Na sababu ya msingi sana iliyosababisha Nchi kuamua kuwa na vyama vingi vya siasa ni Kwamba, ulinganifu wa maoni hukinza au huzuia ustawi na maendeleo. Kutokana na sababu hii watu wawili au vikundi viwili vinapaswa kufurahia kuwa na mitazamo tofauti, Kwa vile cheche ya maendeleo huanza pale mitazam miwili inapogongana. Au maana yake Nchi ambazo zina vyama vingi, kasi ya maendeleo ni kubwa ikiwa vyama vya upinzani in imara.
Lakini, Migongano ya mitazamo isiwe ya kiuadui bali iwe in fursa ya nzuri ambapo kila mmoja au chama kinapata nafasi ya kyjifunza kutoka kwa mwenzake.

Mwanafalsafa mmoja aliwahi kusema, "Papa pamoja na Mkulima ni bora kuliko Papa pekee. Maana yake hakuna mtu anayejua kila kitu, na hakuna mtu aliye bora kuliko mwenzake Kwa kila kitu. Papa anatarajiwa kuwa anajua mambo Mengi sana lakini akiongezeka hats mtu mmoja anaweza kuwa na tasrifs au wazo ambalo Kwa Bahati mbaya Papa hana. Na katika siasa, chama tawala kinahitaji mawazo kutoka upinzani. Lakini upinzani uwe ukitambua mazingira yapi chama tawala kitapokea maoni ya upinzani.

Huwezi ukamtukana jirani yako asubuhi halafu unaenda kwake kumpa ushauri jioni. Jirani huyo akiwa muungwana atakykaeisha lakini hatakusikiliza. Upinzani unatakiwa ujenge mazingira na chama tawala yatakayowawezesha kukaa pamoja na kushauriana.
Utaratibu au mbinu ya kushinikiza Kwa maandamano tija yake ni ndogo sana na huchukua muda mrefu na huumiza watu wengi na no mbinu ya kiharakati.
Aidha, hoja za upinzani ziwe wazi: Mfano, suala la demokrasia.Watanzaia wanatakiwa wajue demokrasia ndani ya CHADEMA bado ni changa.

Mwaka 2009, Zitto aliwekewa mizengwe alipotaka kugombea uwenyekiti na mwaka 2014 nafasi ya Mwenyekiti ilikuwa na mizengwe. Nafasi ya makamu Mwenyekiti ilikuwa na mizengwe pia. Uteuzi wa viti maalum ulikuwa mbovu . Sasa upinzani unapozunguka na ajenda hii ya kudai demokrasia haina maana. Ajenda nyingine wanayoitaja ni Ufisadi. Serikali ya CCM imeonyesha matumaini. Upinzani wenyewe wamevuruga Kwa kuwatetea mafisadi. Ajenda ya Ufisadi Kwa upinzani hawana tena. Nadhani CHADEMA wanatetea maslahi yao siyo ya watanzania waluo wengi.

Mfumo wowote hauwezi kukosa makosa yawe ya kiutendaji au usimamizi. Lakini ni Kweli serikali ya JPM imejitahidi sana, nilitegemea upinzani utafute kukaa na chama tawala ili kutafuta namna ya kupata katiba mpya na mambo mengine ya msingi kuliko maandamano bila kikomo.
Papa pamoja na Mkulima ni bora kuliko Papa pekee, lakini Mkulima atambue na kumheshimu Papa. Tutafakari.

Fred Mpendazoe
 
Ah hahahahaaaa kweli mninga noma,
hadi suruali inatoka viraka vya matako lazima utii
 
Ukiangalia hapo kwenye RED ni hakika Mpendazoe hayupo pamoja na Chadema na Upinzani.

.......... Aidha, hoja za upinzani ziwe wazi: Mfano, suala la demokrasia. Watanzaia wanatakiwa wajue demokrasia ndani ya CHADEMA bado ni changa.
.......... mwaka 2014 nafasi ya Mwenyekiti ilikuwa na mizengwe. Nafasi ya makamu Mwenyekiti ilikuwa na mizengwe pia. Uteuzi wa viti maalum ulikuwa mbovu . Sasa upinzani unapozunguka na ajenda hii ya kudai demokrasia haina maana. Ajenda nyingine wanayoitaja ni Ufisadi. ...............Upinzani wenyewe wamevuruga Kwa kuwatetea mafisadi. Nadhani CHADEMA wanatetea maslahi yao siyo ya watanzania waluo wengi.
Fred Mpendazoe
 
Hayo Mpendazoe aliyohainisha yalikuwepo kabla ajajiunga na Chadema. Kwanini sasa hivi ndio tatizo?
 
Upinzani usivyopenda kukoselewa.. Wenyewe kwa wenyewe.. Naona Mpendazoe leo ataitwa majina yote.. Mpendazoe ndio yupo hivi.. Aliwai mkosoa JK kipindi.. Mpendazoe bado ni mbunge wa kishapu(CCM)2005-2010,
Juz wapinzani walimsifu Bashe kwa kukosoa serikali ya CCM. Upinzani kweli Vimbwanga
 
Back
Top Bottom